bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Ezekiel 29
Ezekiel 29
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 28
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 30 →
1
Katika mwaka wa 10 katika mwezi wa kumi siku yake ya kumi na mbili neno la Bwana likanijia la kwamba:
2
Mwana wa mtu, mwelekezee Farao, mfalme wa Misri, uso wako na kumfumbulia yote yatakayomjia yeye nayo nchi yake yote nzima ya Misri!
3
Sema ukimwambia: Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Utaniona, nikikujia, wewe Farao, mfalme wa Misri, uliye mamba mkubwa aoteaye katika majito yake katikati na kusema: Ni langu hili jito langu, nami nimelifanyizia kuwa langu!
4
Nitakutia ndoana kubwa katika taya zako, kisha nitawagandamanisha samaki wa majito yako magambani pako, nikupandishe na kukutoa ndani ya majito yako pamoja na samaki wote waliomo majitoni mwako, wakigandamana na magamba yako.
5
Kisha nitakubwaga nyikani wewe pamoja na samaki wote waliokuwamo majitoni mwako, hutaokotwa wala hutakusanywa, ila nitakutoa, nyama wa porini na ndege wa angani wakule.
6
Ndipo, wote wakaao Misri watakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana, kwa kuwa walikuwa kwao wa mlango wa Isiraeli kama mwanzi wa kujiegemezea.
7
Lakini walipokushika mikononi mwao, ukakunjika, ukawapasua mabega yao yote; tena walipojiegemeza kwako, ukavunjika na kuvilemaza viuno vyao vyote.
8
Kwa hiyo Bwana Mungu anasema hivi: Utaniona, nikikupelekea panga, niangamize kwako watu na nyama.
9
Ndipo, nchi ya Misri itakapokuwa peke yake kwa kuharibiwa, ndipo, watakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana, kwa kuwa alisema: Jito ni langu, mimi ndiye aliyelifanya.
10
Kwa hiyo utaniona, nikikujia wewe, hata majito yako, niitoe nchi ya Misri, iharibiwe kabisa, mpaka iwe peke yake tu kuanzia Migidoli kufikisha Siwene hata mipaka ya Nubi.
11
Hautapita kwake mguu wa mtu, wala mguu wa nyama hautapita kwake, wala hawatakaa watu miaka 40.
12
Nitaitoa nchi ya Misri kuwa peke yake katikati ya nchi nyingine zilizo peke yao nazo, nayo miji yake itakuwa peke yao katikati ya miji mingine iliyo mabomoko tu, itakuwa hivyo miaka 40. Nao Wamisri nitawatawanya kwenye mataifa mengine na kuwatupatupa katika nchi zao.
13
Kwani hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Miaka 40 itakapokwisha, nitawakusanya Wamisri na kuwatoa kwenye makabila ya watu, walikotawanyikia.
14
Ndipo, nitakapoyafungua mafungo yao Wamisri, niwarudishe katika nchi ya Patirosi, ndiyo nchi, waliyozaliwa; ndiko, watakakokuwa ufalme ukaao chini tu.
15
Katika nchi za kifalme nyingine itakaa chini tu, haitaweza kuyainukia mataifa tena, kwani nitawapunguza, wawe wachache tu, wasiyatawale mataifa.
16
Wala hawatakuwa tena egemeo lao mlango wa Isiraeli la kunikumbusha manza, walizozikora walipowageukia kuwafuata. Ndipo, watakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana Mungu.
17
Ikawa katika mwaka wa 27 siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza, ndipo, neno la Bwana liliponijia la kwamba:
18
Mwana wa mtu, Nebukadinesari, mfalme wa Babeli, amevitumikisha vikosi vyake utumishi mkubwa huko Tiro, mpaka vichwa vyote vikapata vipara, nayo mabega yote yakachubuka, lakini hakuna walichokipata huko Tiro, wala yeye wala vikosi vyake, kwa huo utumishi wao, waliomtumikia kule.
19
Kwa hiyo Bwana Mungu anasema hivi: Mtaniona, nikimpa Nebukadinesari, mfalme wa Babeli, nchi ya Misri, azichukue mali zao na kuyateka mateka yao na kuyapokonya mapokonyo yao; hayo yatakuwa mshahara wa vikosi vyake.
20
Kwa kumlipa kazi zake, alizozitumikia huko, nitampa nchi ya Misri, kwa kuwa amenifanyizia kazi; ndivyo, asemavyo Bwana Mungu.
21
Siku ile nitakuza pembe kwao wa mlango wa Isiraeli, nami nitakupa kukifunua kinywa chako katikati yao; ndipo, watakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana.
← Chapter 28
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 30 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48