bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Ezekiel 22
Ezekiel 22
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 21
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 23 →
1
Neno la Bwana likanijia la kwamba:
2
Wewe mwana wa mtu, hutauhukumu, kweli hutauhukumu mji huo ujaao damu za watu? Uujulishe machukizo yake yote!
3
Sema: Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Wewe ndiwe mji uliomwaga mwake damu za watu, siku zake zitimie, ukafanya magogo ya kutambikia, ukajipatia uchafu nayo.
4
Kwa hizo damu zako, ulizozimwaga, umekora manza, tena kwa hayo magogo ya kutambikia, uliyoyafanya, umejipatia uchafu, hivyo umezifikisha siku zako karibu, ukaja penye mwisho wa miaka yako. Kwa hiyo nitakutia soni kwa wamizimu, usimangwe katika nchi zote.
5
Nchi zilizoko karibu yako nazo zilizoko mbali yako zitakusimanga kwamba: Umelipatia jina lako uchafu, ukafanya matata mengi.
6
Tazama, wakuu wa Isiraeli wote walikuwa mwako wakiitumia mikono yako kumwaga damu za watu.
7
Mwako watu hawachi wala baba wala mama, nao wageni huwafanyia ukorofi mwako, wafiwao na wazazi nao wajane watu huwatesa mwako.
8
Patakatifu pangu wewe hupabeza, nazo siku zangu za mapumziko wewe huzichafua.
9
Mwako mna watu wanaowaonea wenzao, wapate kumwaga damu zao, tena mwako wamo wanaokula vilimani vyakula vya tambiko, hata uzinzi watu hufanya mwako.
10
Yenye soni ya baba watu huyafunua mwako, mwako huwatumia kwa nguvu nao wanawake wenye uchafu kwa kuwa na siku zao.
11
Wako wanowafanyizia wake wa wenzao yachukizayo, tena wako wanojichafua kwa kuwatumia wakwe wao wa kike kufanya uzinzi nao, tena wako wanaowatumia kwa nguvu nao maumbu zao waliozaliwa na baba yao.
12
Mwako wamo wanotaka kupenyezewa fedha, kusudi wamwage damu, tena huchukua faida na nyongeza za kupunja, mkiwadanganya wenzenu kwa ukorofi, lakini mimi mmenisahau; ndivyo, asemavyo Bwana Mungu.
13
Lakini utaniona, nikiyapiga makofi yangu kwa ajili ya mali zako, ulizojipatia kwa udanganyifu, na kwa ajili ya damu zako zilizomwagwa mwako mjini katikati.
14
Je? Moyo wako utasimama? Je? Mikono yako itakuwa na nguvu zao siku zile, nitakapokufanyizia mambo? Mimi Bwana nimeyasema, nami nitayafanya.
15
Nitakutawanya kwa wamizimu na kukutupatupa katika nchi zao; hivyo nitaukomesha uchafu wako kabisa, uishe kwako!
16
Nawe utakuwa mwenye upujufu machoni pao wamizimu; ndipo, utakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana.
17
Neno la Bwana likanijia la kwamba:
18
Mwana wa mtu, walio mlango wa Isiraeli wameniwia kama mavi ya chuma, wao wote ni kama shaba nyekundu na shaba nyeupe na chuma na risasi katika tanuru, wamegeuka kuwa mitapo ya fedha.
19
Kweli hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Kwa kuwa ninyi nyote mmegeuka kuwa mitapo ya fedha, mtaniona, nikiwakusanya ninyi mjini mwa Yerusalemu;
20
kama fedha na shaba nyekundu na chuma na shaba nyeupe zinavyokusanywa ndani ya tanuru, ziwashiwe moto, zipate kuyeyuka, hivyo ndivyo, nitakavyowakusanya kwa makali yangu na kwa machafuko yangu yenye moto, niwatie mle ndani kuwayeyusha.
21
Kweli nitawakusanya, niwawashie moto wa machafuko yangu; ndivyo, nitakavyowayeyusha mle ndani.
22
Kama wanavyoyeyusha fedha ndani ya tanuru, ndivyo mtakavyoyeyushwa ndani yake. Ndipo, mtakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana, nimewamwagia makali yangu yenye moto.
23
Neno la Bwana likanijia la kwamba:
24
Mwana wa mtu, iambie nchi hii: Wewe ndiwe nchi isiyotakasika, isiyonyweshwa mvua siku ya kukasirikiwa.
25
Wafumbuaji wake waliomo mwake wamekula njama, wakawa kama simba angurumaye akinyafua nyama, aliowakamata; nao wakazila roho za watu, wakazitwaa nazo mali zao na vitu vyao vyenye kiasi, wakawaua waume wao wanawake wengi waliokuwamo, wakawageuza kuwa wajane.
26
Watambikaji wao wakayapotoa Maonyo yangu, wakapachafua Patakatifu pangu hawakuyapambanua matakatifu nayo yatumiwayo tu, wala hawakuyajulisha watu kuyapambanua yaliyo machafu nayo yaliyotakata, tena wameyafumba macho yao penye siku zangu za mapumziko nikapatiwa uchafu katikati yao.
27
Wakuu wao waliokuwa mle mjini wakawa kama chui wanaonyafua nyama waliowakamata, hutaka kumwaga damu za watu na kuziangamiza roho zao, kusudi wajipatie mali za madanganyo yao.
28
Nao wafumbuaji wake huyapaka mambo yao yote chokaa, wakiona maono ya uwongo na kusema: Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema, naye Bwana hakusema neno.
29
Watu wa nchi hii hukorofisha kabisa na kupokonya sana, hutesa wanyonge na wakiwa, hukorofisha nao wageni kwa njia zisizonyoka.
30
Nikatafuta mtu wa kwao afaaye kuujenga ukuta na kusimama mbele yangu palipoatuka ufa, aikingie nchi hii, nisiiangamize, lakini sikumwona.
31
Nikawamwagia makali yangu nikawamaliza kwa moto wa machafuko yangu, nikawatwika njia zao vichwani pao; ndivyo asemavyo Bwana Mungu.
← Chapter 21
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 23 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48