bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Ezekiel 20
Ezekiel 20
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 19
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 21 →
1
Ikawa katika mwaka wa 7 mwezi wa tano siku ya kumi, ndipo waume wazee wa Kiisiraeli walipokuja kumwuliza Bwana, wakakaa mbele yangu.
2
Neno la Bwana likanijia la kwamba:
3
Mwana wa mtu, sema na wazee wa Kiisiraeli, uwaambie: Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Inakuwaje, mkija kuniuliza? Hivyo, nilivyo Mwenye uzima, siulizwi nanyi! ndivyo, asemavyo Bwana Mungu.
4
Haitafaa, ukiwahukumu wewe? Je? Haitafaa ukiwahukumu wewe, mwana wa mtu? Wajulishe machukizo ya baba zao!
5
Waambie: Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Siku ile, nilipowachagua Waisiraeli, niliuinua mkono wangu na kuwaapia walio uzao wa mlango wa Yakobo, nikajijulisha kwao katika nchi ya Misri, nikauinua mkono wangu na kuwaapia kwamba: Mimi ni Bwana Mungu wenu.
6
Siku ile niliuinua mkono wangu na kuwaapia, ya kuwa nitawatoa katika nchi ya Misri na kuwapeleka katika nchi, niliyowachagulia kuwa nchi ichuruzikayo maziwa na asali, tena kuwa nchi iliyo urembo wa nchi zote.
7
Ndipo, nilipowaambia: Yatupeni kila mtu hayo yatapishayo kwa kutazamwa tu! Msijipatie uchafu kwa kuyatambikia magogo yao Wamisri ya kutambikia! Mimi Bwana ni Mungu wenu.
8
Kisha wakanikataa wasipotaka kunisikia, hawakuyatupa kila mtu matapisho yake aliyoyatazama, wala hawakuyaacha magogo yao Wamisri ya kutambikia, nikasema: Nitawamwagia makali yangu yenye moto, machafuko yangu yamalizike kwao kulekule katika nchi ya Misri.
9
Lakini nikafanya mengine kwa ajili ya Jina langu, lisitiwe uchafu machoni pao wamizimu, kwani wanakaa wakizungukwa nao, nami nilijijulisha machoni pao kwamba: Nitawatoa katika nchi ya Misri.
10
Basi, nikawatoa katika nchi ya Misri, nikawapeleka nyikani.
11
Nikawapa maongozi yangu, nikawajulisha nayo mashauri yangu, nayo ndiyo yatakayompa mtu uzima, akiyafanya.
12
Nikawapa nazo siku zangu za mapumziko, ziwe kielekezo cha maagano, tuliyoyaagana mimi nao, wajue, ya kuwa mimi ni Bwana awatakasaye.
13
Lakini walio mlango wa Isiraeli wakanikataa nako nyikani: maongozi yangu hawakuyafuata, mashauri yangu wakayabeza, nayo ndiyo yatakayompa mtu uzima, akiyafanya. Nazo siku zangu za mapumziko wakazipitia uchafu sana, nikasema: Nitawamwagia makali yangu yenye moto huku nyikani, yawamalize.
14
Lakini nikafanya mengine kwa ajili ya Jina langu, lisitiwe uchafu machoni pao wamizimu walioona kwa macho yao, jinsi nilivyowatoa.
15
Nami nikauinua mkono wangu na kuwaapia huko nyikani kwamba: Sitawapeleka katika nchi ile, niliyowapa, ichuruzikayo maziwa na asali, iliyo urembo wa anchi zote,
16
kwa kuwa waliyabeza mashauri yangu, hawakuyafuata maongozi yangu, wakazipatia siku zangu za mapumziko uchafu, kwani mioyo yao ikayaendea magogo yao ya kutambikia.
17
Lakini macho yangu yakawaonea uchungu, nisiwaangamize; basi, nikaacha kuwamaliza nyikani.
18
Nikawaambia wana wao huko nyikani: Maongozi ya baba zenu msiyafuate, wala msiyashike mashauri yao, wala msijichafue kwa kuyatambikia magogo yao!
19
Mimi Bwana ni Mungu wenu, yafuateni maongozi yangu! Yashikeni nayo mashauri yangu, myafanaye!
20
Zitakaseni siku zangu za mapumziko, ziwe kielekezo cha maagano, tuliyoyafanya mimi nanyi, mjue, ya kuwa mimi ni Mungu wenu!
21
Lakini hao wana nao wakanikataa: maongozi yangu hawakuyafuata, mashauri yangu hawakuyashika, wayafanye, nayo ndiyo yatakayompa mtu uzima, akiyafanya; siku zangu za mapumziko wakazipatia uchafu, nikasema: Nitawamwagia makali yangu yenye moto, machafuko yangu yamalizike kwao nyikani.
22
Kisha nikaurudisha mkono wangu, nikafanya mengine kwa ajili ya Jina langu, lisitiwe uchafu machoni pao wamizimu walioona kwa macho yao, jinsi nilivyowatoa.
23
Nami nikauinua mkono wangu na kuwaapia huko nyikani kwamba: Nitawatawanya kwenye wamizimu na kuwatupatupa katika nchi zao,
24
kwa kuwa hawakuyafanya mashauri yangu, wakayabeza maongozi yangu, wakazipatia siku zangu za mapumziko uchafu, wakayatazamia kwa macho yao magogo, baba zao waliyoyatambikia.
25
Ndipo, mimi nami nilipowatolea maongozi yasiyokuwa mema, hata amashauri yasiyoweza kuwapa uzima.
26
Nikawapatia uchafu kwa vipaji vyao vya tambiko, wakawapitisha motoni wote waliofungua tumbo la mama, kusudi niwastushe, wajue, ya kuwa mimi ni Bwana.
27
Kwa hiyo sema na mlango wa Isiraeli, wewe mwana wa mtu, uwaambie: Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Hata kwa neno hili baba zenu walinitukana, wakilivunja agano.
28
Nilipokuwa nimekwisha kuwapeleka katika nchi, niliyowaapia kwa kuuinua mkono wangu kwamba: Nitawapa basi, po pote walipoona kilima kirefu, napo walipoona mti wenye majani mengi, ndipo, walipochinja ng'ombe zao za tambiko, wakatoa hapohapo vipaji vyao vya tambiko, kusudi wanikasirishe, wakavukiza hapo uvumba wao wenye mnuko wa kupendeza, wakamwagia hapo vinywaji vyao vya tambiko.
29
Nikawauliza: Kiko kilima gani, mnachokijia hapo? Kwa hiyo jina lake likaitwa Kilima hata siku ya leo.
30
Kwa hiyo uambie mlango wa Isiraeli: Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Je? Mnajipatia uchafu kwa kuzishika njia za baba zenu? Je? Nanyi mnafanya ugoni kwa kuyafuata matapisho yao?
31
Hata kwa kutoa vipaji vyenu vya tambiko, mkiwapitisha wana wenu motoni, mnajipatia uchafu na kuyatumikia magogo yenu yote ya kutambikia mpaka siku ya leo, sasa je? Mimi niulizwe nanyi mlio mlango wa Isiraeli? Ndivyo, asemavyo Bwana Mungu: Hivyo nilivyo Mwenye uzima, sitaulizwa nanyi kabisa!
32
Nayo yanayowazwa rohoni mwenu hayatakuwa kabisa, ninyi mkisema: Nasi na tuwe, kama wamizimu nao wa koo za nchi hizi walivyo, tukitumikia miti na mawe.
33
Ndivyo, asemavyo Bwana Mungu: Hivyo, nilivyo Mwenye uzima, mimi nitakuwa mfalme wenu kwa kiganja chenye nguvu na kwa mkono ukunjukao na kwa makali yenye moto yamwagwayo.
34
Nami nitawatoa kwenye makabila mengine nikiwakusanya na kuwatoa katika nchi hizi, mlikotupwa kwa kiganja chenye nguvu na kwa mkono ukunjukao na kwa makali yenye moto yamwagwayo.
35
Nitawapeleka katika nyika ya makabila mengine; ndiko, nitakakowakatia mashauri uso kwa uso.
36
Kama nilivyowakatia baba zenu shauri katika nyika ya Misri, ndivyo, nitakavyofanya shauri nanyi; ndivyo, asemavyo Bwana Mungu.
37
Nitawapitisha chini ya fimbo ya uchungaji, nije kuwashurutisha kulishika agano.
38
Nitatenga kwenu wakatavu nao walionikosea, nikiwatoa katika nchi wakaako ugeni, wasiingie nchi ya Waisiraeli; ndipo, mtakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana.
39
Tena kwa ajili yenu mlio mlango wa Isiraeli Bwana Mungu anasema hivi: Haya! Nendeni kila mtu kuyatumikia magogo yenu ya kutambikia! Lakini siku za nyuma mtanisikiliza kabisa, msilitie jina la Patakatifu pangu tena uchafu kwa vipaji vyenu vya tambiko na kwa magogo yenu ya kutambikia.
40
Kwani ndivyo, asemavyo Bwana: Katika mlima wangu mtakatifu utakaokuwa mlima mrefu wa Isiraeli ndiko, watakakonitumikia wao wa milango yote ya Isiraeli nazo nchi zake zote; tena ndiko, nitakakowapendeza nikitaka kuvipokea vipaji vyenu, mtakavyonitolea, nayo malimbuko yenu ya kunitambikia katika yote, mtakayonitakasia.
41
Hapo nitawapendeza na kuutaka mnuko mzuri, nitakapowatoa kwenye makabila mengine na kuwakusanya, mzitoke hizo nchi, mlikotawanywa; ndipo, nitakapotakaswa kwenu machoni pao wamizimu.
42
Ndipo, mtakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana, nikiwapeleka katika nchi ya Isiraeli, katika ile nchi niliyowaapia na kuuinua mkono wangu kwamba: Nitawapa baba zenu.
43
Nanyi huko mtazikumbuka njia zenu na matendo yenu, mliyojipatia uchafu nayo, nanyi mtajichukia wenyewe kwa ajili ya mabaya yenu yote, mliyoyafanya.
44
Ndipo, mtakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana, nitakapowafanyizia hivyo kwa ajili ya Jina langu, lakini sivyo kwa ajili ya njia zenu mbaya, wala kwa ajili ya matendo yenu maovu, ninyi wa mlango wa Isiraeli; ndivyo, asemavyo Bwana Mungu.
45
Neno la Bwana likanijia la kwamba:
46
Mwana wa mtu, uelekeze uso wako kutazama upande wa kusini, uitangazie nchi yenye jua kali, ukiufumbulia mwitu ulioko kwenye mbuga za kusini yatakayokuwa.
47
Uuambie huo mwitu ulioko kusini: Lisikie neno la Bwana! Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Utaona, nikiwasha moto kwako utakaokula kwako miti mibichi yote na miti mikavu yote; miali ya moto huo uwakao haitazimika, mpaka nyuso zote toka kusini hata kaskazini ziunguzwe nao.
48
Ndipo, wote wenye miili watakapoona ya kuwa mimi ni Bwana, ya kuwa mimi nimewasha moto usiozimika.
49
Nikasema: E Bwana Mungu, hao hunisema kwamba: Yeye siye atumiaye mafumbo?
← Chapter 19
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 21 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48