bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Genesis 14
Genesis 14
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 13
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 15 →
1
Ikawa siku zile za Amurafeli, mfalme wa Sinari, ndipo, yeye na Arioki, mfalme wa Elasari, na Kedori-Laomeri, falme wa Elamu, na Tidali, mfalme wa Goyimu,
2
wakaenda kupiga vita na Bera, mfalme wa Sodomu, na Birsa, mfalme wa Gomora na Sinabu, mfalme wa Adima, na Semeberi, mfalme wa Seboimu, na mfalme wa Bela unaoitwa Soari.
3
Hawa wote wakajiunga, wakakutana bondeni kwa Sidimu kwenye Bahari ya Chumvi.
4
Kwani wale walimtumikia Kedori-Laomeri miaka kumi na miwili, lakini katika mwaka wa kumi na tatu walimvunjia maagano.
5
Kwa hiyo Kedori-Laomeri na wafalme waliokuwa naye wakaja katika mwaka wa kumi na nne, wakawapiga wale Majitu kule Astaroti-Karnaimu nao Wazuzi kule Hamu nao Waemi katika nchi ya tambarare ya Kiriataimu,
6
nao Wahori milimani kwao Seiri mpaka Eli-Parani ulioko upande wa nyikani.
7
Kisha wakarudi, wakafika kwenye chemchemi ya Misipati, ndio Kadesi, wakaipiga nchi yote ya Waamaleki nao Waamori waliokaa Hasasoni-Tamari.
8
Ndipo, walipotoka, mfalme wa Sodomu na mfalme wa Gomora na mfalme wa Adima na mfalme wa Seboimu na mfalme wa Bela, ndio Soari, wakajipanga katika bonde la Sidimu kupigana.
9
Nao wa Kedori-Laomeri, mfalme wa Elamu, na Tidali, mfalme wa Goyimu, na Amurafeli, mfalme wa Sinari, na Arioki, mfalme wa Elasari, walikuwa wafalme wanne, nao wale ni watano.
10
Nako kule bondeni kwa Sidimu kulikuwa na mashimo mengi ya lami, nao wafalme wa Sodomu na wa Gomora walipokimbizwa wakatumbukia mlemle, nao watu waliosalia wakakimbilia milimani.
11
Ndipo, walipoyateka mapato yote ya Sodomu na ya Gomora, navyo vilaji vyao vyote, wakaenda zao.
12
Naye Loti, mwana wa nduguye Aburamu, wakamteka na mapato yake, wakenda zao, kwani alikaa Sodomu.
13
Mtu mmoja aliyejiponya akaja, akamsimulia Mwebureo Aburamu yaliyokuwa; naye alikuwa akikaa katika kimwitu cha Mwamori Mamure aliyekuwa ndugu yao Eskoli na Aneri, nao hao walikuwa wamefanya maagano na Aburamu.
14
Aburamu aliposikia, ya kuwa ndugu yake ametekwa, akawachukua wazalia wa nyumbani mwake 318 waliozijua kazi za vita, akapiga mbio akiwafuata mpaka Dani.
15
Usiku akawagawanya watu wake, akawashambulia, akawapiga; kisha akawakimbiza mpaka Hoba ulioko kushotoni kwa Damasko.
16
Akayarudisha yale mapato yote, naye ndugu yake Loti akamrudisha pamoja na mapato yake, nao wanawake wa watu waliotekwa.
17
Aliporudi kwa kumpiga Kedori-Laomeri na wale wafalme waliokuwa naye, mfalme wa Sodomu akatoka kumwendea njiani kule bondeni kwa Sawe, ndio bondeni kwa Mfalme.
18
Naye Melkisedeki, mfalme wa Salemu, akamotolea mkate na mvinyo, naye alikuwa mtambikaji wa Mungu alioko huko juu.
19
Akambariki na kusema: Aburamu na atukuzwe kwa kuwa wake Mungu, mwenye mbingu naa nchi!
20
Atukuzwe naye Mungu alioko huko juu, kwa kuwa amewatia adui zako mkononi mwako! Ndipo Aburamu alipompa fungu la kumi la mali zote, alizokuwa nazo.
21
Kisha mfalme wa sodomu akamwambia Aburamu: Nipe watu wangu tu, mali uzitwae wewe.
22
Lakini Aburamu akamwambia mfalme wa Sodomu: Mkono wangu namnyoshea Bwana Mungu alioko huko juu, aliye mwenye mbingu na nchi, kwamba:
23
Katika mali zote zilizo zako sitachukua uzi wala kikanda tu cha kiatu, usiseme: Aburamu mali zake nyingi nimempa mimi.
24
Hawa vijana tu wape chakula chao! Nao waume hawa waliokwenda pamoja nami, Aneri na Eskoli na Mamure, wao na wayachukue mafungu yao!
← Chapter 13
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 15 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50