bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Job 39
Job 39
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 38
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 40 →
1
Je? Unajua wakati, minde wanapozalia, au umeangalia, majike ya kulungu wanapopatia mimba?
2
Miezi yao ya kuwa wenye mimba umekwisha kuihesabu? Tena unajua wakati, wanapozalia?
3
Huchutama, kisha huwazaa watoto wao, huko ndiko kuukomesha uchungu wao.
4
Watoto wao hupata nguvu kwa kukua penye mapori matupu; wakijiendea na kutoka kwao hawarudi tena.
5
Ni nani aliyewatuma punda milia kujiendea tu? au ni nani aliyeyafungua mafungo yao vihongwe?
6
Si mimi niliyewapa nyika kuwa nyumba zao nalo jangwa la chumvi kuwa makao yao?
7
Wao huyacheka makelele yaliyomo mijini, maana hawazisikii tena sauti za ukorofi za wasimamizi.
8
Milimani ndiko, wanakojionea malisho yao, vijani vibichi vyote huvifuatafuata.
9
Je? Nyati atapendezwa akikutumikia? Atatafuta kilalo cha kuwamo zizini mwako?
10
Je? Unaweza kumfunga nyati kwa kamba, akulimie matuta, akikufuata na kulivuta jembe mabondeni pako?
11
Kwa kuwa nguvu zake ni nyingi, unaweza kumwegemea, umwachie kazi zako za shambani?
12
Atayapeleka mazao yako nyumbani, ukimtegemea hivyo? Au yaliyomo chanjani mwako atayakusanya vema?
13
Mabawa ya mbuni huchezacheza, lakini je? Hayo mabawa na manyoya yake yako na upole?
14
Kwani mayai yake huyaacha hapo mchangani, huo mchanga uyaangue kwa joto lake;
15
husahau, ya kama labda mguu utapapita utakaoyakanyaga, au nyama wa porini atayapondaponda.
16
Watoto wake huwakuza kwa ukali, kama sio wake, haogopi kwamba: Labda hautafaa huo utunzaji wake.
17
Kwani Mungu humsahaulisha werevu wa kweli, wala hakumgawia utambuzi wo wote.
18
Lakini anapoyapigapiga mabawa yake, aondoke, humcheka naye farasi pamoja naye ampandaye.
19
Je? Ni wewe uliyempa farasi nguvu zake kubwa? Je? Ni wewe uliyemvika singa za shingoni?
20
Je? Ni wewe unayemtuma, aogopeshe watu akiruka kwa mara moja kama nzige na kufoka sana?
21
Huparapara bondeni akizifurahia nguvu zake, hutoka kwenda kukutana nao washikao mata.
22
Hucheka waoga, maana hastuki, wala penye panga harudi nyuma.
23
Podo hupiga kelele juu yake, nayo mikuki imetukayo pamoja na chembe za mishale.
24
Akichafuka kwa ukali humeza nchi, baragumu likilia, hasimami,
25
ila kila anapolisikia baragumu husema: Haya! Toka mbali hunusa, mapigano yaliko, akiyasikia matangazo ya wakuu na makelele ya vikosi.
26
Je? Ni kwa utambuzi wako kipanga akiruka angani na kuyanyosha mabawa yake kwenda kusini?
27
Au ni kwa agizo lako, tai akipaa juu sana na kujitengenezea kiota cha mahali palipo juu?
28
Hutua penye miamba, apate kulala magengeni juu; ngome yake ilipo, ndipo papo hapo.
29
Toka huko juu huchungulia akitafuta chakula, macho yake huyaona nayo yaliyoko mbali.
30
Makinda yake hufyonza damu, napo panapo nyamafu yupo hapo. Bwana akamjibu Iyobu akisema:
← Chapter 38
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 40 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42