bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Job 15
Job 15
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 14
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 16 →
1
Yuko mwerevu wa kweli atakayejibu yenye ujuzi ulio kama upepo?
2
Au yuko atakayelijaza tumbo lake upepo utokao maawioni kwa jua?
3
Atamwonya mwenziwe kwa maneno yasiyofaa? Au atajisemea tu kwa mapuzi yasiyompatia mtu kitu?
4
Kisha wewe unatangua kicho kiwacho chote, nayo mawazo ya kumnyenyekea Mungu unayabeua.
5
Manza, ulizozikora, zinakifunza kinywa chako, ukachagua ulimi usemao yenye ujanja.
6
Kinachokuumbua kuwa mwovu, si mimi, ni kinywa chako, nayo midomo yako ndiyo inayokusuta.
7
Je? Mtu wa kwanza aliyezaliwa ni wewe? Au ulitoka tumboni mwa mama, milima ilipokuwa haijawa?
8
Je? Ulizisikiliza njama za Mungu? Je? Ndiko, ulikouvuta werevu wa kweli, ukujie wewe?
9
Unajua mambo gani, tusiyoyajua nasi? Unao utambuzi gani usiopatikana kwetu?
10
Wenye mvi walio wazee nako kwetu sisi wako, siku zao ni nyingi sana kuliko hizo za baba yako.
11
Je? Hivyo, Mungu anavyotuliza mioyo, unaviwazia kuwa vidogo? Nalo neno la upole si kitu kwako?
12
Mbona moyo wako unakuchukua, ukupeleke penginepo? Mbona macho yako unayang'arisha hivyo?
13
Inakuwaje, ukiigeuza roho yako, ije kumpingia Mungu, ukamtolea maneno kama hayo kinywani mwako?
14
Mtu ndio nini, aweze kutakata? Aliyezaliwa na mwanamke awezaje kuongoka?
15
Kumbuka hili tu: nao watakatifu wake hawezi kuwategemea, nazo mbingu hazitakati machoni pake!
16
Sembuse mtu amchukizaye kwa upotevu, yeye mtu afanyaye maovu, kama ni kunywa maji tu!
17
Nitakufunza, nisikilize! Niliyoyaona, na niyasimulie.
18
Werevu wa kweli wanayoyatangaza ni yayo hayo, kwani waliyoambiwa na baba zao hawakuyasahau;
19
walikuwa wamepewa nchi hii wao peke yao tu, wala hakuwako mgeni aliyepita kwao.
20
Walisema: Asiyemcha Mungu hukaa siku zote na uchungu wake, vilevile mkorofi miaka yote, aliyowekewa na kuhesabiwa.
21
Sauti za mastusho huingia masikioni mwake, akikaa na kutengemana, mwangamizaji humjia.
22
Hayategemei, ya kwamba atatoka gizani, hujiwazia kuwa amechaguliwa kuuawa na upanga.
23
Hutangatanga kujipatia chakula, lakini akione wapi? Anajua, ya kuwa kando yake imekwisha kuwekwa siku ya giza.
24
Mateso na masongano humtia woga, nayo humshinda kwa nguvu kama za mfalme aliyejiweka tayari kupiga vita.
25
Kwa kuwa ameukunjua mkono wake, ampingie Mungu, akajivunia kuwa mwenye uwezo mbele yake Mwenyezi.
26
Akapiga mbio na kunyosha shingo, aje kumshinda, akijikingia ngao yake yenye vitovu
27
Akaunonesha uso wake kuwa wenye mafuta, navyo viuno vyake akavinenepesha.
28
Katika miji iliyotakiwa kuwa mahame ndimo, alimotua, akakaa katika nyumba, ambazo watu hawazikai, ndizo zinazongoja tu kuwa machungu ya mawe.
29
Kwa hiyo hatapata mali nyingi, nazo atakazozipata hazitakaa, wala mazao yake hayatafurikia katika nchi hii.
30
Hatapata kuondoka mle gizani, nayo machipukizi yake hukaushwa na ndimi za moto, naye atatoweshwa kwa nguvu za pumzi za kinywa chake Mungu.
31
Asitegemee mambo yaliyo ya bure, maana atadanganyika, nayo yatakayokuwa malipo yake yatakuwa ya bure.
32
Siku yake ikiwa haijatimia bado, hayo yatatimia, shina lake halitapata kabisa, litakapochipuka tena.
33
Kama mizabibu inavyopukutisha mapooza yao, au kama michekele inavyopakatisha maua yao,
34
hivyo utakuwa mlango wake ambezaye Mungu, utakosa wazao wo wote, nao moto utayala mahema yao waliowapenyezea watu.
35
Mateso ndio mimba zao, kwa hiyo huzaa maovu, hivyo matumbo yao hutoa udanganyifu. Iyobu akajibu akisema:
← Chapter 14
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 16 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42