bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Job 5
Job 5
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 4
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 6 →
1
Haya! Ita, kama yuko mtu anayekuitikia! Kwao walio watakatifu utamtokea nani?
2
Kwani majonzi humwua mjinga, nao wivu humwua mpuzi.
3
Mimi niliona mjinga, akishusha mizizi, lakini mara sikuwa na budi kuliapiza hilo kao lake.
4
Watoto wake hawakupata wokovu, uliwakalia mbali, Walipowaponda langoni, hakuwako mponya.
5
Mavuno yake yakaliwa na mwingine aliyekuwa na njaa, akayachukua na kuyatoa penye vitalu, ingawa ni vyenye miiba, nao wenye kiu huzitwetea mali zao.
6
Kwani upotovu hautoki uvumbini, wala usumbufu hauchipuki hapa nchini,
7
ila mtu huzaliwa, apate kusumbuka, awe kama cheche za moto zinazoruka juu.
8
Lakini aliye Mungu mimi ningemtafuta, naye Mungu ningemwambia shauri langu.
9
Hufanya mambo makuu yasiyochunguzika, vioja vyake havihesabiki:
10
hutoa mvua kuinyesha nchi, ayapatie mashamba maji ya juu.
11
Walio wanyenyekevu huwakweza, huwapandisha kuufikia wokovu wao wasikitikao.
12
Huyatangua mawazo yao walio werevu, mikono yao isiweze kufanya kifaacho.
13
Nao wenye ubingwa huwakamata kwa werevu wao, mashauri yao wapotovu yaangamie upesi.
14
Nao mchana wao huguiwa na giza, wapapasepapase mnamo saa sita, kama ni usiku.
15
Ndivyo, anavyowaokoa wamaskini, ukali wa upanga usiwaue, wala mikono ya wenye nguvu isiwashinde.
16
Hivyo ndivyo, kingojeo kinavyomtokea naye mnyonge, lakini uovu hufumbwa kinywa chake.
17
*Tazama! Mwenye shangwe ni mtu, Mungu anayemchapa! Kwa hiyo usikatae kuonywa na Mwenyezi!
18
Kweli yeye huumiza, lakini tena huuguza; atakapotia kidonda, mikono yake hukiponya.
19
Atakuokoa katika masongano sita, yawe hata saba, kisioneke kibaya kitakachokugusa.
20
Penye njaa atakukomboa namo kufani, hata vitani atakukomboa mikononi mwao wenye panga.
21
Penye mapigo ya ndimi za watu utafichika, usiogope hapo napo, mwangamizo utakapokuja;
22
utaucheka mwangamizo, hata njaa, nao nyama wakali wa nchi hutawaogopa.
23
Kwani nayo mawe ya mashambani utapatana nayo, nao nyama wa porini watatengemana huko, uliko.
24
Ndipo, utakapolijua hema lako kuwa lenye utengemano, napo utakapolitazama kao lako, hutaona kitakachokoseka.
25
Tena utayaona mazao yako kuwa mengi, navyo vizazi vya kwako vitakuwa vingi kama majani ya nchi.
26
Nguvu zako zitakuwa hazikupunguka, utakapoingia kaburini, kama viganda vinavyoingizwa, mavuno yanapotimia.*
27
Tazama! Haya tumeyachunguza kuwa hivyo kweli; yasikie, nawe upate kuyajua moyoni mwako! Iyobu akajibu akisema:
← Chapter 4
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 6 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42