bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Job 1
Job 1
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 2 →
1
Kulikuwa na mtu katika nchi ya usi, jina lake Iyobu. Mtu huyu alikuwa mnyofu wa kweli mwenye kumcha Mungu, nayo mabaya alikuwa ameyaepuka.
2
Kwake walizaliwa wana saba wa kiume na watatu wa kike.
3
Makundi yake yalikuwa mbuzi na kondoo pamoja 7000 na ngamia 3000 na majozi ya ng'ombe 500 na punda majike 500, hata watumwa wake wakawa wengi sana. Kwa hiyo yule mtu alikuwa mkuu kuliko watu wote waliokaa upande wa maawioni kwa jua.
4
Wanawe wa kiume walifanya nyumbani mwake kila mmoja sikukuu yake; ndipo, walipowaalika maumbu zao watatu kula na kunywa pamoja nao.
5
Ikawa, kila walipozila hizo sikukuu zao, Iyobu hutuma kwao, akawatakasa kesho yake asubuhi akiwatolea ng'ombe za tambiko, wao wote kila mtu yake, kwani Iyobu alisema: Labda wanangu wamekosa wakiacha kumcha Mungu mioyoni mwao. Hivyo ndivyo, Iyobu alivyovifanya siku zote.
6
Ikawa siku moja, wana wa Mungu walipokuja kumtokea Bwana, Satani naye akaja katikati yao.
7
Bwana akamwuliza Satani: Umetoka wapi? Satani akamjibu Bwana akisema: Natoka katika kutembea katika nchi na kujiendea huko na huko.
8
Bwana akamwuliza Satani: Umemwangalia mtumishi wangu Iyobu? Kwani katika nchi hakuna mtu kama yeye, ni mnyofu wa kweli mwenye kumcha Mungu, nayo mabaya ameyaepuka.
9
Satani akamjibu Bwana akisema: Je? Iyobu anamcha Mungu bure?
10
Wewe humwangalii mwenyewe na nyumba yake nayo yote yaliyo yake po pote? Ukazibariki kazi za mikono yake, nayo makundi yake yameieneza nchi.
11
Haya! Ukunjue mkono wako, uyapige yote yaliyo yake! Ndipo, atakapokutukana usoni pako.
12
Bwana akamwambia Satani: Tazama, yote yaliyo yake nakupa! Ila yeye mwenyewe tu usimguse kwa mkono wako! Ndipo, Satani alipotoka usoni pake Bwana.
13
Ikawa siku moja, wanawe wa kiume na wa kike walipokula sikukuu na kunywa nvinyo nyumbani mwa ndugu yao aliyezaliwa wa kwanza,
14
mjumbe akaja kwake Iyobu, akamwambia: Ng'ombe walipokuwa wanalima, nao punda walipolisha kando yao,
15
mara watu wa Saba wakatushambulia, wakawachukua, nao vijana wakawapiga kwa ukali wa panga zao, mimi nikapona peke yangu tu, nikupashe habari.
16
Huyu angali akisema, akaja mwingine, akasema: Moto wa Mungu umeanguka toka mbinguni, ukawaka kwenye mbuzi na kondoo, ukawala pamoja na vijana, mimi nikapona peke yangu tu, nikupashe habari.
17
Huyu angali akisema, akaja mwingine, akasema: Wakasidi wamekuja vikosi vitatu, wakatushambulia, wakawakamata ngamia, wakawachukua, nao vijana wakawapiga kwa ukali wa panga zao, mimi nikapona peke yangu tu, nikupashe habari.
18
Huyu angali akisema, akaja mwingine, akasema: Wanao wa kiume na wa kike walipokula sikukuu na kunywa nvinyo nyumbani mwa ndugu yao aliyezaliwa wa kwanza,
19
mara upepo mkubwa uliotoka upande wa nyika ukazipiga pembe zote nne za ile nyumba, ikawaangukia wale vijana, wakafa; mimi nikapona peke yangu tu, nikupashe habari.
20
Ndipo, Iyobu alipoinuka, akazirarua nguo zake, akajinyoa kichwa chake, akajitupa chini kumwangukia Mungu,
21
akasema: Nilipotoka tumboni mwa mama nilikuwa mwenye uchi, tena nitakapotoka huku nitakuwa mwenye uchi vilevile. Bwana ndiye aliyenipa, Bwana ndiye aliyeyachukua tena, Jina la Bwana na litukuzwe!
22
Katika mambo hayo yote Iyobu hakukosa, wala hakumwazia Mungu kuwa mwenye mambo yasiyopasa.
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 2 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42