bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Ezekiel 44
Ezekiel 44
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 43
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 45 →
1
Akanirudisha kwenda kwa jengo la lango la nje la Patakatifu lielekealo maawioni kwa jua, nalo lilikuwa limefungwa.
2
Bwana akaniambia: Lango hili sharti likae limefungwa, lisifunguliwe, wala asiingie mtu humo, kwa kuwa Bwana Mungu wa Isiraeli aliingia humo; kwa hiyo liwe limefungwa.
3
Naye atakayekuwa mkuu, yeye mkuu peke yake atakaa humu, ale chakula mbele ya Bwana, ataingia kwa njia ya ukumbi wa hilo jengo la lango, kisha atatoka kwa njia ileile.
4
Kisha akanipeleka kwenda kwa jengo la lango la kaskazini la hiyo Nyumba. Nilipotazama nikaona, utukufu wake Bwana, ulivyoijaza Nyumba, nikaanguka kifudifudi.
5
Bwana akaniambia: Mwana wa mtu, yaweke moyoni mwako utakayoyaona kwa macho yako nayo utakayoyasikia kwa masikio yako, yote nikayoyasema na wewe kwa ajili ya maongozi yote yaipasayo Nyumba ya Bwana na kwa ajili ya maonyo yake uyaweke moyoni mwako, ujue, mtakapoiingia Nyumba hii, napo pote, mtakapopatoka hapa Patakatifu.
6
Nao walio mlango wa Isiraeli ulio mkatavu waambie: Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Ninyi mlio mlango wa Isiraeli, yaacheni machukizo yenu yote, mliyoyafanya! Kwani ni mengi.
7
Mwalileta wageni wasiotahiriwa wala mioyo wala miili, wapaingie Patakatifu pangu, waipatie Nyumba yangu uchafu, mliponiletea chakula changu cha tambiko, cha mafuta na cha damu; hivyo ndivyo, mlivyolivunja Agano langu kwa kuyafanya hayo machukizo yenu yote.
8
Wenyewe hamkutumika na kuushika utumishi wa vitakatifu vyangu, mkawaweka wao kuwa mahali penu watumishi wa kutumikia Patakatifu pangu.
9
Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Mgeni yeyote asiyetahiriwa wala moyo wala mwili asipaingie tena Patakatifu pangu, ijapo awe mmoja wao wale wageni wote wakaao kwa wana wa Isiraeli katikati.
10
Ila Walawi walioniacha na kujiendea mbali hapo, Waisiraeli walipopotea, watatwikwa manza zao, walizozikora, ndio wale waliopotea kwa kuniacha wakiyafuata magogo yao ya kutambikia.
11
Hao watapatumikia Patakatifu pangu na kuyangoja malango ya Nyumba hii na kuwa watumishi wa humu Nyumbani; ndio watakaozichinja ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima nazo zile nyingine, watu watakazozitoa za tambiko; hapo ndipo, watakaposimama mbele yao, wawatumikie.
12
Kwa kuwa waliwatumikia watu mbele ya magogo yao ya kutambikia, wakawakosesha hivyo walio mlango wa Isiraeli, wakore manza, kwa sababu hii nimewaapia kwa kuuinua mkono wangu kwamba: Watatwikwa manza zao, walizozikora; ndivyo, asemavyo Bwana.
13
Lakini wasinikaribie na kufanya kazi za utambikaji, wala wasivikaribie vitakatifu vyangu vyenyewe; hivyo watashikwa na soni kwa kutwikwa machukizo yao, waliyoyafanya.
14
Kwa hiyo nitawaweka kuwa watumishi wa kutumikia humu Nyumbani, waufanye utumishi wake wote na kazi zote zitakazofanyizwa humu.
15
Lakini watambikaji wa Kilawi walio wana wa Sadoki, walioushika utumishi wa Patakatifu pangu, wana wa Isiraeli walipopotea na kuniacha, hao ndio watakaonikaribia, wanitumikie na kusimama mbele yangu, wakiniletea mafuta na damu; ndivyo, asemavyo Bwana Mungu.
16
Hao watapaingia Patakatifu pangu, waikaribie meza yangu wakinitumikia kwa kuushika utumishi wangu.
17
Nao watakapoingia malangoni mwa ua wa ndani sharti wavae mavazi ya pamba, wasiwe na nguo zo zote za manyoya ya kondoo wakifanya kazi za utambikaji mle malangoni mwa ua wa ndani namo humu Nyumbani!
18
Vichwani sharti wavae vilemba vya nguo za pamba, hata viunoni sharti wavae suruali za pamba, wasijifunge nguo zitoazo jasho.
19
Lakini watakapotoka kwenda katika ua wa nje, ni ule ua wa nje, watu walipo, sharti wayavue mavazi yao, waliyoyavaa wakifanya kazi za utumishi, wayaweke katika vile vyumba vya Patakatifu, kisha wavae mavazi mengine, wasiwapatie watu utakatifu kwa hayo mavazi yao.
20
Vichwa vyao wasivinyoe kabisa, wala wasiache mavunga, yakue kabisa, ila nywele zao za vichwani wazikatekate.
21
Tena wote walio watambikaji wasinywe mvinyo watakapouingia ua wa ndani.
22
Wala wasichukue mjane wala mwanamke aliyeachwa kuwa wake zao, ila waoe wanawali walio wa uzao wa mlango wa Isiraeli au mjane aliye mjane wa mtambikaji.
23
Wawafundishe watu wangu kupambanua kilicho kitakatifu nacho kinachotumika kwa watu siku zote, tena wawajulishe kupambanua yaliyo machafu nayo yaliyotakata.
24
Tena watu wakigombana, hao ndio wanaopaswa na kuwasimamia na kuwaamua, nao wawaamue kwa mashauri yangu. Sharti wayashike Maonyo yangu na maongozi yangu kwenye mikutano yote ya sikukuu zangu, nazo siku zangu za mapumziko sharti wazitakase!
25
Mtu aliyekufa wasimkaribie, wasijipatie uchafu! Wajipatie uchafu tu kwa baba na mama na mwana wa kiume na wa kike na kwa ndugu na kwa umbu asiyeolewa bado.
26
Atakapokwisha kueuliwa, wamhesabie tena siku saba!
27
Kisha siku, atakapopaingia Patakatifu, auingie ua wa ndani kufanya kazi ya utumishi hapo Patakatifu, kwanza apeleke ng'ombe ya tambiko ya weuo; ndivyo, asemavyo Bwana Mungu.
28
Tena fungu litakalowapasa kuwa lao, basi, mimi nitakuwa fungu lao, kwa hiyo msiwape mali zo zote kwao Waisiraeli za kuzishika kuwa zao! Mimi ni mali zao za kuzishika kuwa zao.
29
Vipaji vya tambiko nazo ng'ombe za tambiko za weuo na za upozi wao watazila, navyo vyo vyote vitakavyokuwa mwiko kwao Waisiraeli kuvila vitakuwa mali zao.
30
Nayo malimbuko yote pia yanayotolewa kwa kuwa ya kwanza, navyo vipaji vyenu vyote vingine, mtakavyovitoa, vitakuwa mali zao watambikaji nao unga wenu wa kwanza wa kupika mikate mtawapa watambikaji, mbaraka izikalie nyumba zenu.
31
Lakini kila nyama aliyekufa kibudu au aliyeraruliwa na nyama mwingine, watambikaji wasile, kama ni ya ndege au ya nyama.
← Chapter 43
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 45 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48