bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Ezekiel 33
Ezekiel 33
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 32
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 34 →
1
Neno la Bwana likanijia la kwamba:
2
Mwana wa mtu, sema nao walio ukoo wako ukiwaambia: Kama ninailetea nchi panga, watu wa nchi hiyo watamchukua mtu mmoja miongoni mwao, wamweke kuwa mlinzi wao.
3
Atakapoziona panga, zikiijia hiyo nchi, atapiga baragumu, awaonye wale watu.
4
Lakini mtu akiisikiliza tu sauti ya baragumu pasipo kuonyeka, panga zitamkamata, nayo damu yake atatwikwa yeye kichwani.
5
Akiisikia sauti ya baragumu pasipo kuonyeka, damu yake atatwikwa yeye, lakini yeye aonyekaye ataiponya roho yake.
6
Lakini kama mlinzi anaona, panga zikija, asipige baragumu, watu hawaonyeki; basi, panga zikija, zikimkamata mtu mmoja tu wa kwao, yeye atakamatwa kwa ajili ya manza, alizozikora, lakini damu yake nitamlipisha mlinzi.
7
Wewe nawe, mwana wa mtu, nimekuweka kuwa mlinzi wa mlango wa Isiraeli, utakaposikia neno kinywani mwangu, sharti uwaonye na kuwaambia hilo neno langu.
8
Nikimwambia asiyenicha: Wewe usiyenicha, utakufa kabisa, nawe humwambii neno hili la kumwonya asiyenicha, aiache njia yake, basi, yeye asiyenicha atakufa kwa ajili ya manza, alizozikora, lakini damu yake nitaitaka mkononi mwako.
9
Lakini kama wewe ulimwonya asiyenicha kwa ajili ya njia yake na kumwambia, arudi na kuiacha hiyo njia yake, naye asiporudi na kuiacha hiyo njia yake basi, yeye atakufa kwa manza, alizozikora, lakini wewe utakuwa umeiponya roho yako.
10
*Kwa hiyo, wewe mwana wa mtu, uambie mlango wa Isiraeli: Ninyi husema hivi kwamba: Tukitwikwa mapotovu yetu na makosa yetu, sisi tutazimia tu; hivyo tutawezaje kupata uzima?
11
Waambie: Ndivyo, asemavyo Bwana Mungu: Hivyo, nilivyo Mwenye uzima, sipendezwi na kufa kwake asiyenicha, ila yeye asiyenicha, akirudi na kuiacha njia yake, apate uzima. Rudini! Rudini na kuziacha njia zenu mbaya! Kwa nini mnataka kufa, ninyi mlio mlango wa Isiraeli?
12
Nawe mwana wa mtu, waambie wana wa ukoo wako: Wongofu wa mwongofu hautamponya siku, atakapofanya mapotovu, wala asiyenicha hataangushwa kwa hivyo, asivyonicha, siku atakaporudi na kunicha, wala mwongofu hatapata uzima kwa wongofu wake siku, atakapokosa.
13
Nikimwambia mwongofu, ya kuwa atapata uzima, naye akiuegemea wongofu wake, afanye mapotovu, basi, wongofu wake wote hautakumbukwa tena, naye atakufa kwa ajili ya hayo mapotovu, aliyoyafanya.
14
Tena nikimwambia asiyenicha: Utakufa kabisa, naye akirudi na kuyaacha makosa yake, afanye yaliyo sawa yaongokayo:
15
yeye asiyenicha akirudisha aliyopewa ya kumwekea mtu, akilipa aliyoyanyang'anya watu, akiyafuata maongozi ya wenye uzima, basi, naye ataupata uzima wa kweli, asife kabisa.
16
Makosa yake yote, aliyoyakosa, hayatakumbukwa tena; kwa kuwa amefanya yaliyo sawa yaongokayo, ataupata uzima wa kweli.*
17
Wana wa ukoo wako husema: Njia ya Bwana hainyoki, lakini njia yao ndiyo isiyonyoka.
18
Mwongufu akirudi na kuuacha wongofu wake, afanye mapotovu, atakufa kwa ajili yao.
19
Tena asiyemcha Mungu akirudi, aje kumcha Mungu, afanye yaliyo sawa yaongokayo, basi, yeye atapata uzima.
20
Mkisema: Njia ya Bwana hainyoki, kwa hiyo nitawapatiliza ninyi mlio mlango wa Isiraeli kila mtu, kama njia zake zilivyo.
21
Ikawa katika mwaka wa 12 wa kuhamishwa kwetu siku ya tano ya mwezi wa kumi, ndipo, mtoro aliyetoka Yerusalemu aliponijia kuniambia: Umetekwa ule mji!
22
Lakini mkono wake Bwana ulikuwa juu yangu jioni kabla ya kuja kwake yule mtoro, naye alinifumbua kinywa, mpaka yule akinijia asubuhi; ndivyo, nilivyofumbuliwa kinywa, nisiwe tena bubu kabisa.
23
Neno la Bwana likanijia la kwamba:
24
Mwana wa mtu, watu wayakaliayo yale mabomoko katika nchi ya Isiraeli husema kwamba: Aburahamu alikuwa mmoja tu, akaipata nchi hii, iwe yake; nasi tulio wengi tulipewa nchi hii, iwe yetu.
25
Kwa hiyo waambie: Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Ninyi hula nyama zenye damu, tena huyaelekezea magogo yenu ya kutambikia macho yenu, tena humwaga damu za watu! Je? Hivyo mtaipata nchi hii, iwe yenu?
26
Ninyi hujishikiza kwa panga zenu, hufanaya machukizo mkichafua kila mtu mke wa mweziwe! Je? Hivyo mtaipata nchi hii, iwe yenu?
27
Sharti uwaambie hivi: Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Hivyo, nilivyo Mwenye uzima, wayakaliao yale mabomoko watauawa kwa panga, nao walioko shambani nitawatoa, waliwe na nyama wa porini, nao walioko vilimani ngomeni na mapangoni watakufa kwa magonjwa mabaya.
28
Nitaigeuza nchi hii kuwa mapori yaliyo peke yao, niyakomeshe majivuno yao ya nguvu zao, milima ya Isiraeli itakapokuwa peke yao, kwa kuwa hatapapita mtu.
29
Ndipo, watakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana, nitakapoigeuza nchi hii kuwa mapori yaliyo peke yao kwa ajili ya machukizo yote, waliyoyafanya.
30
Nawe mwana wa mtu, wana wao walio ukoo wako huzisimulia habari za kwako barazani namo milangoni mwa nyumba, husemezana kila mmoja na mwenziwe, kila mtu na ndugu yake kwamba: Njoni, msikie, kama ni neno gani lililotoka kwake Bwana!
31
Hivyo wanakujia kama watu wanaojijilia tu, kisha wao walio ukoo wangu hujikalia mbele yako, wayasikilize maneno yangu, lakini hawayafanyi; kwa vinywa vyao husema maneno mazuri ya kupendeza, lakini kwa kufanya hao hushika mioyoni mwao njia za kupata faida tu.
32
Tazama, wewe unakuwa kwao kama mtu mwenye sauti nzuri aimbaye wimbo wa kupendeza pamoja na kuupatanisha na marimba; huyasikia maneno yako, lakini hawayafanyi kabisa.
33
Hapo, yatakapotimia, - nayo yatatimia kweli, - ndipo, watakapojua, ya kuwa ni mfumbuaji aliyekuwa katikati yao.
← Chapter 32
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 34 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48