bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Ezekiel 48
Ezekiel 48
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 47
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
1
Haya ndiyo majina ya mashina: upande wa kaskazini kandokando ya njia ya Hetiloni kufika Hamati hata Hasari-Enani penye mpaka wa Damasko upande wa kaskazini kandokando ya Hamati ndiko kutakakokuwa fungu moja, la Dani toka upande wa maawioni kwa jua hata baharini.
2
Kwenye mpaka wa Dani toka upande wa maawioni kwa jua hata upande wa baharini ni fungu moja, la Aseri.
3
Kwenye mpaka wa Aseri toka upande wa maawioni kwa jua hata upande wa baharini ni fungu moja, la Nafutali.
4
Kwenye mpaka wa Nafutali toka upande wa maawioni kwa jua hata upande wa baharini ni fungu moja, la Manase.
5
Kwenye mpaka wa Manase toka upande wa maawioni kwa jua hata upande wa baharini ni fungu moja, la Efuraimu.
6
Kwenye mpaka wa Efuraimu toka upande wa maawioni kwa jua hata upande wa baharini ni fungu moja, la Rubeni.
7
Kwenye mpaka wa Rubeni toka upande wa maawioni kwa jua hata upande wa baharini ni fungu moja, la Yuda.
8
Kwenye mpaka wa Yuda toka upande wa maawioni kwa jua hata upande wa baharini kuwe fungu la kueuliwa, mtakalolitoa; upana wake uwe mianzi 25000, tena urefu uwe kama fungu moja jingine toka upande wa maawioni kwa jua hata upande wa baharini; tena huko katikati kuwe na Patakatifu!
9
Hata fungu la kueuliwa sharti mmtolee Bwana, urefu wake uwe mianzi 25000, tena upana wake uwe mianzi 10000.
10
Hilo fungu takatifu litakuwa lao watambikaji, wapate mahali penye kaskazini, urefu wake uwe mianzi 25000, nako upande wa baharini upana uwe mianzi 10000, nako upande wa maawioni kwa jua upana uwe mianzi 10000, tena kusini urefu uwe mianzi 25000, nako huko katikati kuwe na Patakatifu pa Bwana.
11
Fungu hilo liwe lao watambikaji waliotakaswa, walio wana wa Sadoki, walioyaangalia, niliyowaambia, wayaangalie; ndio wasiopotea hapo, wana wa Isiraeli walipopotea, kama Walawi walivyopotea.
12
Kwa hiyo hapo patakuwa fungu lao, ni kipande cha lile fungu la kueuliwa lililo nchi takatifu yenyewe kwenye mpaka wa Walawi.
13
Tena Walawi wapate kandokando ya mpaka wa watambikaji mahali penye urefu wa mianzi 25000, nao upana uwe mianzi 10000; urefu wote uwe mianzi 25000, nao upana wote uwe mianzi 10000.
14
Lakini nchi hiyo wasiiuze kipande tu, wala wasiibadili kipande kwa nchi nyingine, kusudi nchi hii iliyo ya kwanza kwa uzuri wasiitie mikononi mwa mwingine, kwani ni nchi takatifu ya Bwana.
15
Yale 5000 yatakayosalia kwa upana wa mianzi wa 25000 yawe mali ya huo mji wote, watu wapate pa kukaa na pa kulisha, huo mji wenyewe ukiwa katikati.
16
Vipimo vyake viwe hivyo: upande wa kaskazini mianzi 4500, upande wa kusini mianzi 4500, upande wa maawioni kwa jua mianzi 4500, upande wa baharini mianzi 4500.
17
Mahali pa mji pa kulisha pawe upande wa kaskazini mianzi 250, upande wa kusini mianzi 250, upande wa maawioni kwa jua mianzi 250, nako upande wa baharini mianzi 250.
18
Kisha patasalia kwa urefu kandokando ya lile fungu takatifu la kueuliwa mahali penye mianzi 10000 kuelekea maawioni kwa jua, na mianzi 10000 kuelekea baharini, ndipo kandokando ya lile fungu takatifu la kueuliwa; mahali hapo mazao yake yaliwe nao watumikiao mle mjini.
19
Hao watumikiao mle mjini watakuwa wa mashina yote ya Isiraeli, nao ndio watakaopalima hapo.
20
Fungu lote la kueuliwa, mtakalolitoa, liwe mianzi 25000 kwa pande zote nne, ndipo patakapokuwa fungu takatifu la kueuliwa pamoja na hilo fungu litakalokuwa lake huo mji.
21
Patakaposalia patakuwa pake mkuu upande wa huku na upande wa huko penye lile fungu takatifu la kueuliwa na penye lile fungu litakalokuwa lake huo mji kuifuata ile mianzi 25000 ya hilo fungu la kueuliwa mpakani kwenda upande wa maawioni kwa jua na upande wa baharini vilevile kuifuata ile mianzi 25000 kwenye mpaka uelekeao baharini sawasawa na mafungu mengine; hapo patakuwa pake mkuu. Hilo fungu takatifu la kueuliwa pamoja na Nyumba Takatifu itakuwa hapo katikati.
22
Fungu lao Walawi nalo fungu lake mji, yote mawili yatakuwa katikati katika fungu lake mkuu; hilo fungu lake litakuwa katikati kwenye mpaka wa Yuda na kwenye mpaka wa Benyamini.
23
Nayo mashina yaliyosalia mafungu yao ni haya: toka upande wa maawioni kwa jua hata upande wa baharini ni fungu moja, la Benyamini.
24
Kwenye mpaka wa Benyamini toka upande wa maawioni kwa jua hata upande wa baharini ni fungu moja, la Simeoni.
25
Kwenye mpaka wa Simeoni toka upande wa maawioni kwa jua hata upande wa baharini ni fungu moja, la Isakari.
26
Kwenye mpaka wa Isakari toka upande wa maawioni kwa jua hata upande wa baharini ni fungu moja, la Zebuluni.
27
Kwenye mpaka wa Zebuluni toka upande wa maawioni kwa jua hata upande wa baharini ni fungu moja, la Gadi.
28
Kisha mpaka wa Gadi upande wa kusini uelekeao kwenye jua kali utoke Tamari, ufike Kadesi penye Maji ya Magomvi, kisha ufuate mto kufika kwenye Bahari Kubwa.
29
Hizo ndizo nchi, mtakazoyagawanyia mashina ya Isiraeli kwa kupiga kura kuwapatia mafungu yatakayokuwa yao. Hayo ndiyo mafungu yao makuu; ndivyo asemavyo Bwana Mungu.
30
Pa kutokea mle mjini patakuwa hivyo: upande wa kaskazini utakuwa wa mianzi 4500.
31
Nayo malango ya mji yataitwa kwa majina ya mashina ya Isiraeli. Malango matatu yataelekea kaskazini: lango moja la Rubeni, lango moja la Yuda, lango moja la Lawi.
32
Nao upande wa maawioni kwa jua utakuwa wa mianzi 4500, nao utakuwa na malango matatu: lango moja la Yosefu, lango moja la Benyamini, lango moja la Dani.
33
Nao upande wa kusini utakuwa wa mianzi 4500, nao utakuwa na malango matatu: lango moja la Simeoni, lango moja la Isakari, lango moja la Zebuluni.
34
Nao upande wa baharini utakuwa wa mianzi 4500, nao utakuwa na malango matatu: lango moja la Gadi, lango moja la Aseri, lango moja la Nafutali.
35
Kuuzunguka mji wote itakuwa njia yenye urefu wa mianzi 18000. Jina lake huo mji litakuwa toka siku ile: Bwana yumo.
← Chapter 47
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48