bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Job 41
Job 41
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 40
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 42 →
1
Je? Unaweza kumvua nondo wa baharini kwa ndoana au kuufunga ulimi wake kwa kamba katika taya la chini?
2
Au utaweza kumtia ugwe puani mwake? Au utaweza kulitoboa shavu lake kwa kulabu?
3
Je? Atazidi kukulalamikia? Au atakuambia maneno ya upole?
4
Atafanya agano na wewe, umchukue, awe mtumishi wako kale na kale?
5
Je? Utamchezesha kama ndege, ukimfunga wa kufurahisha vijana wa kike?
6
Chama cha wavuvi kinamchuuzia na kuwagawanyia wachuuzi vipande vipande?
7
Je? Utaweza kueneza mikuki ngozini pake au kichwani pake vyusa vya wavuvi?
8
Haya! Mpelekee mkono wako, umkamate! Ndipo, utakapolikumbuka pigano hilo, usilirudie tena.
9
Tazama! Hicho kingojeo cha kumkamata ni uwongo, ukimtazama tu utakufa ganzi.
10
Hakuna ajipaye moyo wa kumwamsha; tena yuko nani atakayesimama usoni pangu, mimi Mungu?
11
Yuko nani aliyeanza kunipa kitu, nimlipe? Yote pia yaliyoko chini ya mbingu ni yangu mimi.
12
Sitanyamaza, nisiseme, jinsi viungo vyake vilivyo, nazo nguvu zake, jinsi zilivyo kubwa, nayo matengenezo yake, jinsi yalivyo mazuri.
13
Yuko nani awezaye kulichuna vazi lake? Yuko nani atiaye mkono katika mataya yake yenye meno mawilimawili?
14
Yuko nani awezaye kuifungua milango ya kinywa chake? Kwani pande zote zinayo meno yaogopeshayo.
15
Magamba yake ni mazuri mno kwa hivyo, yanavyojipanga: kama ni kukazwa kwa nguvu ya chapa, hugandamana karibukaribu,
16
hushikamana kabisa kila moja na mwenzake, upepo tu usiweze kupita katikati yao.
17
Kweli kila moja linagandamana na mwenzake, yanashikana kwa nguvu, yasitengeke.
18
Akienda chafya humulikisha mwanga, nayo macho yake yanafanana nayo makope ya mapambazuko.
19
Mienge ya moto hutoka kinywani mwake, nayo hurukisha macheche ya moto.
20
Katika mianzi ya pua yake hutoka moshi kama wa chungu kichemkacho au wa moto wa matete.
21
Pumzi yake huunguza kama makaa yenye moto, hata miali ya moto hutoka kinywani mwake.
22
Shingoni pake ndipo, nguvu zinapokaa, mbele yake yako matetemeko na mastusho.
23
Manofu ya mwili wake yanashupaa, kwa kukazana hapo, yalipo, hayatikisiki.
24
Moyo wake nao ni mgumu kama jiwe, ugumu wake ni kama wa jiwe la chini la kusagia.
25
Akiinuka, nao wenye nguvu hushikwa na woga, kwa kustushwa hukosa njia ya kukimbilia.
26
Ukimpiga kwa upanga haumwingii, wala mkuki wala mshale wala chuma cho chote.
27
Chuma hukiwazia kuwa jani kavu, nayo shaba huiwazia kuwa mti uliobunguka.
28
Mishale ya upindi haiwezi kumkimbiza, nayo mawe ya kombeo kwake hugeuka kuwa kama makapi.
29
Marungu huwaziwa naye kuwa mabua makavu, tena huicheka shindo ya mkuki, ukitupwa.
30
Upande wake wa chini una vigae vyenye pembe, alipogaagaa ni kama matopeni, palipopita gari la kupuria.
31
Hukichafua nacho kilindi, kiwe kama chungu kinachochemka; huivuruga nayo bahari, iwe kama dawa, zikivurugwa chunguni.
32
Nyuma yake hiyo njia, aliyoishika, huangazika, hilo povu la kilindi mtu angeliwazia kuwa mvi.
33
Huku nchini hakuna afananaye naye; alichoumbiwa, ni hiki: asistuke kamwe!
34
Wote walio wakuu huwatazama tu, kuliko wenye majivuno wote mfalme ndiye yeye. Iyobu akamjibu Bwana akisema:
← Chapter 40
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 42 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42