bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Ezekiel 18
Ezekiel 18
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 17
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 19 →
1
Neno la Bwana likanijia la kwamba:
2
Ninyi hulitumiaje katika nchi ya Isiraeli fumbo kama hilo la kwamba: Baba walipokula zabibu bichi, ndipo, wana alipokufa ganzi la meno.
3
Ndivyo, asemavyo Bwana Mungu: Hivyo, nilivyo Mwenye uzima, hatakuwako tena kwenu atakayelitumia fumbo hili kwao Waisiraeli.
4
Tazameni: Roho zote za watu ni zangu, kama ni roho za baba, au kama ni roho za wana, zote ni zangu; roho ya mtu atakayekosa ndiyo itakayokufa.
5
Mtu akiwa mwongofu, afanye yaliyo sawa yaongokayo,
6
asile vilimani juu, wala asiyatazamie kwa macho yake magogo ya kutambikia ya mlango wa Isiraeli, wala asimchafue mke wa mwenziwe, wala asimkaribie mwanamke mwenye siku zake,
7
wala asimtese mtu, ila aliyemkopa amrudishie aliyompa yeye ya kumwekea, asinyang'anye isiyo mali yake, wenye njaa awagawie vyakula vyake, wenye uchi awavike nguo,
8
asikopeshee kupata faida, wala asichukue nyongeza za kupunja, mkono wake auzuie, usipotoe, aamue kwa kweli, mtu akigombana na mwenziwe,
9
ayafuate maongozi yangu na kuyashika mashauri yangu na kufanya yaliyo kweli, basi, mtu aliye hivyo ni mwongofu, naye atapata uzima wa kweli; ndivyo, asemavyo Bwana Mungu.
10
Mtu kama huyo akizaa mwana aliye mkorofi, amwage damu, afanye moja tu la mabaya yale,
11
yeye baba yake asiyoyafanya yote, kama anakula vilimani juu, au kama anamchafua mke wa mwenziwe,
12
au kama anawatesa wanyonge na wakiwa, au kama ananyang'anya mali yake, au kama harudishi aliyopewa ya kumwekea mtu, au kama anayatazamia kwa macho yake magogo ya kutambikia, ayafanye yachukizayo,
13
au kama anakopeshea kupata faida, au kama anachukua nyongeza za kupunja, basi, yeye atapata kabisa uzima wa kweli, ila atakufa kweli kwa kuyafanya hayo machukizo yote akitwikwa manza zake za damu, alizozikora.
14
Huyu akizaa mwana, naye akiyaona makosa yote, baba yake aliyoyatenda, lakini akiyaona tu, asiyafanye yaliyo kama hayo,
15
asile vilimani juu, wala asiyatazamie kwa macho yake magogo ya kutambikia ya mlango wa Isiraeli, wala asimchafue mke wa mwenziwe,
16
wala asimtese mtu, wala asimtoze mtu mali za kumwekea, wala asinyang'anye isiyo mali yake, ila wenye njaa awagawie vyakula vyake, wenye uchi awavike nguo,
17
auzuie mkono wake, usipotoe mnyonge, wala usichukue faida wala nyongeza za kupunja, ayafanye mashauri yangu na kuyafuata maongozi yangu, basi aliye hivyo hata kufa kwa ajili ya manza, baba yake alizozikora, ila atapata uzima wa kweli.
18
Lakini baba yake aliyekorofisha kwa ukorofi wake, aliyemnyang'anya ndugu mali isiyo yake, aliyefanya katikati ya wenziwe wa ukoo yasiyo mema, mtamwona, yeye akifa kwa ajili ya hizo manza, alizozikora.
19
Mkiuliza: Sababu gani mwana hatwikwi naye manza za baba yake? ni hivyo: mwana alifanya yaliyo sawa yaongokayo, akayashika maongozi yangu yote na kuyafanya, kwa hiyo atapata uzima wa kweli.
20
Roho ya mtu atakayekosa ndiyo itakayokufa, lakini mwana hatatikwa manza za baba yake, wala baba hatatwikwa manza za mwanawe, nao wongofu wake mwongofu utamkalia, nao ubezi wake asiyemcha Mungu utamkalia.
21
Lakini asiyemcha Mungu akirudi na kuyaacha makosa yake yote, aliyoyafanya, ayashike maongozi yangu yote na kufanya yaliyo sawa yaongokayo, basi, atapata uzima wa kweli, hatakufa.
22
Nayo mapotovu yake yote, aliyoyafanya, hayatakumbukwa, ila atapata uzima kwa wongofu wake, alioufanya.
23
Ndivyo, asemavyo Bwana Mungu: Mnaniwaziaje kwamba: Nitapendezwa, asiyenicha akifa? Je? Sitapendezwa, akirudi na kuziacha njia zake, apate uzima?
24
Lakini mwongofu akigeuka na kuuacha wongofu wake, afanye mapotovu, ayafanye hayo machukizo yote, wasiomcha Mungu wanayoyafanya, je? Atapata uzima? Sivyo, wongofu wote, alioufanya, hautakumbukwa, kwa kuwa amevunja maagano, naye kwa ajili ya makosa yake, aliyoyakosa, atakufa.
25
Mkisema: Kumbe njia ya Bwana hainyoki! Sikieni, ninyi wa mlango wa Isiraeli: Je? Njia yangu hainyoki? Sizo njia zenu zisizonyoka?
26
Mwongofu akirudi na kuuacha wongofu wake, afanya maovu, atakufa kwa ajili yao, kweli, kwa ajili ya hayo maovu, aliyoyafanya, atakufa.
27
Tena asiyemcha Mungu akirudi na kumcha Mungu afanye yaliyo sawa yaongokayo, huyu ataipatia roho yake uzima.
28
Akipata kuona, akirudi na kuyaacha mapotovu yake yote, aliyoyafanya, atapata uzima wa kweli, hatakfufa.
29
Wao wa mlango wa Isiraeli wakisema: Njia ya Bwana hainyoki, inakuwaje, njia zangu zisiponyoka? Ninyi wa mlango wa Isiraeli, sizo njia zenu zisizonyoka?
30
Kwa hiyo nitawapatiliza ninyi wa mlango wa Isiraeli kila mtu, kama njia zakezilivyo; ndivyo, asemavyo Bwana Mungu. Rudini na kujigeuza na kuyaacha mapotovu yenu yote, yasiwawie tena makwazo ya kuwakosesha!
31
Yatupeni mapotovu yenu yote mliyoyafanya ya kuwapotoa wenzenu, yawatoke ninyi! Kisha jipatieni mioyo mipya! na roho mpya! Mbona mnataka kufa, ninyi wa mlango wa Isiraeli?
32
Kweli sipendezwi na kufa kwake mwenye kufa; ndivyo asemavyo Bwana Mungu. Kwa hiyo jigeuzeni, mpate uzima!
← Chapter 17
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 19 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48