bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Genesis 45
Genesis 45
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 44
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 46 →
1
Yosefu asipoweza kuvumilia tena kwa ajili yao wote waliosimama kwake, ndipo alipoita kwamba: Watoeni wote humu mwangu! Kwa hiyo hakusimama mtu mwake, Yosefu alipojitambulisha kwa ndugu zake.
2
Lakini alipopaza sauti kwa kulia, Wamisri wakavisikia, nao wa nyumbani mwa Farao wakavisikia.
3
Kisha Yosefu akawaambia ndugu zake: Ni mimi Yosefu! Baba yangu yuko mzima bado? Lakini ndugu zake hawakuweza kumjibu, kwani walimstukia.
4
Ndipo, Yosefu alipowaambia ndugu zake: Nifikieni karibu! Nao walipokwisha kumkaribia, akawaambia: Ni mimi ndugu yenu Yosefu, mliyemwuza kupelekwa Misri.
5
Lakini sasa msisikitike, wala msijikasirikie, ya kuwa mliniuza kupelekwa huku! Kwani Mungu ndiye aliyenituma kwenda mbele yenu, nipate kuwaponya.
6
Kwani huu ni mwaka wa pili wa kuingia njaa katika nchi hii, ingaliko miaka mitano isiyo na kulima wala kuvuna.
7
Kwa hiyo Mungu alinituma kwenda mbele yenu, niwapatie ninyi masao katika nchi hii na wokovu mkubwa wa kuwaponya ninyi.
8
Sasa sio ninyi mlionituma kuja huku, ila ni Mungu mwenyewe. Naye akaniweka kuwa baba yake Farao na bwana wa nyumba yake yote na mtawala nchi zote za Misri.
9
Pigeni mbio, mpande kwenda kwa baba yangu, mmwambie: Hivi ndivyo, anavyosema mwanao Yosefu: Mungu ameniweka kuwa bwana wa nchi yote nzima ya Misri; telemka kuja kwangu, usikawilie!
10
Na ukae katika nchi ya Goseni, upate kuwa karibu yangu, wewe na wanao na wana wa wanao na mbuzi na kondoo wako na ng'ombe wako navyo vyote, ulivyo navyo.
11
Nitakutunza huku, kwani ingaliko bado miaka mitano ya njaa; zisiangamizwe mali zako wewe nazo zao walio wa mlango wako, nazo zao wote, ulio nao.
12
Macho yenu ninyi yanaona, nayo macho ya ndugu yangu Benyamini yanaona, ya kuwa ni kinywa changu mimi kinachosema nanyi.
13
Msimulieni baba yangu, utukufu wangu wote ulivyo huku Misri, nayo yote, mliyoyaona! Pigeni mbio, mmtelemshe baba yangu kuja huku!
14
Kisha akamkumbatia nduguye Benyamini, akali machozi; Benyamini naye akalia machozi shingoni pake.
15
Nao kaka zake wote akanoneana nao pamoja na kulia machozi; kisha kaka zake wakaongea naye.
16
Uvumi uliposikilika nyumbani mwa Farao kwamba: Ndugu zake Yosefu wamefika! akapendezwa Farao nao watumishi wake.
17
Naye Farao akamwambia Yosefu: Waaambie ndugu zako: Fanyeni hivi: wachukuzeni nyama wenu mizigo, mpate kwenda zenu! Mtakapofika katika nchi ya Kanaani,
18
mchukueni baba yenu nao wa milango yenu, mje kwangu! Nitwapa kipande cha nchi ya Misri kilicho kizuri, mle manono ya nchi hii!
19
Wewe umekwisha kuagizwa, uwaambie: Fanyeni hivi: jichukulieni huku katika nchi ya Misri magari ya kuwachukulia watoto wenu na wake zenu! Naye baba yenu mchukueni, mje naye!
20
Msijiumize kwa ajili ya vyombo vyenu! Kwani mema yote ya nchi nzima ya Misri ni yenu!
21
Nao wana wa Isiraeli wakafanya hivyo, maana Yosefu akawapa magari kwa ile amri ya Farao, akawapa nazo pamba za njiani.
22
Nao wote akawapa nguo za zikukuu, kila mmoja yake; lakini Benyamini akampa fedha 300 na nguo tano za sikukuu.
23
Naye baba yake akampelekea vitu hivi: punda kumi waliochukua vitu vizuri vya Misri na majike ya punda kumi waliochukua ngano na chakula kingine na pamba za njiani za baba yake.
24
Alipoagana na ndugu zake, waende zao, akawaambia: Msigombane njiani!
25
Ndivyo, walivyotoka Misri, wapande kwenda katika nchi ya Kanaani kwa baba yao Yakobo.
26
Wakamsimulia kwamba: Yosefu yuko mzima bado, naye ndiye anayeitawala nchi yote nzima ya Misri; lakini moyo wake ukapigwa bumbuazi, hakuyategemea maneno yao.
27
Wakamwambia maneno yote, Yosefu aliyowaambia; naye alipoyaona hayo magari, Yosefu aliyoyatuma kumchukua, ndipo, roho yake ilipomrudia baba yao Yakobo.
28
Kisha Isiraeli akasema: Lililo kuu ni hili: mwanangu Yosefu angaliko mzima. Nitakwenda, nimwone, kabla sijafa.
← Chapter 44
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 46 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50