bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Ezekiel 32
Ezekiel 32
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 31
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 33 →
1
Ikawa katika mwaka wa 12 siku ya kwanza ya mwezi wa kumi na mbili, ndipo, neno la Bwana liliponijia la kwamba:
2
Mwana wa mtu, mtungie Farao, mfalme wa Misri, ombolezo la kwamba: Ulifananishwa na mwana wa simba alioko kwenye mataifa, nawe ulikuwa kama mamba aliomo kwenye maji mengi, mara kwa mara ulitokea kwa nguvu katika mito yako, ukachafua maji kwa miguu yako na kuivurugavuruga mito yao.
3
Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Nitautanda wavu wangu juu yako kwenye mkutano wa makabila mengi ya watu, nao watakupandisha pakavu kwa jarife langu.
4
Kisha nitakuacha hapo penye nchi kavu nikikutupa porini; kisha nitaleta ndege wa angani wote, wakukalie, nao nyama wote wa nchi hiyo nitawashibisha kwako.
5
Hata milimani juu nitazipeleka nyama za mwili wako, nayo mabonde nitayajaza uvundo wa kwako.
6
Nchi nitainywesha mafuriko yako yatokayo kwa damu yako, yafike hata milimani, nayo makorongo yatajazwa hayo yatokayo kwako.
7
Hapo, nitakapokuzima, nitaifunika mbingu, nazo nyota zake nitazitia giza, hata jua nitalifunika kwa wingu, hata mwezi hautaangaza mwanga wake.
8
Mianga yote iangazayo mbinguni nitaitia giza kwa ajili yako, hata nchi yako nitaieneza giza; ndivyo, asemavyo Bwana Mungu.
9
Kisha nitasikitisha mioyo ya watu wa makabila mengi, nitakapopeleka habari za kuvunjwa kwako kwa mataifa katika nchi, usizozijua wewe.
10
Hivyo nitastusha makabila mengi kwa ajili yako, nao wafalme wao watapigwa na bumbuazi kwa ajili yako, nitakapouchezesha upanga wangu mbele yao; ndivyo, watakavyoingiwa na woga mara kwa mara, Kila mtu kwa ajili ya roho yake, siku ile, utakapoangushwa.
11
Kwani hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Upanga wa mfalme wa Babeli utakujia.
12
Kwa panga za wapiga vita wenye nguvu nitawaua watu wako, ingawa wawe wengi, kwani wale wote ndio wakali kuliko mataifa mengine; watayapoteza majivuno ya Wamisri, watu wao walio wengi watakapoangamizwa.
13
Nao nyama wao wote nitawatowesha kwenye yale maji mengi, mguu wa mtu usiyachafue tena, wala nyama asiyachafue kwa kuyavurugavuruga.
14
Ndipo, nitakapoyachuja maji yao, nayo majito yao nitayaendesha kama mafuta yanavyokwenda; ndivyo, asemavyo Bwana.
15
Nitakapoigeuza nchi ya Misri kuwa pori tu, nchi itakapokuwa peke yake tu, yote yaliyoko yakitoweka, nitakapowapiga wote wakaao huko, ndipo, watakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana.
16
Hili ndilo ombolezo la kuimba kwa kuomboleza; wanawali wa mataifa waliimbe kwa kuiombolezea nchi ya Misri, nao watu wake wengi watawaombolezea hivyo; ndivyo, asemavyo Bwana Mungu.
17
Ikawa katika mwaka wa 12 siku ya kumi na tano ya mwezi, ndipo, neno la Bwana liliponijia la kwamba:
18
Mwana wa mtu, walilie hao watu wengi wa Misri, uwashushe pamoja na wanawali wa mataifa wenye utukufu kuwafikisha mahali palipo chini ya nchi kwao washukao shimoni.
19
Unampita nani kwa uzuri? Shuka tu, ulazwe kwao wasiotahiriwa!
20
Wataanguka katikati yao waliouawa kwa panga; panga za kuwaua zimekwisha tolewa; ivuteni hiyo nchi pamoja na watu wake wote walio wengi!
21
Ndipo, wapiga vita wenye nguvu walioko kuzimuni watakapomwambia yeye nao waliomsaidia: Wameshuka kulala hawa wasiotahiriwa waliouawa kwa panga.
22
Wako Waasuri na makundi yao yote ya watu, makaburi yao yanapazunguka pale po pote, wote wamekufa kwa kuumia wakiangushwa kwa panga.
23
Wamepata makaburi yao kuzimuni pembeni, nayo makundi yao ya watu yanayazunguka makaburi yao wenyewe; hao wote wamekufa kwa kuumia wakiangushwa kwa panga; nao ndio waliostusha watu wakubwa katika nchi yao walio hai.
24
Wako Waelamu nao watu wao wengi; wanalizunguka kaburi lake; hao wote wamekufa kwa kuumia wakiangushwa kwa panga, wameshuka pasipo kutahiriwa mahali palipo chini ya nchi; nao ndio waliostusha watu walipokuwa katika nchi yao walio hai, sasa wanashikwa na soni kwao walioshuka shimoni.
25
Katikati yao waliouawa kwa panga wamewapa pa kulala penye watu wao wengi, nayo makaburi yao hawa yanawazunguka wenyewe. Wote ni watu wasiotahiriwa waliouawa kwa panga, kwani walistusha watu walipokuwa katika nchi yao walio hai, lakini sasa wanashikwa na soni kwao walioshuka shimoni, katikati yao waliouawa kwa panga wamepata mahali pao.
26
Wako Wameseki na Watubali nao watu wao wengi, makaburi yao hawa yanawazunguka wenyewe; hawa wote ni watu wasiotahiriwa, walikufa wakiumia kwa panga; kwani walistusha watu walipokuwa katika nchi yao walio hai.
27
Hawatalala pamoja na wapiga vita walioanguka kwao wasiotahiriwa, walioshuka kuzimuni pamoja na vyombo vyao vya vita wakiziweka panga zao chini ya vichwa vyao, lakini maovu, waliyoyafanya, yanaifunika mifupa yao, kwani hao wapiga vita walistusha watu walipokuwa katika nchi yao walio hai.
28
Hivyo wewe nawe utavunjwa katikati yao wasiotahiriwa, ulale nao waliokufa wakiumia kwa panga.
29
Wako Waedomu, wafalme wao na wakuu wao, waliokuwa wenye nguvu za kupiga vita, lakini nao wamepewa mahali pao kwao waliokufa wakiumia kwa panga, walale nao kwao wasiotahiriwa walioshuka shimoni.
30
Wako wakuu wa kaskazini wote pamoja na Wasidoni wote walioshuka kwao waliokufa wakiumia kwa panga; walikuwa wakistusha watu kwa nguvu zao za kupiga vita, lakini soni za kushindwa zikawapata nao, sasa wanalala pasipo kutahiriwa kwao waliokufa wakiumia kwa panga wakishikwa na soni kwao walioshuka shimoni.
31
Farao atakapowaona hao atajituliza kwa ajili ya watu wake waliokuwa wengi. Farao na vikosi vyake vyote watakufa wakiumia kwa panga; ndivyo, asemavyo Bwana Mungu.
32
Kwani nalimpa kustusha watu, alipokuwa katika nchi yao walio hai, lakini naye atalazwa katikati yao wasiotahiriwa pamoja nao waliokufa wakiumia kwa panga, yeye Farao nao watu wake walio wengi. Ndivyo, asemavyo Bwana Mungu.
← Chapter 31
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 33 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48