bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Genesis 42
Genesis 42
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 41
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 43 →
1
Yakobo alipoona, ya kuwa Misri vyakula viko, Yakobo akawaambia wanawe: Mbona mnatazamiana?
2
Akasema: Tazameni, nimesikia, ya kuwa Misri vyakula viko! Telemkeni kwenda huko, mtununulie ngano huko, tupate kupona, tusife!
3
Basi, kaka zake Yosefu kumi wakatelemka kununua ngano kule Misri.
4
Lakini Benyamini, nduguye Yosefu, Yakobo hakumtuma kwenda na kaka zake, kwani alisema: Labda ataona kibaya njiani.
5
Wana wa Isiraeli wakaingia katikati yao wengine waliokwenda kununua ngano, kwani njaa ilikuwa imeingia hata katika nchi ya Kanaani.
6
Naye Yosefu alikuwa mtawala nchi hiyo, naye ndiye aliyewauzia ngano watu wote wa nchi hiyo. Kaka zake Yosefu walipofika kwake wakamwinamia, mpaka nyuso zao zikifika chini.
7
Yosefu alipowaona kaka zake akawatambua, lakini akajitendekeza, kama hawajui, akasema nao maneno magumu, akawauliza: Mmetoka wapi? Wakasema: Tumetoka katika nchi ya Kanaani kuja huku kununua ngano.
8
Ijapo Yosefu aliwatambua, wao hawakumtambua.
9
Ndipo, Yosefu alipozikumbuka ndoto zake, alizoziota kwa ajili yao, kisha akawaambia: Mu wapelelezi, mmekuja kutazama, nchi hii inakokuwa wazi.
10
Wakamwambia: Sivyo, bwana wetu. Watumwa wako wamkuja tu kununua ngano.
11
Sisi sote tu wana wa mtu mmoja, sisi tu watu wa kweli; watumwa wako hawajawa bado wapelelezi.
12
Lakini akawaambia: Sivyo, mmekuja kutazama, nchi hii inakokuwa wazi.
13
Ndipo, waliposema: Sisi watumwa wako tulikuwa ndugu kumi na wawili, wana wa mtu mmoja katika nchi ya Kanaani; na sasa mdogo wetu yuko kwa baba yetu, lakini mmoja hayupo.
14
Lakini Yosefu akwaambia: Ni hivyo, nilivyowaambia kwamba: Mu wapelelezi.
15
Kwa neno hili nitawajaribu: Hivyo, Farao alivyo mzima, hamtatoka huku, ndugu yenu mdogo asipokuja huku.
16
Toeni mmoja miongoni mwenu, aende kumchukua ndugu yenu! Nanyi wengine mtafungwa. Hivyo mtaumbuliwa, kama maneno yenu ni ya kweli, au kama sivyo; hivyo, Farao alivyo mzima, mu wapelelezi.
17
Kisha akawafunga kifungoni siku tatu.
18
Siku ya tatu Yosefu akawaambia: Fanyeni hivi, mpate kupona! Kwani mimi ni mtu mwenye kumcha Mungu.
19
Kama ninyi m watu wa kweli, mwenzenu mmoja tu afungwe kifungoni! Lakini ninyi wengine nendeni kupeleka ngano za kuondoa njaa nyumbani mwenu!
20
Kisha sharti mniletee ndugu yenu mdogo, maneno yenu yajulike kuwa ya kweli, msife. Wakafanya hivyo.
21
Ndipo, waliposemezana wao kwa wao: Kweli hapa tunalipishwa tuliyomkosea ndugu yetu. Tulipoona, roho yake ilivyosongeka, naye alipotulalamikia, hatukumsikia. Kwa sababu hii hangaiko hili limetupata.
22
Rubeni akawajibu kwamba: Sikuwaambia ninyi kwamba: Msimkosee mtoto? Lakini mlikataa kunisikia; sasa mnaona, damu yake inalipizwa.
23
Nao hawakujua, ya kuwa Yosefu amewasikia, kwa kuwa walikuwa wanaye mkalimani.
24
Ndipo, Yosefu alipoondoka kwenda kulia machozi. Aliporudi kusema nao, akamchukua Simeoni, akamfunga machoni pao.
25
Kisha Yosefu akaagiza watu, wavijaze vyombo vyao ngano, nazo fedha zao za kila mmoja wazirudishe katika gunia lake, wawape hata pamba za njiani; nao wale wakawafanyizia hivyo.
26
Kisha wakawachukuza punda wao mizigo yao ya ngano, wakatoka huko kwenda zao.
27
Walipofika kambini, mmoja wao akalifungua gunia lake, ampe punda chakula, akaziona fedha zake hapo juu ndani ya gunia lake.
28
Akawaambia ndugu zake: Kumbe fedha zangu zimerudishwa, zimo ndani ya gunia langu! Ndipo, mioyo yao ilipopigwa bumbuazi kwa kustuka, wakaambiana wao kwa wao: Mbona Mungu anatufanyizia haya?
29
Waliporudi kwa baba yao Yakobo katika nchi ya Kanaani wakamsimulia yote yaliyowapata njiani, wakasema:
30
Yule bwana wa nchi hiyo ametuambia maneno magumu, akatusingizia kuwa watu wa kuipeleleza nchi hiyo,
31
tukamwambia: Sisi tu watu wa kweli, hatujawa bado wapelelezi;
32
sote tulikuwa ndugu kumi na wawili, wana wa baba yetu mmoja, naye mdogo sana yuko kwa baba yetu katika nchi ya Kanaani.
33
Ndipo, yule bwana wa nchi hiyo alipotuambia: Hivi nitajua, ya kuwa m wakweli: mwenzenu mmoja mwacheni huku kwangu! Kisha chukueni vilaji vya kuondoa njaa nyumbani mwenu, mwende zenu!
34
Kisha sharti mniletee ndugu yenu mdogo, nipate kujua, ya kuwa hamu wapelelezi, ya kuwa mu wakweli; ndipo, nitakapowapa naye ndugu yenu, nanyi mtaweza kuchuuza katika nchi hii.
35
Ikawa walipoyamimina magunia yao wakaona kila mtu kifuko chake cha fedha katika gunia lake; walipoona, ya kuwa ni vifuko vya fedha zao kweli, wakashikwa na woga wote, wao na baba yao.
36
Ndipo, baba yao Yakobo alipowaambia: Mwaninyang'anya wana wangu wote. Yosefu hayupo, Simeoni hayupo, sasa mnataka kumchukua Benyamini naye. Haya yote yamenipata!
37
lakini Rubeni akamwambia baba yake: Wanangu wawili utawaua, nisipomrudisha Benyamini kwako. Mtie mkononi mwangu! Mimi nitamrudisha kwako.
38
Lakini akasema: Huyu mwanangu hatatelemka pamoja nanyi, kwani kaka yake amekufa, naye amesalia peke yake; atakapopatwa na kibaya cho chote njiani katika hiyo safari mtakayokwenda mtanisukuma mimi mwenye mvi kushuka kuzimuni na kusikitika.
← Chapter 41
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 43 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50