bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Genesis 46
Genesis 46
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 45
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 47 →
1
Isiraeli akaondoka pamoja nayo yote, aliyokuwa nayo, akaja Beri-Seba; ndiko, alikomchinjia Mungu wa baba yake Isaka ng'ombe za tambiko.
2
Naye Mungu akamtokea Isiraeli usiku, akamwita kwamba: Yakobo! Yakobo! Akaitikia: Mimi hapa!
3
Naye akamwambia: Mimi ni Mungu, Mungu wa baba yako; usiogope kutelemka Misri! Kwani ndiko, nitakakokupa kuwa taifa kubwa.
4
Mimi nitatelemka pamoja na wewe kwenda Misri, nami nitakupandisha tena kuja huku, naye Yosefu atayafumba macho yako kwa mkono wake.
5
Yakobo alipoondoka Beri-Seba, wana wa Isiraeli wakampandisha baba yao Yakobo garini nao watoto wao na wake zao, ndiyo yale magari, Farao aliyoyatuma kumchukua.
6
Wakayachukua nayo makundi yao na mapato yao, waliyoyapata katika nchi ya Kanaani, wakafika Misri, yeye Yakobo nao wa uzao wake wote pamoja naye.
7
Wanawe na wajukuu wake nao wanawe wa kike na wajukuu wake wa kike nao wa uzao wake wote aliwapeleka Misri kwenda naye.
8
Haya ndiyo majina ya wana wa Isiraeli waliokwenda Misri. Yakobo na wanawe: Mwana wa kwanza wa Yakobo ni Rubeni.
9
Nao wana wa Rubeni ni Henoki na Palu na Hesironi na Karmi.
10
Nao wana wa Simeoni ni Yemueli na Yamini na Ohadi na Yakini na sohari na Sauli, mwana wa mwanamke wa Kanaani.
11
Nao wana wa Lawi ni Gersoni na Kehati na Merari.
12
Nao wana wa Yuda ni Eri na Onani na Sela na Peresi na Zera; lakini Eri na Onani walikuwa wamekufa katika nchi ya Kanaani. Nao wana wa peresi walikuwa Hesironi na Hamuli.
13
Nao wana wa Isakari ni Tola na Puwa na Yobu na Simuroni.
14
Nao wana wa Zebuluni ni Seredi na Eloni na Yaleli.
15
Hawa ndio wana wa Lea, aliomzalia Yakobo huko Mesopotamia, naye mwanawe wa kike ni Dina. Wanawe wote pamoja, wa kiume na wa kike, ni watu 33.
16
Nao wana wa Gadi ni Sifioni na Hagi na suni na Esiboni, tena Eri na Arodi na Areli.
17
Nao wana wa Aseri ni Imuna na Isiwa na Iswi na Beria na umbu lao Sera; nao wana wa Beria ni Heberi na Malkieli.
18
Hawa ndio wana wa Zilpa, Labani aliyempa mwanawe Lea; naye alimzalia Yakobo hawa watu 16.
19
Wana wa Raheli, mkewe Yakobo, ni Yosefu na Benyamini
20
Naye Yosefu katika nchi ya Misri alizaliwa Manase na Efuraimu; ndio, aliomzalia Asenati, binti Potifera, mtambikaji wa Oni.
21
Nao wana wa Benyamini ni Bela na Bekeri na Asibeli, Gera na Namani, Ehi na Rosi, Mupimu na Hupimu na Ardi.
22
Hawa ndio wana wa Raheli, Yakobo aliozaliwa; wote pamoja ni watu 14.
23
Nao wana wa Dani ni Husimu.
24
Nao wana wa Nafutali ni Yaseli na Guni na Yeseri na Silemu.
25
Hawa ndio wana wa Biliha, Labani aliyempa mwanawe Raheli; naye alimzalia Yakobo hawa watu 7.
26
Watu wote waliokwenda Misri na Yakobo ni 66; ndio waliotoka kiunoni mwake, tena wake zao wana wa Yakobo.
27
Nao wana wa Yosefu aliozaliwa huko Misri, ni watu wawili; hivyo watu wote pia wa mlango wa Yakobo waliokuja Misri walikuwa 70.
28
Yakobo akamtuma Yuda kwenda mbele yake kwa Yosefu, amwonyeshe nchi ya Goseni, kisha wakaiingia hiyo nchi ya Goseni.
29
Ndipo, Yosefu alipolitandika gari lake, akamwendea baba yake Isiraeli huko Goseni. Alipomwonekea, akamkumbatia shingoni akalia machozi hapo shingoni pake kitambo kizima.
30
Kisha Isiraeli akamwambia Yosefu: Sasa na nife, kwani nimekwisha kuuona uso wako, ya kuwa u mzima bado.
31
Kisha Yosefu akawaambia ndugu zake nao wa mlango wa baba yake: Nitapanda kumpasha Farao habari ya kwamba: Ndugu zangu nao wa mlango wa baba yangu waliokaa katika nchi ya Kanaani wamefika kwangu.
32
Nao watu hawa ni wachungaji, kwani ni wenye makundi, nao mbuzi na kondoo wao na ng'ombe wao nayo yote, waliyokuwa nayo, wameyaleta huku.
33
Naye Farao atakapowaita na kuwauliza: Kazi yenu nini?
34
na mmwambie: Watumwa wako ni wachungaji tangu ujana wetu mpaka sasa; nasi tulivyo, ndivyo, nao baba zetu walivyokuwa, kusudi mpate kukaa katika nchi ya Goseni; kwani Wamisri huwachukiza wachungaji wote.
← Chapter 45
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 47 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50