bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Ezekiel 38
Ezekiel 38
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 37
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 39 →
1
Neno la Bwana likanijia la kwamba:
2
Mwana wa mtu, uelekeze uso wako kumtazama Gogi katika nchi ya Magogi aliye mkuu wa Rosi na wa Meseki na wa Tubali, umfumbulie yatakayomjia,
3
ukisema: Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Utaniona, nikikujia wewe Gogi uliye mkuu wa Rosi na wa Meseki na wa Tubali.
4
Nitakugeuza nikikutia hatamu katika taya zako, nikutoe katika nchi yako pamoja na vikosi vyako vyote, farasi nao wawapandao, wao wote watakuwa wamevaa nguo za urembo, nao watakuwa mkutano mkubwa wenye ngao kubwa na ndogo, nao wote watashika panga.
5
Kwako unao Wapersia na Wanubi na Waputi, wao wote ni wenye ngao na kofia za vita.
6
Wagomeri na vikosi vyao nao wa mlango wa Togarma wakaao kaskazini mbali sana na vikosi vyao, kweli ni makabila mengi, uliyo nayo.
7
Jipangeni na kujiweka tayari, wewe na mikutano yako yote iliyokusanyika kwako, nawe uwe mlinzi wao!
8
Siku zitakapopita nyingi, utakaguliwa; miaka iliyowekwa itakapokwisha, utakwenda katika nchi iliyopata nguvu tena kwa kupona madonda ya panga, ufike kwao waliokusanywa na kutolewa kwa makabila mengi, wakae tena katika milima ya Isiraeli, iliyokuwa siku zote mapori matupu. Wao ndio waliotolewa kwenye makabila mengine, wakae salama wote pamoja.
9
Ndiko, utakakopanda, uwajie kama upepo wa chamchela, utaifunika hiyo nchi kama wingu, wewe na vikosi vyako vyote vya yale makabila mengi, uliyo nayo.
10
Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Siku ile yatakuingia moyoni mambo yatakayokuwazisha mawazo mabaya.
11
Ndipo, utakaposema: Nitapanda kwenda katika nchi iliyo wazi, nitaingia kwenye watu wanaotulia, wanaokaa salama; wote wanakaa pasipo boma, hawajui makomeo wala milango.
12
Huko utataka kuteka mateka na kunyang'anya mali za watu, uinulie mkono wako mahame yanayokaa watu tena, uteke watu waliokusanywa na kutolewa kwenye mataifa, waliojipatia tena ng'ombe na mali nyingine, wanaokaa katikati ya dunia.
13
Wasaba na Wadedani na wachuuzi wa Tarsisi na masimba yao wenye nguvu watakuuliza: Je? Umekuja kuteka mateka na kunyang'anya mali za watu? Umeikusanya mikutano yako kuchukua fedha na dhahabu, kujipatia ng'ombe na mali nyingine za watu, kuteka mateka mengi?
14
Kwa hiyo, mwana wa mtu, mfumbulie Gogi yatakayompata ukimwambia: Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Siku hiyo, walio ukoo wangu wa Isiraeli watakapokaa salama, hutaijua?
15
Ndipo, utakapoondoka mahali pako huko mbali kaskazini wewe na makabila mengi pamoja na wewe, wote ndio wapanda farasi, ni mkutano mkubwa na vikosi vingi.
16
Utapanda kuwajia walio ukoo wangu wa Isiraeli, utaifunika nchi hiyo kama wingu. Siku zilizowekwa zitakapokwisha, nitakupeleka katika nchi yangu, kusudi wamizimu wapate kunijua mimi, nitakapojitokeza kuwa mtakatifu, nikikupatiliza, wewe Gogi, machoni pao.
17
Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Kumbe si wewe, niliyemsema siku za kale kwa vinywa vya watumishi wangu, wale wafumbuaji wa Isiraeli, waliofumbua siku zile miaka kwa miaka, ya kuwa nitakupeleka wewe, uwajie?
18
Ndivyo, asemavyo Bwana Mungu: Siku ile, Gogi atakapoiingia nchi ya Isiraeli, ndipo, makali yangu yenye moto yatakaponipanda kuingia puani mwangu.
19
Kwa wivu wangu na kwa moto wa machafuko yangu nasema: Siku hiyo itakuwa na tetemeko kubwa katika nchi ya Isiraeli.
20
Kwa kuniona watatetemeka samaki wa baharini na ndege wa angani na nyama wa porini na vidudu vyote vitambaavyo katika nchi nao watu wote wanaokaa katika nchi; ndipo, milima itakapoporomoka, nayo magenge yataanguka, nayo maboma yote yataanguka chini.
21
Kisha nitaziita panga katika milima yangu yote, zije kumpiga; ndivyo, asemavyo Bwana Mungu; ndipo, upanga wa kila mtu utakapompiga ndugu yake.
22
Nami nitampatiliza kwa magonjwa mabaya na kwa kumwaga damu zao, tena nitanyesha mvua ifurikayo maji na mvua ya mawe na ya moto uchanganyikao na mawe ya viberitiberiti; hizo mvua nitamnyeshea yeye na vikosi vyake na yale makabila mengi, aliyo nayo.
23
Hivyo nitajitokeza kuwa mkubwa na mtakatifu, nijulikane machoni pa wamizimu wengi, nilivyo; ndipo, watakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana.
← Chapter 37
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 39 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48