bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Ezekiel 13
Ezekiel 13
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 12
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 14 →
1
Neno la Bwana likanijia la kwamba:
2
Mwana wa mtu wafumbuaji wa Isiraeli wanaowafumbulia yatakayokuwa wafumbulie wewe yatakayowajia. Waambie hao wafumbuaji wanaosema kwa hayo yaliyomo mioyoni mwao: Lisikieni neno la Bwana!
3
Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Wafumbuaji hawa wajinga watapatwa na mambo! Maana huzifuata roho zao, husema mambo, wasiyoyaona!
4
Kama mbweha walivyo kwenye mabomoko, ndivyo, wafumbuaji wako, Isiraeli, walivyo.
5
Hamkukwea hapo palipoatuka nyufa, wala hamkuuzungushia mlango wa Isiraeli boma, wapate kusimama kwenye mapigano, siku ya Bwana itakapokutia.
6
Wameona maono yasiyokuwako, nayo maaguo yao ni ya uwongo, wakisema: Ndivyo, asemavyo Bwana, lakini Bwana hakuwatuma, nao wakangojea, alitimize neno lao.
7
Je? Hamkuona maono yasiyokuwako? Hamkusema maaguo ya uwongo, mliposema: Ndivyo, asemavyo Bwana, nami nalikuwa sikuyasema?
8
Kwa hiyo Bwana Mungu anasema: Kwa kuwa mmesema yasiyokuwako, mkaona mambo ya uwongo, kwa hiyo mtaniona, nikiwajia ninyi; ndivyo, asemavyo Bwana Mungu.
9
Itakuwa, mkono wangu uwajie hao wafumbuaji walioona yasiyokuwako na kuagua uwongo; hawatakula bia nao walio ukoo wangu, wala hawataandikwa katika kitabu cha mlango wa Isiraeli, wala hawataiingia nchi ya Isiraeli; ndipo, watakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana Mungu.
10
Wanawapoteza mara kwa mara walio ukoo wangu wakisema: kumetengemana, lakini utengemano hauko; tena watu wakijenga boma wenyewe, hao utawaona, wakilipaka chokaa.
11
Kwa sababu hii waambie hao mafundi wa kupaka chokaa: Litaanguka! Itakunya mvua ifurikayo maji, nami nitanyesha mvua ya mawe, yaliangukie, hata upepo wa kimbunga utalibomoa;
12
ndipo, mtakapoona, hilo boma likianguka, nanyi mtaulizwa: Chokaa, mliyolipaka, iko wapi?
13
Kweli hivyo ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Kwani machafuko yangu yenye moto nitaleta upepo wa kimbunga wa kulibomoa, hata mvua ifurikayo maji itakunya kwa makali yangu, nayo mvua ya mawe ya kuangamiza itaanguka kwa yale machafuko yangu yenye moto.
14
Ndipo, nitakapolibomoa boma, mlilolipaka chokaa, nitaliangusha chini, msingi wake utokee; napo, litakapoanguka, mtaangamia huko katikati. Ndipo, mtakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana.
15
Hayo machafuko yangu yenye moto nitayamaliza huko katika hilo boma nako kwao waliolipaka chokaa, kisha nitawaambia: Hilo boma haliko tena, wala hao waliolipaka chokaa hawako tena.
16
Nao ndio waliokuwa wafumbuaji wa Isiraeli walioufumbulia Yerusalemu yatakayokuwa na kuupatia maono yenye utengemano, utengemano usipokuwa kabisa; ndivyo, asemavyo Bwana Mungu.
17
Wewe mwana wa mtu, uso wako uuelekezee wanawake wa ukoo wako wanaoagua kwa hayo yaliyomo mioyoni mwao, uwafumbulie yatakayowajia!
18
Sema: Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Watapatwa na mambo hao wanawake wanaoshona vitambaa vya uganga katika maungo yote ya mikono, wanaotengeneza hata miharuma ilinganayo na vichwa vya kila umbo, kusudi wapate kunasa roho za watu! Je? Mwataka kuzinasa roho zao walio ukoo wangu, mziokoe roho zenu wenyewe?
19
Mkanitia uchafu mbele yao walio wa ukoo wangu mkiweza kupata makufi mawili tu ya mawele au vipande vichache vya mkate; ndivyo, mnavyoziua roho za watu wasioipaswa na kufa, nazo roho za wengine wasiopaswa na kupona mnaziponya, mkiwaogopea walio ukoo wangu, wanaopenda kusikia maneno ya uwongo.
20
Kweli hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Mtaniona, nikivijia vitambaa vyenu vya uganga, mnavyovitumia vya kunasia roho za watu, kama ni ndege, nitavirarua mikononi mwenu, nizinasue zile roho za watu kwenda zao, ni zile roho, mlizozinasa, kama ni ndege.
21
Nayo miharuma yenu nitairarua, niwaokoe mikononi mwenu walio ukoo wangu, wasiwe mateka tena mikononi mwenu. Ndipo, mtakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana.
22
Kwa madanganyo yenu mmeiumiza mioyo yao waongofu, nisiowaumiza mimi, mkaishupaza mikono yao wasionicha, wasiweze kurudi katika njia zao mbaya, wapate uzima.
23
Kwa sababu hii hamtaona tena maono yasiyokuwako, wala hamtaagua tena maaguo, kwani walio ukoo wangu nitawaponya mikononi mwenu; ndipo, mtakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana.
← Chapter 12
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 14 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48