bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Genesis 50
Genesis 50
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 49
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
1
Yosefu akamwangukia baba yake usoni, akamlilia na kumnonea.
2
Kisha Yosefu akawaagiza watumishi wake waganga, wampake baba yake manukato; ndipo, hao waganga walipompaka Isiraeli manukato,
3
mpaka siku 40 zikitimia, kwani kuzitimiza hizo siku ndio desturi ya kupaka manukato. Nao Wamisri akamwombolezea siku 70.
4
Siku za maombolezo zilipokwisha pita, Yosefu akawaambia wao wa nyumbani mwake Farao kwamba: Kama nimeona upendeleo machoni penu, semeni masikioni pake Farao ya kwamba:
5
Baba yangu ameniapisha kwamba: Tazama! Mimi ninakufa; sharti unizike katika kaburi langu, nililojichimbia katika nchi ya kanaani. Sasa ninataka kupanda kwenda huko, nimzike baba yangu, kisha nirudi.
6
Naye Farao akasema: Panda kwenda huko, umzike baba yako, kama alivyokuapisha.
7
Yosefu alipopanda kwenda huko kumzika baba yake, wakaenda naye watumwa wazee wote wa nyumbani mwake Farao nao wazee wote wa nchi ya Misri,
8
nao wote wa mlango wa Yosefu nao ndugu zake nao wote wa mlango wa baba yake; watoto wao tu na mbuzi na kondoo na ng'ombe wao waliwaacha katika nchi ya Goseni.
9
Nayo magari na wapanda farasi wakapanda naye, wakawa kikosi kikubwa sana.
10
Walipofika pake Atadi pa kupuria ngano palipo ng'ambo ya huko ya Yordani wakafanya maombolezo makuu yenye vilio kabisa. Ndivyo, Yosefu alivyolala matanga siku saba kwa ajili ya baba yake.
11
Wenyeji wa nchi ya Kanaani walipoyaona hayo matanga pake Atadi pa kupuria ngano wakasema: Matanga haya ya Wamisri ni makuu kweli, kwa sababu hii wakapaita jina lake mahali pale palipo ng'ambo ya huko ya Yordani: Tanga la Misri.
12
Kisha wanawe wakayafanya yayo hayo, aliyowaagiza:
13
wao wanawe wakamchkua na kumpeleka katika nchi ya Kanaani, kisha wakamzika katika lile pango katika shamba la Makipela, ndilo shamba lile, Aburahamu alilolinunua kwa Mhiti Efuroni kuwa mahali pake pa kuzikia, napo palikuwa panaelekea Mamure.
14
Yosefu alipokwisha kumzika baba yake akarudi Misri, yeye na ndugu zake nao wote waliopanda naye kwenda kumzika baba yake.
15
Lakini kaka zake Yosefu wakaogopa, kwa kuwa baba yao amekufa, wakasema mioyoni: Labda Yosefu atatuchukia, atulipize mabaya, tuliyomfanyizia.
16
Kwa hiyo wakatuma kwake Yosefu kumwambia kwamba: Baba yako alipokuwa hajafa bado alituagiza kwamba:
17
Hivi ndivyo, mtakavyomwambia Yosefu: E ndugu, yaondoe mapotovu na makosa yao ndugu zako! Kwani walikufanyizia mabaya. Sasa waondolee watumishi wa Mungu wa baba yako hayo mapotovu! Yosefu akalia machozi, walipomwambia maneno haya.
18
Kisha kaka zake wenyewe wakaenda, wakamwangukia na kumwambia: Sisi hapa tu watumwa wako.
19
Lakini Yosefu akawaambia: Msiogope! Je? Mimi ninapashika mahali pake Mungu?
20
Kweli ninyi mwaliwaza kunifanyizia mabaya, lakini Mungu aliyageuza kuwa mema, ayafanye yaliyo waziwazi leo, aponye watu wengi.
21
Kwa hiyo msiogope sasa! Mimi nitawatunza ninyi na watoto wenu. Hivyo akawatuliza mioyo akisema nao kwa upole.
22
Yosefu akakaa Misri, yeye pamoja nao walio wa mlango wa baba yake; nayo miaka yake Yosefu ya kuwapo ilikuwa 110.
23
Yosefu akaona wana wa Efuraimu hata kizazi cha tatu, nao wana wa Makiri, mwana wa Manase, wakazaliwa magotini pake Yosefu.
24
Kisha Yosefu akawaambia ndugu zake: Mimi ninakufa, lakini ninyi Mungu atawapatia njia ya kuwatoa katika nchi hii na kuwapandisha kwenda katika hiyo nchi, aliyowaapia akina Aburahamu na Isaka na Yakobo kuwapa.
25
Kisha Yosefu akawaapisha wana wa Isiraeli kwamba: Hapo, Mungu atakapowakagua ninyi, sharti mwichukue mifupa yangu kwenda nayo!
26
Kisha Yosefu akafa mwenye miaka 110, wakampaka manukato, wakamweka ndani ya sanduku huko Misri.
← Chapter 49
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50