bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Ezekiel 28
Ezekiel 28
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 27
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 29 →
1
Neno la Bwana likanijia la kwamba:
2
Mwana wa mtu, mwambie mfalme wa Tiro: Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Moyo wako umejikuza kwamba: Mungu ni mimi, tena ninakaa pake Mungu baharini katikati! Kumbe nawe u mtu, hu Mungu, nawe moyo wako ukajiwazia kuwa kama moyo wa Mungu!
3
Je? Wewe u mwerevu wa kweli kuliko Danieli, lisifichike jambo lo lote, usipolipambazua?
4
Kwa werevu wako wa kweli na kwa utambuzi wako ulijipatia mali, ukalimbika dhahabu na fedha katika maweko yako.
5
Kwa kuwa mwenye werevu mwingi ulio wa kweli ukaziongeza sana mali zako kwa biashara zako, ulizozifanya; kwa hizo mali zako moyo wako ukajikuza.
6
Kwa hiyo Bwana Mungu anasema hivi: Kwa kuwa moyo wako unajiwazia kuwa kama moyo wa Mungu,
7
kwa sababu hiyo utaniona, nikikupelekea wageni, ndio mataifa yenye ukali kupita wengine. Nao watazichomoa panga zao kupigana na uzuri wa werevu wako wa kweli, wauchafue uangafu wako.
8
Watakusukuma, ushuke shimoni, nawe utakufa baharini katikati, kama waliopigwa na panga wanavyokufa.
9
Je? Usoni pa mwuaji utasema tena: Mungu ni mimi? Nawe u mtu, hu Mungu, tena utakuwa mkononi mwake akupigaye kwa upanga.
10
Utakufa mikononi mwa wageni, kama wanavyokufa wasiotahiriwa, kwani mimi nimeyasema; ndivyo, asemavyo Bwana Mungu.
11
Neno la Bwana likanijia la kwamba:
12
Mwana wa mtu, mtungie mfalme wa Tiro ombolezo! Mwambie: Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Wewe ulikuwa kielelezo cha ulinganifu, tena mwenye werevu wa kweli mwingi na mwenye kuutimiza uzuri.
13
Ukawa Edeni katika bustani ya Mungu, ukalipamba vazi lako kwa vito vya kila namna: sardio na topazio na yaspi na krisolito na oniki na berilo na safiro na ametisto na sumarato na dhahabu; siku hiyo ulipoumbwa, kazi za patu zako na filimbi zako zilikuwa zimetengenezwa, zikuwie tayari.
14
Ukawa kama Kerubi aliyepakwa mafuta kuwa mlinzi, nikakuweka juu ya mlima mtakatifu wa Mungu, ukawako ukitembea katika mawe yenye moto katikati.
15
Ukawa pasipo kosa lo lote katika njia zako tangu siku ile, ulipoumbwa, mpaka upotovu ulipooneka kwako.
16
Lakini kwa uchuuzi wako mwingi ukajaa makorofi ndani yako, ukakosa, nami nikakukimbiza kwenye mlima wa Mungu, kwa kuwa ulijipatia uchafu, nikakutowesha uliyekuwa kama Kerubi alindaye, uondoke katika yale mawe yenye moto.
17
Moyo wako ulijikuza kwa ajili ya uzuri wako, ukauharibu werevu wako wa kweli kwa ajili ya uangafu wako; ndipo, nilipokubwaga chini, nikakutoa machoni pao wafalme, wakutumbulie macho.
18
Kwa manza zako nyingi ulizozikora, tena kwa kupotoa uchuuzi wako, ulipatia Patakatifu pako uchafu; kwa hiyo nikatoa moto mwako katikati, ukakuteketeza, nikakutoa kuwa mavumbi ya nchi machoni pao wote waliokutazama.
19
Wote waliokujua katika makabila ya watu hukustukia, kwa kuwa umegunduliwa na maangamizo, nawe hutakuwapo tena kale na kale.
20
Neno la Bwana likanijia la kwamba:
21
Mwana wa mtu, uuelekezee Sidoni uso wako na kuufumbulia yatakayokuwa!
22
Sema: Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Utaniona, nikikujia, Sidoni, nijitokeze katikati yako kuwa mtukufu. Ndipo, watakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana, nitakapouhukumu, nijulike mwake, ya kuwa ni mtakatifu.
23
Nitatuma kwake magonjwa mabaya na damu barabarani mwake, waangushwe mwake chini po pote waliopigwa kwa panga; ndipo, watakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana.
24
Mlango wa Isiraeli hautaona tena miiba ya kuwachoma wala machomo ya kuwaumiza kwao wote wanaokaa na kuwazunguka waliowabeza; ndipo, watakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana Mungu.
25
Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Nitakapowakusanya walio ukoo wa Isiraeli na kuwatoa kwenye makabila yote, walikotawanyikia, ndipo, nitakapoutokeza kwao utakatifu wangu, wao wa mataifa wauone; nao watakaa katika nchi yao, niliyompa mtumishi wangu Yakobo.
26
Nao watakaa huko kwa kutulia, wajenge nyumba, wapande mizabibu; watakaa kwa kutulia, kwa kuwa nitawakatia mashauri kwao wote wanaokaa na kuwazunguka waliowabeza. Ndipo, watakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana Mungu wao.
← Chapter 27
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 29 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48