bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Ezekiel 8
Ezekiel 8
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 7
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 9 →
1
Ikawa katika mwaka wa sita siku ya tano ya mwezi wa sita nilipokuwa nimekaa nyumbani mwangu pamoja na wazee wa Yuda waliokaa mbele yangu, ndipo, mkono wa Bwana Mungu uliponiangukia.
2
Nilipotazama nikaona, kama ni sura ya mtu; toka hapo palipokuwa kama kiuno mpaka chini ni moto, tena toka penye kiuno mpaka juu kulionekana kuwa kama kumetuka kulikokuwa kama kwa shaba iliyong'aa sana.
3
Kisha akakunjua kilichofanana na mkono, akanishika kishungi cha kichwani, upepo ukanichukua kuwa katikati ya nchi na ya mbingu, ukanipeleka Yerusalemu katika maono ya Kimungu pa kuliingilia lango la ndani lilioelekea kaskazini; ndipo, palipokuwa pamewekwa kinyago cha wivu kilichotia wivu.
4
Nikauona hapo utukufu wa Mungu wa Isiraeli, kama nilivyouona katika ile mbuga ya bondeni.
5
Akaniambia: Mwana wa mtu yaelekeze macho yako upande wa kaskazini! Nilipoyaelekeza macho yangu upande wa kaskazini, nikakiona hicho kinyago cha wivu kaskazini langoni pa kuingia penye meza ya kutambikia.
6
Akaniambia: Mwana wa mtu, unayaona, hao wanayoyafanya? Ni machukizo makubwa, watu wa mlango wa Isiraeli wanayoyafanya hapa, niondoke Patakatifu pangu mwenda mbali. Tena utaona mengine yaliyo machukizo makubwa zaidi.
7
Kisha akanipeleka langoni penye ua; nilipotazama nikaona tundu moja ukutani.
8
Akaniambia: Mwana wa mtu, penya humu ukutani! Nikapenya mle ukutani, nikaona mlango mmoja.
9
Akaniambia: Ingia, uyaone hayo machukizo mabaya, hao wanayoyafanya hapo!
10
Basi, nikaingia; nilipotazama nikaona kila mfano wa wadudu na wa nyama watapishao, nayo magogo yote, wao wa mlango wa Isiraeli wanayoyatambikia, yalikuwa yamechorwa ukutani kupazunguka po pote.
11
Mbele yao walikuwa wamesimama wazee 70 wa mlango wa Isiraeli, naye Yazania, mwana wa Safani, alisimama katikati yao; kila mtu alishika chetezo mkononi mwake, mvuke wa moshi wa uvumba ukapanda juu.
12
Akaniambia: Umeyaona, mwana wa mtu, wazee wa mlango wa Isiraeli wanayoyafanya gizani kila mmoja katika vyumba vyake vya vinyago? Kwani husema: Hakuna Bwana anayetuona, Bwana ameondoka katika nchi hii.
13
Akaniambia: Utaona tena mengine yaliyo machukizo makubwa zaidi, hao wanayoyafanya.
14
Akanipeleka penye lango la kuingia Nyumbani mwa Bwana lililoko upande wa kaskazini, nikaona humo wanawake waliokaa wakimlilia Tamuzi.
15
Akaniambia: Umeyaona, mwana wa mtu? Utaona tena mengine yaliyo machukizo mabaya kuliko haya.
16
Akanipeleka katika ua wa ndani wa Nyumba ya Bwana, nikaona hapo pa kuliingilia Jumba la Bwana katikati ya ukumbi na meza ya kutambikia waume kama 25, walikuwa wameligeuzia Jumba la Bwana migongo yao, lakini nyuso zilielekea upande wa maawioni kwa jua, wakiliangukia jua na kuyaelekea maawio yake.
17
Akaniambia: Umeyaona, mwana wa mtu? Je? Kuyafanya haya machukizo, wanayoyafanya hapa, hakukuutoshea mlango wa Isiraeli? Imekuwaje, wakiieneza nchi makorofi ya kunikasirisha mara kwa mara? Watazame, jinsi wanavyoyashika yale machipuko ya miti mbele ya pua zao.
18
Mimi nami nitawatolea makali yangu yenye moto; jicho langu halitawaonea uchungu, wala mimi sitawahurumia; ingawa wanililie masikioni kwa sauti kuu, sitawasikia kabisa.
← Chapter 7
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 9 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48