bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Ezekiel 46
Ezekiel 46
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 45
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 47 →
1
Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Lango la ua wa ndani lielekealo maawioni kwa jua sharti liwe limefungwa siku sita za kazi, lakini siku ya mapumziko lifunguliwe, hata siku ya mwandamo wa mwezi lifunguliwe.
2
Mkuu akiingia penye ukumbi wa hilo lango toka nje, asimame hapo penye mhimili wa hilo lango, watambikaji waitengeneze ng'ombe yake ya tambiko ya kuteketezwa nzima nazo ng'ombe za tambiko za kushukuru, naye amwangukie Mungu penye kizingiti cha hilo lango, kisha atoke; kisha lango hilo lisifungwe mpaka jioni.
3
Nao watu wa nchi hii wamwangukie Bwana hapo pa kuliingilia hilo lango siku za mapumziko na za miandamo ya mwezi.
4
Nazo ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima, mkuu atakazomtolea Bwana siku za mapumziko, ziwe wana kondoo sita wasio na kilema na dume mmoja asiye na kilema.
5
Tena kilaji cha tambiko kiwe frasila moja ya unga kwa yule dume, lakini kwa wana kondoo kiwe, kama mkono wake utakavyotoa, tena pishi moja na nusu ya mafuta kwa kila frasila moja ya unga.
6
Siku ya mwandamo wa mwezi atatoa ndama ya ng'ombe ya kiume asiye na kilema na wana kondoo sita na dume moja, wote sharti wawe pasipo kilema.
7
Frasila moja ya unga kwa yule ndama, tena frasila moja ya yule dume la kondoo iwe kilaji cha tambiko, nacho cha wana kondoo kiwe, kama mkono wake utakavyoleta, tena kwa kila frasila ya unga pishi moja na nusu ya mafuta.
8
Mkuu akiingia aingie kwa njia ya ukumbi wa hilo lango, hata kutoka atoke kwa njia hiyohiyo.
9
Lakini watu wa nchi hii wakimtokea Bwana kumwangukia penye mikutano ya sikukuu, wao walioingia katika lango la kaskazini sharti watoke penye lango la kusini, nao walioingia katika lango la kusini sharti watoke penye lango la kaskazini, mtu asirudi kwa njia ya lango lile, aliloliingia, ila atoke kwa lile la ng'ambo.
10
Naye mkuu ataingia pamoja nao, wakiingia, kisha atatoka, nao wakitoka.
11
Penye sikukuu napo penye mikutano ya sikukuu kilaji cha tambiko kiwe frasila moja ya unga kwa kila ndama, vilevile frasila moja ya unga kwa kila dume la kondoo, lakini kwa wana kondoo kiwe, kama mkono wake utakavyotoa, tena pishi moja na nusu ya mafuta kwa kila frasila moja ya unga.
12
Kama mkuu anataka kumtolea Bwana kwa kupenda mwenyewe ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima au za kushukuru, basi, wamfungulie lile lango lielekealo maawioni kwa jua, azitoe ng'ombe zake za tambiko za kuteketezwa nzima nazo za kushukuru, kama anavyofanya siku za mapumziko, kisha atoke! Akiisha kutoka, na walifunge hilo lango.
13
Nawe umtolee Bwana kila siku mwana kondoo wa mwaka mmoja asiye na kilema kuwa ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima, ufanye hivyo kila kutakapokucha!
14
Hata kilaji cha tambiko sharti ukitoe kila kutakapokucha, kiwe pishi moja ya unga na vibaba viwili vya mafuta ya kumiminiwa katika huo unga uliopepetwa vizuri. Hiki kilaji cha tambiko cha Bwana kimeagizwa cha siku zote za kale na kale.
15
Sharti mtoe mwana kondoo nacho hicho kilaji cha tambiko pamoja na mafuta yake kila kutakapokucha kale na kale.
16
Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Kama mkuu anampa mmoja wao wanawe fungu la nchi yake, litakuwa lao hata wanawe, walishike, liwe fungu lao, walilolipata.
17
Lakini kama anampa mmoja wao watumishi wake fungu la nchi yake, aliyoipata, litakuwa lake mpaka mwaka mkuu wa ukombozi; ndipo, litakaporudi kwake mkuu; ni wanawe tu watakaokaa na fungu lake, liwe lao.
18
Tena mkuu asichukue fungu lililo la watu akiwakorofisha na kuwafukuza kwao. Lililo lake ni fungu lile tu, alilopewa kulishika, liwe lake, nalo ndilo, atakaloachia wanawe, kusudi walio ukoo wangu wasitawanyike, mtu akiweza kuondolewa katika fungu, alilolishika, liwe lake.
19
Akanipeleka hapo pa kuingia palipokuwa kando ya lile lango la kuviingilia vile vyumba vitakatifu vya watambikaji vielekeavyo kaskazini; hapo nikaona mahali pembeni panapoelekea baharini.
20
Akaniambia: Humu ndimo, watambikaji wanamopikia nyama za ng'ombe za tambiko za upozi nazo za weuo, tena ndimo, wanamochomea vilaji vya tambiko, kusudi wasivipeleke katika ua wa nje na kuwapatia watu utakatifu.
21
Kisha akanitoa na kunipeleka katika ua wa nje, akanipitisha penye pembe zake nne za huo ua; ndipo, nilipoona penye kila pembe ya huo ua ua mwingine.
22
Penye pembe zote nne za huo ua palikuwa na nyua zilizofungwa kwa ukuta, urefu wao ulikuwa mikono 40, nao upana 30, kipimo chao hizo nyua ni kimoja tu.
23
Zote nne zilizungukwa na ukuta wa mawe; chini penye hizo kuta kuzizunguka zote palikuwa pametengenezwa majiko.
24
Akaniambia: Hizi ndizo nyumba za wapishi, watumishi wa Nyumba hii walimopikia nyama za ng'ombe za tambiko za watu.
← Chapter 45
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 47 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48