bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Ezekiel 7
Ezekiel 7
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 6
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 8 →
1
Neno la Bwana likanijia la kwamba:
2
Wewe mwana wa mtu, hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyoiambia nchi ya Isiraeli: Mwisho uko! Huo mwisho unazijia pande zote nne za nchi hii.
3
Sasa mwisho unakujia, nikiyatuma makali yangu, yakujie, nikupatilizie njia zako zote na kukulipisha machukizo yako yote.
4
Jicho langu halitakuonea uchungu, wala mimi sitakuhurumia, kwani nitakulipisha njia zako, machukizo yako yatokee kwako katikati; ndipo, mtakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana.
5
Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Kibaya kimoja kitakapopita, mtaona, kibaya kingine kinakuja!
6
Mwisho unakuja! Mwisho huo unakuja, ukuamkie! Tazama tu: unakuja!
7
Siku yako mbaya inakuja ukaaye katika nchi hii; wakati unakuja, siku iko karibu, nayo ni ya mastuko, siyo ya kupiga vigelegele milimani.
8
Sasa bado kidogo nitakumwagia machafuko yangu yenye moto, niyatimize kwako makali yangu, nikikupatilizia njia zako na kukulipisha machukizo yako yote.
9
Jicho langu halitokuonea uchungu, wala mimi sitakuhurumia nikikulipisha njia zako, machukizo yako yatokee kwako katikati; ndipo, mtakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana apigaye.
10
Itazami hiyo siku! Utaiona, inakuja! Siku mbaya imetokea! Fimbo imechanua, majivuno yamechipuka.
11
Ukorofi umeinuka kuwa fimbo ya kuwapiga wasiomcha Mungu; hakuna chao kilichosalia, wala cha mali zao, wala cha urembo wao, wala cha utukufu wao, waliokuwa nao.
12
Wakati umekuja, siku imetimia, ndipo asifurahi mwenye kununua, wala asisikitike mwenye kuuza, kwani makali yenye moto yanazijia mali zao zote.
13
Kwani mwenye kuuza hatakipata tena alichokiuza, ingawa awepo na kukaa mwenye uzima, kwani hayo yaliyofumbuliwa kwa ajili ya mali zao zote hayageuki, kwa ajili ya manza, walizozikora, hakuna atakayejikalisha uzimani kwa nguvu zake.
14
Yapigeni tu mabaragumu na kuyatengeneza yote! Hakuna atakayekwenda vitani. Kwani makali yangu yenye moto yamezijia mali zao zote.
15
Panga ziko nje, magonjwa mabaya na njaa zimo nyumbani; alioko shambani atakufa kwa panga, naye aliomo mjini njaa na magonjwa yatamla.
16
Nao watakaopona kwa kukimbia watakuwa milimani kama hua walioko mabondeni, hao wote watakuwa wanalia kila mtu kwa manza zake yeye, alizozikora.
17
Mikono yote italegea, nayo magoti yote yatayeyuka kuwa kama maji.
18
Watajifunga magunia, wakipigwa na bumbuazi sana, nyuso zao zote, zitaiva kwa kuona soni, navyo vichwa vyao vyote vitakuwa vimenyolewa.
19
Fedha zao watazitupa barabarani, nazo dhahabu zao zitakuwa kama zenye uchafu, kwani dhahabu zao na fedha zao hazitaweza kuwaponya siku hiyo, Bwana atakapochafuka, wala hazitazishibisha roho zao, wala hazitayajaza matumbo yao, kwani ndizo zilizowaponza, wazikore manza zao.
20
Uzuri wa hayo mapambo yao ukawatia majivuno, wakayatumia kuvitengeneza vinyago vyao vichukizavyo kwa kutapisha kwao. Kwa hiyo nimezigeuza kuwa kwao kama zenye uchafu.
21
Kisha nitazipa mikononi mwa wageni, wazipokonye, namo mwao wasionicha katika nchi hii, waziteke, kisha wazichafue.
22
Nami nitaugeuza uso wangu, usipatazame, wakipachafua palipokuwa urembo wangu; ndipo, wanyang'anyi watakapopaingia, wapachafue.
23
Fanyiza minyororo! Kwani nchi hii imejaa mashauri ya damu, nao mji huu umejaa makorofi.
24
Nami nitaleta walio wabaya kuliko wamizimu wengine, wazichukue nyumba zao; nayo majivuno yao wenye nguvu nitayakomesha, patakatifu pao pakitiwa uchafu.
25
Mwangamizo unakuja; ndipo, watakapotafuta pa kuponea, wasipapate.
26
Teso litafuatwa na teso jingine, zile habari mbaya zitafuatwa na habari mbaya nyingine; ndipo, watakapotafuta mfumbuaji, azifumbue, lakini watambikaji watapotelewa na Maonyo, nao wazee hawatajua mizungu.
27
Mfalme ataomboleza, naye aliye mkuu kituko kitakuwa vazi lake, nayo mikono ya watu wa nchi hii itastushwa; nitakapowalipisha njia zao na kuwakatia shauri liyapasalo mashauri yao, ndipo watakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana.
← Chapter 6
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 8 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48