bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Job 3
Job 3
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 4 →
1
Kisha Iyobu akakifumbua kinywa chake, akaiapiza siku yake;
2
yeye Iyobu akaanza kusema kwamba:
3
Siku niliyozaliwa ingalifaa, kama ingaliangamia, pamoja na usiku ule, waliposema: Mimba hii ni mtoto wa kiume.
4
Siku hiyo ingalifaa, kama ingalikuwa yenye giza, kama Mungu wa huko juu asingaliitafuta, kama mchana nao usingaliiangaza.
5
Giza lenye kivuli kiuacho na liitake kuwa lake, mawingu yenye weusi na yaikalie na kuifunika, yageuzayo mchana kuwa giza na yaipatie vituko.
6
Kama giza tupu lingaliupokonya, usiku ule nao ungalifaa, kama usingalihesabiwa katika siku za mwaka huo, wala kama usingaliingia katika hesabu ya miezi!
7
Ningeuona kuwa mwema, kama usingalizaa kitu, wala kama usingalisikia sauti ya shangwe.
8
Wajuao kuziloga siku sharti wauapize, ndio wao waliojipa mioyo kumchochea naye nondo wa baharini.
9
Nyota zake za mapambazuko na ziguiwe na giza, usione mwanga ukiungojea, wala vishale vya mapambazuko usivione,
10
kwa kuwa haukufunga mlango wa tumbo la mama yangu na kuyaficha masumbuko, macho yangu yasiyaone!
11
Mbona sikuweza kufa nilipotoka tumboni mwa mama? Mbona sikuzimia nilipotoka tumboni mwake?
12
Mbona nilipokelewa na kuwekwa magotini? Mbona nikapata maziwa ya kuyanyonya?
13
Kama sivyo, ningelala sasa na kutulia, ningelala usingizi na kujipatia mapumziko;
14
ningekuwa pamoja na wafalme na wenye hukumu wa nchi waliojijengea machuguu makubwa ya kuzikiwa humo;
15
au ningekuwa pamoja na wakuu waliokuwa wenye dhahabu, waliozijaza nyumba zao na kulimbika fedha;
16
au ningalikwisha kuchimbiwa tu kama mimba iliyoharibika, nisipate kuwapo kama wachanga wasiouona mwanga.
17
Huko ndiko, wanakokomea kuchafuka wasiomcha Mungu; ndiko, wanakopumzikia waliojichokesha kwa kuzitumia nguvu zao.
18
Huko wafungwa wote pamoja hutengemana, hawasikii tena sauti ya msimamizi.
19
Huko wadogo na wakubwa ni wamoja, nao watumwa wamekwisha kombolewa, wasiwe mali za mabwana zao.
20
Sababu gani anampa msumbufu kuona mwanga? Sababu gani anampa kuwapo mwenye uchungu rohoni?
21
Ndio wanaokingojea kifo, lakini hawakipati; kuliko vilimbiko vilivyofichwa hutaka kukizua.
22
Hao wangefurahi na kushangilia, wangechangamka kweli, kama wangeona kaburi.
23
Hao ni watu waliofichwa maana ya njia zao, wao ndio, Mungu aliowazibia mizungu yote pia.
24
Sharti kwanza nipige kite, ninapotaka kula, navyo vilio vyangu humwagika kama maji.
25
Kwani ninapostukia kistusho, hichohicho hunipata, nacho nilichokiogopa hunijia.
26
Sipati kutengemana wala kutulia wala kupumzika, kwani mahangaiko hunijia. Elifazi wa Temani akamjibu akisema:
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 4 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42