bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Genesis 1
Genesis 1
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 2 →
1
Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi.
2
Nayo nchi ilikuwa peke yake pasipo kitu, nalo giza lilivifunika vilindi, nayo Roho Ya Mungu ilikuwa imejitanda juu ya maji.
3
Mungu akasema: Na uwe mwanga! Ndipo, mwanga ulipokuwa.
4
Mungu akauona mwanga kuwa mwema, kisha Mungu akatenganisha mwanga na giza;
5
mwanga Mungu akauita mchana, nalo giza akaliita usiku. Pakawa jioni, pakawa asubuhi, ndio siku ya kwanza.
6
Mungu akasema: Na uwe utando katikati ya maji, uyatenganishe maji na maji!
7
Mungu akaufanya utando, akayatenga maji yaliyoko chini ya utando nayo maji yaliyoko juu ya utando; yakawa hivyo.
8
Utando Mungu akauita mbingu. Pakawa jioni, pakawa asubuhi, ndio siku ya pili.
9
Mungu akasema: Maji yaliyoko chini ya mbingu na yakusanyike mahali pamoja, pakavu paonekane! Yakawa hivyo.
10
Mungu akapaita pakavu nchi, nalo kusanyiko la maji akaliita bahari. Mungu akayaona kuwa mema.
11
Kisha Mungu akasema: Nchi na ichipuze machipuko: mboga ziletazo mbegu na miti ya matunda iletayo matunda, kila mmmoja kwa namna yake, nayo yawe yenye mbegu zao ndani yao za kupandwa katika nchi. Yakawa hivyo.
12
Ndipo, nchi ilipotoa machipuko: mboga ziletazo mbegu kwa namna zao na miti iletayo matunda, kila mmoja kwa namna yake, nayo yalikuwa yenye mbegu zao ndani yao, Mungu akayaona kuwa mema.
13
Pakawa jioni, pakawa asubuhi, ndio siku ya tatu.
14
Mungu akasema: Na iwe mianga penye utando wa mbingu ya kuutenga mchana na usiku, iwe vielekezo vya kujulisha sikukuu na siku nyingine na miaka;
15
nayo iwe mianga utandoni kwa mbingu ya kuiangaza nchi! Yakawa hivyo.
16
Mungu akaifanya mianga miwili iliyo mikubwa: mwanga mkubwa wa kuutawala mchana nao mwanga mdogo wa kuutawala usiku pamoja na nyota.
17
Mungu akaiweka utandoni kwa mbingu, ipate kingaza nchi
18
na kuutawala mchana na usiku, na kuutenga mwanga na giza. Mungu akayaona kuwa mema.
19
Pakawa jioni, pakawa asubuhi, ndio siku ya nne.
20
Mungu akasema: Maji na yajae viumbe vya kuwa humo vyenye uzima, hata ndege na waruke juu ya nchi chini ya utando wa mbingu!
21
Mungu akawaumba nyangumi wakubwa na viumbe vyote wanaokaa majini na kutembea humo, kila mmoja kwa namna yake, nao ndege wote warukao kwa mabawa, kila mmoja kwa namna yake.
22
Mungu akawabariki kwamba: Zaeni, mwe wengi, mjae majini baharini, nao ndege na mawe wengi katika nchi!
23
Pakawa jioni, pakawa asubuhi, ndio siku ya tano.
24
Mungu akasema: Nchi na itoe viumbe vyenye uzima vya kila namna, nyama wa nyumbani na wadudu na nyama wa porini wa kila namna! Yakawa hivyo.
25
Mungu akawafanya nyama wa porini kila mmoja kwa namna yake na wadudu wote wa nchi kila mmoja kwa namna yake. Mungu akayaona kuwa mema.
26
Kisha Mungu akasema: na tufanye mtu kwa mfano wetu, afanane na sisi, awatawale samaki wa baharini na ndege wa angani na nyama na nchi yote nzima na wadudu wote watambaao katika nchi!
27
Mungu akamwumba mtu kwa mfano wake, mfano wake Mungu ndio, aliomwumbia, akamwumba kuwa mume na mke.
28
Mungu akawabariki, Mungu akawaambia: Zaeni wana, mwe wengi, mwijaze nchi, kisha mwitiishe! Watawaleni samaki wa baharini na ndege wa angani na nyama wote pia watambaao katika nchi!
29
Kisha Mungu akasema: Tazameni, nimewapa ninyi mboga zote zenye mbegu zilizoota katika nchi na miti yote izaayo matunda yenye mbegu ndani yao kuwa chakula chenu ninyi!
30
Nao nyama wote wa nchi na ndege wote wa angani nao wote watambaao katika nchi walio viumbe vyenye uzima, nao chakula chao ni majani yote yanayolika. Yakawa hivyo.
31
Mungu alipoyatazama yote, aliyoyafanya, akayaona kuwa mema sana. Pakawa jioni, pakawa asubuhi, ndio siku ya sita.
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 2 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50