bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Genesis 18
Genesis 18
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 17
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 19 →
1
Kisha Bwana akamtokea katika kimwitu cha Mamure, mwenyewe alipokuwa amekaa hapo pa kuingia hemani kwa kuwa jua kali.
2
Alipoyainua macho yake akaona watu watatu, wakisimama hapo, alipo; alipowaona akawapigia mbio na kuondoka hapo pa kuingia hemani, akawainamia chini,
3
akawaambia: Bwana wangu, kama nimeona mapendeleo machoni pako, usipite penye mtumishi wako!
4
Mtaletewa maji kidogo ya kuiosha miguu yenu, kisha mtapumzika chini ya mti huu.
5
Nami nitaleta chakula kidogo, mioyo yenu ipate kutulia, kisha mtakwenda zenu, kwani huku, mnakopita, ni kwake mtuma wenu. Nao wakamwambia: Fanya, kama ulivyosema!
6
Aburahamu akaingia upesi hemani kwa Sara, akamwambia: Chukua upesi pishi sita za unga mwembamba uliochungwa vema, uukande, utengeneze mikate!
7
Kisha Aburahamu akapiga mbio kwenda kwenye ng'ombe, akachukua ndama mwanana mwenye nyama nzuri, akampa kijana, naye akaenda kuitengeneza vizuri.
8
Kisha Aburahamu akawaandalia siagi na maziwa na nyama za ndama, yule alizozitengeneza, nao wakala, mwenyewe akisimama karibu yao chini ya mti.
9
Kisha wakamwuliza: Mkeo Sara yuko wapi? Akajibu: Yumo hemani.
10
Akamwambia: Nitakaporudi kwako siku zizi hizi za mwaka ujao, ndipo, mkeo Sara atakapokuwa mwenye mtoto wa kiume. Naye Sara aliyasikia, maana alikuwa nyuma yake hapo pa kuingia hemani.
11
Lakini Aburahamu na Sara walikuwa wazee wenye siku nyingi, naye Sara alikuwa amekoma kupatwa na yale mambo ya kike.
12
Kwa hiyo Sara akacheka moyoni mwake kwamba: Hivyo, nguvu za mwili wangu zilivyokwisha kupotea, nitawezaje kuipata hiyo furaha? Tena bwana wangu naye ni mzee.
13
Ndipo, Bwana alipomwambia Aburahamu: Mbona Sara anacheka kwamba: Kumbe mimi nitazaa kweli, nami ni mzee?
14
Je? Liko jambo linalomshinda Bwana? Wakati, nitakaporudi kwako, siku zizi hizi za mwaka ujao ndipo, Sara atakapokuwa mwenye mtoto wa kiume.
15
Lakini Sara akakana kwamba: Sikucheka, kwani aliogopa; naye akasema: Sivyo, umecheka.
16
Kisha wale waume wakaondoka huko, wakajielekeza kwenda Sodomu, naye Aburahamu akaenda nao, awasindikize.
17
Bwana akasema: Nitamfichaje Aburahamu ninayotaka kuyafanya?
18
Maana Aburahamu atakuwa taifa kubwa lenye nguvu, namo mwake ndimo, mataifa yote ya nchini yatakamobarikiwa.
19
Kwani ninamjua, ya kuwa atawaagiza wanawe nao wa mlango wake wajao nyuma yake, waishike njia ya Bwana na kufanya yaongokayo nayo ya kweli, Bwana apate kumtimizia Aburahamu aliyomwagia.
20
Kwa hiyo Bwana akasema: Makelele ya Sodomu na ya Gomora ni mengi, nayo makosa yao ni mazito mno.
21
Nimeshuka, nitazame, kama hayo yote, ambayo niliyasikia makelele yao, wameyafanya kweli, au kama hawakuyafanya, nijue.
22
Kisha wale watu wakageuka hapo kwenda Sodomu, lakini aburahamu akasalia hapo akisimama mbele ya Bwana.
23
Aburahamu akafika karibu, akauliza: Utamwondoa mwongofu pamoja naye asiyekucha?
24
Labda mle mjini wamo waongofu 50; basi, utawaondoa nao? Hutapahurumia mahali hapo kwa ajili ya waongofu 50 waliopo?
25
Jambo kama hilo halipasi kabisa, ulifanye, ukimwua mwongofu pamoja naye asiyekucha, mwongofu akiwa kwako kama mwingine asiyekucha. Hili halikupasi kabisa wewe utakayewaamua walimwengu wote, hayo si maamuzi, utakayoyaamua.
26
Bwana akasema: Kama nitawaona waongofu 50 mle mjini mwa Sodomu, nitapahurumia mahali pale pote kwa ajili yao.
27
Aburahamu akajibu kwamba: Tazama nimejipa moyo wa kusema na Bwana, ingawa mimi ni mavumbi na majivu.
28
Labda wale waongofu 50 wamepunguka watano, sasa utaungamiza mji wote kwa ajili ya hao watano? Akasema: Sitauangamiza, kama nitaona humo 45.
29
Akaendelea kusema naye kwamba: Labda wataonekana humo 40 tu. Akasema: Sitafanya kitu kwa ajili yao hao 40.
30
Akasema: Makali ya Bwana yasiwake moto, nikisema tena: Labda wataonekana humo 30 tu. Akasema: Sitafanya kitu, kama nitaona humo 30 tu.
31
Akasema: Tazama, nimejipa moyo wa kusema na Bwana: Labda wataonekana humo 20 tu. Akasema: Sitauangamiza kwa ajili yao hao 20.
32
Akasema: Makali ya Bwana yasiwake moto, nikisema tena mara moja tu: Labda wataonekana humo 10 tu. Akasema: Sitauangamiza kwa ajili yao hao 10 tu.
33
Bwana alipokwisha kusema na Aburahamu akaenda zake, naye Aburahamu akarudi mahali pake.
← Chapter 17
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 19 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50