bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Genesis 19
Genesis 19
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 18
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 20 →
1
Ilipokuwa jioni, wale malaika wawili wakafika Sodomu, naye Loti alikuwa amekaa langoni huko Sodomu. Alipowaona Loti akainuka kuwaendea njiani, akawaangukia usoni chini,
2
akawaambia: Mabwana, njoni kufikia nyumbani mwa mtumwa wenu, mlale, mwioshe miguu yenu! Kesho mtaondoka na mapema kwenda zenu; lakini wakakataa wakisema: Tutalala nje.
3
Ndipo, alipowahimiza sana, mpaka wakifikia kwake; walipoingia nyumbani mwake, akawatengenezea cha kunywa, akachoma mikate isiyochachwa, nao wakala.
4
Walipokuwa hawajalala bado, watu wa ule mji wa Sodomu, vijana kwa wazee, watu wote waliotoka pande zote wakaja, wakaizunguka hiyo nyumba,
5
wakamwita Loti, wakamwuliza: Wako wapi wale waume waliokuja kwako usiku huu? Walete, watutokee, tupate kuwajua!
6
Loti akawatokea hapo pa kuingilia na kuufunga mlango nyuma yake,
7
akasema: Ndugu zangu, msifanye mabaya!
8
Tazameni! Ninao wanangu wa kike wawili wasiojua bado mtu mume, nitawatoa, niwape ninyi, mwafanyizie yaliyo mema machoni penu; lakini waume hao msiwafanyizie neno, kwani kwa sababu hii wmeingia kivulini mwa kipaa changu.
9
Wakasema: Ondoka hapa! Tena wakaambiana: Ni mgeni peke yake kwetu, tena anataka kutuamua. Wakamsonga sana huyu Loti wakitaka kuukaribia mlango, wauvunje.
10
Ndipo, wale watu walipoitoa mikono yao, wakamwingiza Loti kwao nyumbani, kisha wakaufunga mlango.
11
Lakini wale watu waliokuwa nje hapo pa kuingia nyumbani wakawapofusha macho, wadogo kwa wakubwa, wakashindwa kupaona hapo pa kuingia nyumbani.
12
Kisha wale waume wakamwambia Loti: Kama unao ndugu, wakweo na wanao wa kiume na wa kike nao wo wote walio wako humu mjini, wachukue, utoke nao mahali hapa!
13
Kwani sisi tutapaangamiza mahali hapa; kwani makelele yao ni makubwa masikioni mwake Bwana, kwa hiyo Bwana ametutuma, tupaangamize.
14
Loti alipotoka kusema na wakwewe waliowaoa wanawe wa kike, akawaambia: Inukeni, mtoke mahali hapa! Kwani Bwana ataungamiza mji huu. Lakini machoni pao wakwewe alikuwa kama mtu anayetaka kuwachekesha tu.
15
Kulipopambazuka, wale malaika wakamhimiza Loti kwamba: Ondoka! Mchukue mkeo nao wanao wawili wa kike, ulio nao, usiuawe nawe kwa ajili ya manza za mji huu!
16
Alipozuzuika, wale waume wakawashika mikono, yeye na mkewe na wanawe, kwa huruma, Bwana alizowapatia, wakawatoa mjini na kuwapeleka nje.
17
Walipokwisha kuwatoa na kuwapeleka nje, akasema: Iponye roho yako! Usitazame nyuma, wala usisimame huku bondeni mahali pawapo pote, ila kimbilia milimani, usiuawe!
18
Loti akawaambia: Usiseme hivyo, Bwana wangu!
19
Kwa kuwa mtumwa wako aliona upendeleo machoni pako, ukazizidisha huruma zako, ulizonifanyia, uiponye roho yangu! Tazama, sitaweza kukimbilia milimani kwa kwamba: Yale mabaya yatanipata, nami nitakufa.
20
Tazama, huko karibu uko mji wa kuukimbilia, nao ni mdogo; acha, niukimbilie huo, kwa kuwa mdogo, niiponye roho yangu!
21
Naye akamwambia: Basi, hata katika neno hili nitakuitikia, nisiufudikize nao mji huo, uliousema.
22
Jihimize kuukimbilia! Kwani siwezi kufanya lo lote, mpaka ufike humo. Kwa hiyo wakaliita jina la mji huo Soari (Mdogo).
23
Loti alipoingia Soari, jua lilikuwa linachomoza.
24
Ndipo, Bwana aliponyesha mvua ya moto uliochanganyika na mawe ya kiberitiberiti kwenye miji ya Sodomu na Gomora; mvua hii ilitoka kwake Bwana mbinguni.
25
Ndivyo, Mungu alivyoifudikiza hiyo miji nalo hilo bonde lote pamoja na watu waliokaa humo mijini nayo majani yote yaliyochipuka katika nchi ile.
26
Naye mkewe Loti alipoyatazama ya nyuma akawa nguzo ya chumvi.
27
Kesho yake Aburahamu akaamka na mapema kwenda pale, aliposimama mbele ya Bwana.
28
Akachungulia upande wa Sodomu na Gomora na upande wa nchi zote za bonde hilo, mara akaona, moshi ulivyopanda kutoka chini kama moshi wa tanuru.
29
Lakini hapo, Mungu alipoiangamiza miji ya lile bonde, Mungu alimkumbuka Aburahamu, amtoe Loti katika mafudikizo hayo na kumpeleka pengine alipoifudikiza hiyo miji, Loti alimokuwa na kukaa humo.
30
Kisha Loti akatoka Soari, akapanda milimani kukaa huko pamoja na wanawe wawili wa kike, kwani aliogopa kukaa mle Soari; kwa hiyo akakaa pangoni yeye pamoja na wanawe wawili.
31
Kisha yule wa kwanza akamwambia mdogo wake: Baba yetu ni mzee, tena hakuna mtu mume katika nchi hii yote wa kuingia kwetu, kama ilivyo desturi po pote duniani.
32
Haya! Na tumlevye baba yetu kwa mvinyo, kisha tulale naye, tupate kwa baba yetu mimba za kuukalisha mlango!
33
Basi, wakamlevya baba yao usiku huo, kisha yule mkubwa akaingia kwa baba yake, akalala naye, lakini mwenyewe hakujua, alipokuja kulala naye, wala alipoondoka.
34
Kesho yake yule mkubwa akamwambia mdogo wake: Tazama, usiku wa jana nimelala na baba yangu; haya! Na tumlevye kwa mvinyo hata siku ya leo, upate kuingia kwake na kulala naye, tupate kwa baba yetu mimba za kuukalisha mlango!
35
Kisha wakamlevya baba yao kwa mvinyo nao usiku huo, naye mdogo akaingia, akalala naye, lakini mwenyewe hakujua, alipokuja kulala naye, wala alipoondoka.
36
Hivyo ndivyo, wana wa kike wa Loti wote wawili walivyopata mimba kwa baba yao.
37
Yule mkubwa alipozaa mtoto mume akamwita jina lake Moabu (Wa baba), naye ni baba yao Wamoabu mpaka leo.
38
Yule mdogo alipozaa mtoto mume akamwita jina lake Ben-Ami (Mwana wa Kwetu), naye ni baba yao wana wa Amoni mpaka leo.
← Chapter 18
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 20 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50