bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Genesis 32
Genesis 32
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 31
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 33 →
1
Yakobo alipokwenda safari yake akakutana na malaika wa Mungu.
2
Yakobo alipowaona akasema: Hapa ndipo kambi la Mungu, akapaita mahali pale Mahanaimu (Makambi Mawili).
3
Yakobo akatuma wajumbe kwenda katika nchi ya Seiri kwenye bara ya Edomu, wamtangulie kufika kwake mkubwa wake Esau.
4
Akawaagiza kwamba: Hivi ndivyo, mmwambie bwana wangu Esau: Hivi ndivyo, mtumishi wako Yakobo anavyosema: Nimekaa ugenini kwake Labani, nikakawilia huko mpaka sasa,
5
nikapata ng'ombe na punda, mbuzi na kondoo, watumwa wa kiume na wa kike, nikatuma kumpasha bwana wangu habari hizi, nijipatie upendeleo machoni pako.
6
Hao wajumbe waliporudi kwake Yakobo akamwambia: Tumefika kwa mkubwa wako Esau, naye anakuja na watu 400, mkutane njiani.
7
Ndipo, Yakobo alipoogopa sana na kusongeka moyoni, akawagawanya watu, aliokuwa nao, hata mbuzi na kondoo, nao ng'ombe na ngamia kuwa vikosi viwili,
8
akasema: Esau atakapojia kikosi kimoja na kukishinda, hicho kingine kitakachosalia kitapata kupona.
9
Kisha Yakobo akaomba: Mungu wa baba yangu Aburahamu na Mungu wa baba yangu Isaka, wewe Bwana umeniambia: Rudi katika nchi yako kwenye ndugu zako! Mimi nitakufanyizia mema.
10
Hivyo, nilivyo mdogo, sipaswi na magawio yote wala na welekevu wote, uliomfanyizia mtumishi wako. Kwani hapo, nilipouvuka mto huu wa Yordani niliishika hii fimbo yangu tu, lakini sasa ni mwenye vikosi viwili.
11
Niponye mkononi mwa mkubwa wangu Esau! Kwani namwogopa, asije, akanipiga mimi na wamama pamoja na wana.
12
Wewe nawe umesema: Nitakufanyizia mema kweli, nao wa uzao wako nitawafanya kuwa wengi kama mchanga wa ufukoni usiohesabika kwa wingi.
13
Kisha akalala huko usiku huo, akatoa katika yale mapato yaliyokuwa mkononi mwake matunzo ya kumpa kaka yake Esau:
14
mbuzi majike 200 na madume 20, kondoo majike 200 na madume 20,
15
ngamia wanyonyeshao 30 pamoja na wana wao, ng'ombe majike 40 na madume 10, punda majike 20 na wana wa punda 10;
16
akawatia mikononi mwa watumwa wake, kundi kwa kundi peke yake, akawaambia hawa watumwa wake: Nitangulieni, tena katikati ya kila makundi mawili acheni nafasi.
17
Naye wa kwanza akamwagiza kwamba: Mkubwa wangu Esau atakapokutana na wewe na kukuuliza kwamba: Wewe mtu wa nani? Unakwenda wapi? Nao hao nyama, wanaowatanguliza, ni wa nani?
18
Umwambie: Ni wa mtumishi wako Yakobo, ndio matunzo, anayomtumia bwana wangu Esau, naye mwenyewe anatufuata nyuma.
19
Naye wa pili na wa tatu nao wote waliowafuata watumwa hawa akawaagiza kwamba: Mtakapomwona Esau mwambieni maneno yayo hayo!
20
Kisha semeni nanyi: Naye mtumishi wako Yakobo anatufuata nyuma. Kwani alisema moyoni mwake: Nitaupoza uso wake kwa hayo matunzo yatakayonitangulia; nitakapoonana naye halafu, labda atanipokea vema.
21
Kwa hiyo matunzo yakamtangulia, naye akalala usiku huo humo kambini.
22
Usiku huo alipoamka akawachukua wakeze wawili na wale vijakazi wawili na wanawe kumi na mmoja, akaenda kuvuka kivukoni kwa Yakobo;
23
akawachukua, akawavusha hapo mtoni, akayavusha nayo yote, aliyokuwaa nayo.
24
Naye Yakobo mwenyewe akasalia peke yake ng'ambo ya huko. Mara mtu akakamatana naye, mpaka jua lilipopambazuka.
25
Alipoona, ya kuwa hamshindi Yakobo, akamgusa nyonga ya kiuno chake; ndipo, nyonga ya kiuno cha Yakobo ilipoteuka kwa kukamatana naye.
26
Akamwambia Yakobo: Niache, niende zangu! Kwani jua limepambazuka. Lakini akasema: Sitakuacha, usiponibariki.
27
Naye akamwuliza: Jina lako nani? Akasema: Yakobo.
28
Ndipo, aliposema: Hutaitwa tena jina lako Yakobo, ila Isiraeli (Mshinda Mungu), kwani umeshindana na Mungu, hata na watu, ukawashinda.
29
Naye Yakobo akamwuliza kwamba: Niambie jina lako! Akamwambia: Jina langu unaliulizia nini? Kisha akambariki hapo.
30
Yakobo akapaita mahali pale Penieli (Uso wa Mungu) kwamba: Nimeonana na Mungu uso kwa uso, nayo roho yangu ikapona.
31
Alipovuka hapo Penieli, usiku ukamchea, naye alikuwa akichechemea kwa ajili ya kiuno chake.
32
Kwa sababu hii wana wa Isiraeli hawali mshipa ulio juu ya nyonga ya kiuno mpaka siku hii ya leo, kwani yule aliigusa nyonga ya kiuno cha Yakobo penye mshipa wa kiuno.
← Chapter 31
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 33 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50