bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Genesis 39
Genesis 39
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 38
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 40 →
1
Yosefu alipopelekwa Misri, Potifari aliyekuwa mtumishi wa nyumbani mwa Farao na mkuu wao waliomlinda Farao akamnunua mikononi mwao wale Waisimaeli waliompeleka huko.
2
Bwana akawa naye Yosefu, kwa hiyo akafanikiwa alipokuwa nyumbani mwa bwana wake wa Kimisri.
3
Bwana wake alipoona, ya kuwa Bwana yuko pamoja naye, nayo yote, anayoyafanya, Bwana anayafanikisha mikononi mwake,
4
Yosefu akaona upendeleo machoni pake, akampa kumtumikia mwenyewe, kisha akamweka kuisimamia nyumba yake yote, nayo yote, aliyokuwa nayo, akayatia mkononi mwake.
5
Tangu hapo, alipomweka nyumbani mwake kuyasimamia yote, aliyokuwa nayo, Bwana akaibariki nyumba ya huyu Mmisri kwa ajili yake Yosefu; mbaraka ya Bwana ikayakalia yote yaliyokuwa yake nyumbani na shambani.
6
Kwa hiyo akamwachia Yosefu yote, aliyokuwa nayo, yawe mkononi mwake, naye mwenyewe hakujua chake cho chote, isipokuwa chakula chake, alichokila. Naye Yosefu alikuwa mzuri wa umbo na wa uso.
7
Siku zilipopita, mkewe bwana wake akamtupia Yosefu macho, akamwambia: Lala kwangu!
8
Lakini akakataa, akamwambia mkewe bwana wake: Tazama! Bwana wangu hajui cho chote kilichomo humu nyumbani, ninachokiangalia, nayo yote, aliyo nayo, ameyatia mkononi mwangu.
9
Humu nyumbani hamna mkubwa kuliko mimi, wala hamna kitu, alichonikataza, ni wewe peke yako, kwa kuwa wewe ndiwe mkewe. Kwa hiyo nitawezaje kufanya kibaya kilicho kikuu kama hiki nikimkosea Mungu?
10
Hivi ndivyo, alivyomwambia Yosefu siku kwa siku, lakini Yosefu hakumwitikia kulala naye wala kuwa pamoja naye.
11
Ikawa siku moja, alipoingia kufanya kazi zake chumbani, msimokuwa na mtu hata mmoja wao wakazi wa humo chumbani,
12
ndipo, alipomkamata nguo yake na kusema: Lala kwangu! Lakini akaiacha nguo yake mkononi mwake, akakimbia na kutoka nje.
13
Ikawa, alipoona, ya kuwa ameiacha nguo yake mkononi mwake na kukimbia kwenda nje,
14
akawaita waliomo nyumbani, akawaambia kwamba: Tazameni! Ametuletea huyu Mwebureo wa kucheza na sisi! Ameingia mwangu kulala na mimi, lakini nikapiga kelele kubwa.
15
Naye aliposikia, ya kama nimezipaza sauti zangu za kuita watu, akaiacha nguo yake kwangu, akakimbia kwenda nje.
16
Akaiweka nguo yake kwake, hata bwana wake arudi nyumbani mwake.
17
Ndipo, alipomwambia maneno yayo hayo ya kwamba: Yule mtumwa Mwebureo, uliyemleta kwetu kucheza na sisi, ameingia mwangu.
18
Lakini nilipozipaza sauti zangu za kuita watu, akaiacha nguo yake kwangu, akakimbia kwenda nje.
19
Ikawa, bwana wake alipoyasikia haya maneno ya mkewe, aliyomwambia ya kwamba: Mtumwa wako amenifanyia haya na haya, akakasirika na kuwaka moto.
20
Ndipo, bwana wake Yosefu alipomchukua, akamfunga kifungoni mle chumbani, mlimokuwa na wafungwa wa mfalme; humo kifungoni ndimo, Yosefu alimotiwa.
21
Lakini Bwana alikuwa naye Yosefu, akamtolea utu na kumpatia upendeleo machoni pa mkuu wa kifungo.
22
Huyu mkuu wa kifungo akatia mkononi mwa Yosefu wafungwa wote waliokuwamo mle kifungoni, yote waliyoyafanya humo yawe kazi yake yeye.
23
Katika yote, mkuu a kifungo aliyoyatia mkononi mwake, hakikuwamo cho chote, alichokitazama mwenyewe, kwa kuwa Bwana alikuwa na Yosefu, nayo yote aliyoyafanya Bwana akayafanikisha.
← Chapter 38
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 40 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50