bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Ezekiel 21
Ezekiel 21
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 20
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 22 →
1
Neno la Bwana likanijia la kwamba:
2
Mwana wa mtu, uelekeze uso wako kuutazama Yerusalemu, upatangazie Patakatifu na kuifumbulia nchi ya Isiraeli yatakayokuwa!
3
Iambie nchi ya Isiraeli: Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Utaona, nikikujia na kuuchomoa upanga wangu alani mwake, niangamize waongofu na wapotovu, watoweke kwako.
4
Kwa kuwa nitaangamiza waongofu na wapotovu, watoweke kwako, kwa hiyo upanga wangu utachomolewa alani mwake, uwapige wote wenye miili toka kusini hata kasikazini.
5
Ndipo, wote wenye miili watakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana, ya kuwa nimeuchomoa upanga wangu alani mwake, usirudi humo tena.
6
Lakini wewe mwana wa mtu, piga kite! Kwa viuno vilivyovunjika na kwa uchungu ulio mkali piga kite, wakuone!
7
Tena wakikuuliza: Unapiga kite? uwaambie: Kwa hayo, niliyoyasikia, ya kuwa yatakuja, moyo wote umeyeyuka, nayo mikono ikalegea, nayo roho yote ikazimia, nayo magoti yakaja kugeuka kuwa kama maji. Mtaona, yakija kutimia; ndivyo, asemavyo Bwana Mungu.
8
Neno la Bwana likanijia la kwamba:
9
Mwana wa mtu, yafumbue yatakayokuwa ukisema: Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Sema: Uko upanga, ni upanga mwenyewe, umenolewa na kusuguliwa vema.
10
Umenolewa, kusudi uchinje machinjo, ukasuguliwa, kusudi ukatuke kama umeme. Au tuufurahie? Fimbo ya kumpigia mwanangu haishindwi na mti wo wote.
11
Aliutoa, usuguliwe vema, apate kuushika mkononi; nao ukanolewa ule upanga, ukasuguliwa vema, mwuaji apewe mkononi.
12
Piga yowe na kupaza sauti, mwana wa mtu! Kwani huo ndio unaowajia walio ukoo wangu, ndio unaowajia nao wakuu wa Isiraeli; wametupwa kwenye upanga pamoja nao walio ukoo wangu. Kwa hiyo jipige mapaja!
13
Kwani walijaribiwa, lakini imewafaliaje? Sasa je? Fimbo nayo ikatae kuwapiga? Haitakuwa; ndivyo, asemavyo Bwana Mungu.
14
Nawe mwana wa mtu, yafumbue yatakayokuwa ukiyapiga makofi! Kwani huo upanga utakuja mara mbili, hata mara tatu, ndio upanga upigao madonda kabisa, kweli ndio upanga mkubwa upigao madonda, ndio utakaowazunguka,
15
kusudi mioyo iyeyuke, tena wengi waanguke kwa kukwazwa; malangoni pao po pote nitatoa matisho ya huo upanga. A! Umefanywa, umerimete kama umeme! Umenolewa, upate kuchinja!
16
Jitege kupiga kuumeni! Jiweke tayari kupiga kushotoni! Piga po pote, makali yako yatakapoelekea!
17
Mimi nami nitayapiga makofi yangu nitakapoyatuliza makali yangu yenye moto; mimi Bwana nimeyasema.
18
Neno la Bwana likanijia la kwamba:
19
Wewe mwana wa mtu, jitengenezee njia mbili, upanga wa mfalme wa Babeli utakazozishika! Zote mbili zitatoka katika nchi moja; hapo njia pembeni pachore mkono, uelekezee mji, ndivyo uuchore!
20
Tengeneza njia, upanga utayoishika kwenda Rabati ya wana wa Amoni, tena nyingine kwenda Yuda katika Yerusalemu ulio na boma.
21
Kwani mfalme wa Babeli atasimama hapo penye njia panda, zile njia mbili zinapoanzia, apate kuagua uaguaji, akisukasuka mishale au akipiga bao au akitazama maini.
22
Kuumeni kwake kutaanguka kura ya Yerusalemu kwamba: aweke magogo ya kuvunjia boma, afumbue kinywa kupiga kelele, apaze sauti kupiga yowe, aweke magogo ya kuvunjia penye malango, azungushe ukingo wa mchanga, ajenge minara.
23
Nao uaguaji kama huo utakuwa uwongo machoni pao, ijapo wauapie viapo; lakini yeye atawakumbusha manza, walizozikora, kusudi watekwe.
24
Kwa hiyo Bwana Mungu anasema hivi: Kwa kuwa mnanikumbusha manza, mlizozikora, mapotovu yenu yakifunuliwa, makosa yenu yakitokea waziwazi kwa matendo yenu yote, kwa kuwa mnakumbukwa hivyo, basi, mtakamatwa kwa mikono.
25
Lakini wewe mkuu wa Isiraeli uliyejipatia uchafu kwa kuacha kunicha, siku yako imetimia, kwa kuwa ni wakati wa mwisho wa kukora manza.
26
Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Kiondoe kilemba cha kifalme! Ivue nayo taji! Haya ya sasa siyo yatakayokuwa tena. Yaliyoko chini ndiyo, watakayoyakweza, nayo yaliyoko juu ndiyo, watakayoyanyenyekeza.
27
Mabomoko na mabomoko na mabomoko ndiyo, nitakayoyaweka huku; lakini nayo siyo yatakayokuwa vivyo hivyo, mpaka aje, ambaye ni haki yake; yeye ndiye, nitakayempa.
28
Nawe mwana wa mtu, yafumbue yatakayokuwa ukisema: Haya ndiyo Bwana Mungu anayowaambia wana wa Amoni kwa ajili ya matusi yao, sema: Upanga ulio upanga kweli umechomolewa, nao umesuguliwa, upate kuchinja na kuua kabisa, kusudi uwe kama umeme.
29
Lakini wamekutazamia maono yasiyokuwa, wakakuagulia uwongo, wakuvute, uje kuwapiga shingo zao waliojipatia uchafu na kuacha kunicha, kwamba siku yao imetimia, kwa kuwa ni wakati wa mwisho wa kukora manza.
30
Lakini urudishe huo upanga alani mwake! Mahali, ulipoumbwa katika nchi, ulikozaliwa, nitakukatia shauri.
31
Nitakumwagia makali yangu, kwa moto wa machafuko yangu nitakufokea, kisha nitakutia mikononi mwa watu wasio wa kimtu, walio mafundi wa maangamizo.
32
Utakuwa chakula cha moto, damu yako itamwagwa katika nchi yako katikati, hutakumbukwa tena, kwani mimi Bwana nimeyasema.
← Chapter 20
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 22 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48