bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Genesis 3
Genesis 3
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 4 →
1
Nyoka alikuwa mjanja kuliko nyama wote wa porini, Bwana Mungu aliowafanya. Naye akamwambia mwanamke: Kumbe Mungu amewakataza kuila miti yote iliyomo humu shambani?
2
Lakini mwanamke akamwambia nyoka: Tunayala matunda ya miti iliyomo humu shambani;
3
lakini matunda ya mti huu katikati ya shamba Mungu ametuambia: Msiyale! Msiyaguse, msipate kufa!
4
Ndipo, nyoka alipomwambia mwanamke: kufa hamtakufa kabisa.
5
Kwani Mungu anajua, ya kuwa siku, mtakapoula, macho yenu yatafumbuliwa, mwe kama Mungu mkijua mema na mabaya.
6
Mwanamke alipoutazama huo mti akauona kuwa mwema wa kula, hata wa kuyapendeza macho, tena akauona, ya kuwa unapasa kutamaniwa kwa kuerevusha; ndipo, alipochuma tunda mojamoja, akala, akampa hata mumewe, naye akala.
7
Ndipo, macho yao wote wawili yalipofumbuliwa, wakatambua, ya kuwa wako uchi; kwa hiyo wakashona majani ya mkuyu, wakayatumia ya kujifunga viunoni.
8
Jua lilipokuwa limeponga, wakakisikia kishindo cha Bwana Mungu, akitembea shambani; ndipo, Adamu na mkewe walipojificha kwenye miti ya shamba, Bwana Mungu asiwaone.
9
Bwanaa Mungu akamwita Adamu akisema: Uko wapi?
10
Akajibu: Nimekisikia kishindo chako shambani, nikaogopa, kwa kuwa mimi ni mwenye uchi, nikajificha.
11
Akasema: Ni nani aliyekuambia, ya kuwa wewe u mwenye uchi? Hukuula ule mti, niliokukataza, usiule?
12
Naye Adamu akasema: Huyu mwanamke, uliyonipa kuwa nami, yeye amenipa tunda la mti ule, nikalila.
13
Bwana Mungu akamwuliza mwanamke; Mbona umeyafanya hayo? Mwanamke akamwambia: Nyoka amenidanganya, nikala.
14
Ndipo, Bwana Mungu alipomwambia nyoka: Kwa kuwa umeyafanya hayo, utakuwa umeapizwa wewe kuliko nyama wote wa nyumbani na wa porini, utajiburura kwa tumbo lako, ule mavumbi siku zako zote za kuwapo.
15
Na niwachochee, mchukizane, wewe na huyu mwanamke, uzao wako na uzao wake, huyo atakuponda kichwa, nawe utamwuma kisigino.
16
Kisha akamwambia mwanamke: Nitakupatia maumivu mengi, utakapopata mimba, itakuwa kwa machngu mengi, ukizaa watoto; ijapo yawe hivyo, utamtamani mumeo, naye atakutawala.
17
Adamu naye akamwambia: Kwa kuwa umeiitikia sauti ya mkeo, ukaula ule mti, niliokuagiza kwamba: Usiule! nchi imeapizwa kwa ajili yako, uile na kuona uchungu siku zako zote za kuwapo.
18
Itakuoteshea miiba na mibigili, nawe utakula majani ya shambani.
19
Kwa jasho la uso wako utakula chakula, mpaka utakaporudi mchangani, kwani ndimo, ulimochukuliwa, kwani ndiwe mavumbi wewe, nayo mavumbi ndiyo, utakayokuwa tena.
20
Adamu akamwita mkewe jina lake Ewa, kwa kuwa ndiye mama yao wote walio hai.
21
Bwana Mungu akamtengenezea Adamu na mkewe ngozi za kuvaa, akawavika.
22
Kisha Bwana Mungu akasema: Ninamwona Adamu, ya kuwa amekwisha kuwa kama mwenzetu kwa kujua mema na mabaya; labda sasa ataupeleka mkono wake, achume nayo matunda ya mti wa uzima na kuyala, apate kuwapo kale na kale.
23
Kwa hiyo Bwana Mungu akamtoa katika hilo shamba la Edeni, ailime nchi, alimochukuliwa.
24
Ndiyo sababu, aliyomfukuzia Adamu, nao upande wa maawioni kwa jua wa shamba la Edeni akaweka Makerubi wenye panga zimulikazo moto pande zote, wailinde njia iendayo kwenye mti wa uzima.
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 4 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50