bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Genesis 40
Genesis 40
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 39
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 41 →
1
Ikawa, mambo hayo yalipomalizika, mkuu wa watunza vinywaji vya mfalme wa Misri na mkuu wa wachoma mikate wakamkosea bwana wao, mfalme wa Misri.
2
Naye Farao akawakasirikia hawa watumishi wake wawili wa nyumbani mwake, Yule mkuu wa watunza vinywaji naye mkuu wa wachoma mikate.
3
Akawafunga, waangaliwe kifungoni katika nyumba ya mkuu wao waliomlinda mfalme; ndimo, Yosefu alimokuwa naye kwa kufungwa.
4
Naye mkuu wao waliomlinda mfalme akamweka Yosefu kuwaangalia na kuwatumikia, wakawamo hizo siku wakiangaliwa.
5
Usiku mmoja wote wawili wakaota ndoto, kila mtu ndoto yake yenye maana yake, yule mtunza vinywaji vya mfalme naye yule mchoma mikate ya mfalme wa Misri waliokuwa wamefungwa kifungoni.
6
Yosefu alipoingia asubuhi chumbani mwao, awatazame, akawaona, ya kuwa wamenuna,
7
akawauliza hawa wafungwa wa Farao walioangaliwa naye katika nyumba ya bwana wake kwamba: Mbona leo nyuso zenu ni mbaya?
8
Wakamwambia: Tumeota ndoto, lakini mwenye kuzifumbua hakuna. Yosefu akawaambia: Kumbe kufumbua siko kwake Mungu? Lakini nisumulieni!
9
Mkuu wao watunza vinywaji akamsimulia ndoto yake, akamwambia: Katika ndoto yangu nimeona machoni pangu mzabibu;
10
katika mzabibu huu yalikuwamo matawi matatu, nao ulipochipuka, ukachanua maua yake, navyo vichala vyake vikaivisha zabibu.
11
Nacho kikombe cha Farao kilikuwa mkononi mwangu, nikazishika zile zabibu, nikazikamulia katika kikombe cha Farao, kisha nikampa Farao, hicho kikombe mkononi mwake.
12
Yosefu akamwambia: Maana yake ndio hii: hayo matawi matatu ndio siku tatu;
13
siku tatu zitakapopita, Farao atakupa kukiinua kichwa chako, kwani atakurudisha katika kazi yako, umpe kikombe chake Farao mkononi mwake, kama ilivyokupasa kale, ulipokuwa mtunza vinywaji vyake.
14
Lakini utakapopata mema sharti unikumbe na kunihurumia ukiniombea kwake Farao, anitoe humu nyumbani.
15
Kwani nimekwibwa katika nchi ya Waebureo, huku nako sikukosa lo lote, wakanitia humu kifungoni.
16
Mkuu wa wachoma mikate alipoona, ya kuwa amefumbua vema, akamwambia Yosefu: Mimi nami katika ndoto yangu nimejiona, nilipokuwa nimechukua nyungo tatu zenye vikate vyeupe kichwani pangu.
17
Namo katika ungo wa juu vilikuwamo vikate vizuri vyo vyote vya Farao, wachoma mikate wanavyovitengeneza, nao ndege wakavila mwenye ungo kichwani pangu.
18
Yosefu akajibu akisema: Maana yake ndio hii: hizo nyungo tatu ndio siku tatu;
19
siku tatu zitakapopita, Farao atakupa kukiinua kichwa chako, kiwe juu yako zaidi, atakunyonga katika mti, nao ndege watazila nyama za mwili wako.
20
Siku ya tatu ikawa siku ya kuzaliwa kwake Farao; ndipo, alipowaandalia watumishi wake wote karamu; hapo katikati ya watumishi wake akampa mkuu wa watunza vinywaji naye mkuu wa wachoma mikate kuviinua vichwa vyao,
21
akimrudisha mkuu wa watunza vinywaji katika kazi yake ya kutunza vinywaji, ampe Farao kikombe mkononi mwake,
22
naye mkuu wa wachoma mikate akamnyonga, kama Yosefu alivyowafumbulia ndoto.
23
Lakini mkuu wa watunza vinywaji hakumkumbuka Yosefu, akamsahau.
← Chapter 39
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 41 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50