bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Job 32
Job 32
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 31
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 33 →
1
Hao watu watatu walipoacha kumjibu Iyobu, kwa kuwa alikuwa mwongofu machoni pake,
2
ndipo, makali ya Elihu wa Buzi, mwana wa Barakeli wa mlango wa Ramu, yalipowaka moto, naye Iyobu ndiye, makali yake yaliyemwakia, kwa kuwa alijiwazia rohoni mwake kuwa hakumkosea Mungu.
3
Nao wale wenzake watatu makali yake yakawawakia, kwa kuwa hawakuona tena la kumjibu Iyobu la kumwumbua kuwa amekosa.
4
Lakini Elihu alikawia kusema na Iyobu, kwani wale walikuwa wakubwa kumpita yeye kwa siku zao.
5
Elihu alipoona, ya kuwa hakuna jibu tena litokalo vinywani mwao wale watatu, makali yake yakawaka kama moto.
6
Ndipo, Elihu wa Buzi, mwana wa Barakeli, alipojibu, akasema: Mimi ni mdogo kwa miaka, ninyi m wazee, kwa hiyo nimejizuia, nikaogopa kuwaelezea ninyi, ninayoyajua mimi.
7
Nilisema: Wenye uzee na waseme, walio na miaka mingi na waujulishe werevu wa kweli.
8
Lakini kinachowapa watu utambuzi ni roho iliyomo mwao pamoja na pumzi yake yeye Mwenyezi.
9
Lakini wazee wenye miaka mingi sio wanaoerevuka kweli, wao wazee sio wanaoyajua mashauri yaliyo sawa.
10
Kwa hiyo nasema: Nisikilizeni, mimi nami niyaeleze, ninayoyajua!
11
Tazameni! Nimeyangojea maneno yenu, nikausikiliza utambuzi wenu, mlipouchunguza, mvumbue, hayo mambo yalivyo.
12
Ninyi nimewaangalia sana, hii ni kweli; lakini nilipotazama sikumwona aliyemshinda Iyobu, wala mmoja wenu hakuweza kumjibu aliyoyasema.
13
Msiseme: Kwa kuwa ni mwenye werevu wa kweli, tumeona, atakayemshinda ni Mungu, si mtu.
14
Hajajiweka tayari kusema na mimi, lakini kama ninyi mlivyosemeana naye, sitamjibu hivyo.
15
Ndipo, walipostuka, hawakujibu tena, wakawa wamepotelewa na maneno ya kusema.
16
Walipokuwa hawasemi neno, nikangoja, lakini wakasimama tu pasipo kujibu tena.
17
Basi, nami na nijibu fungu langu, nami na niyaeleze, ninayoyajua.
18
Kwani nimejaa maneno ya kusema, roho yangu humu ndani yangu imesongeka, mpaka niyatoe.
19
Tazameni: Tumbo langu linafanana na mvinyo isiyofunguliwa njia, ni kama viriba vipya vinavyotaka kupasuka.
20
Na niseme, humu ndani mpanuke kidogo tu, na niifumbue midomo yangu, nijibu nami.
21
Sitaki kupendelea uso wa mtu, wala maneno yaliyo mafuta ya midomo tu sitamwambia mtu,
22
kwani yaliyo mafuta ya midomo tu sijui kuyasema, muumbaji wangu angeniondoa upesi sana.
← Chapter 31
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 33 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42