bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Genesis 28
Genesis 28
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 27
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 29 →
1
Isaka akamwita Yakobo, akambariki, akamwagiza kwamba: Usioe mwanamke katika vijana wa kike wa Kanaani!
2
Inuka, uende Mesopotamia nyumbani mwa Betueli, babake mama yako, umchukue mkeo huko katika wana wa kike wa Labani, umbu lake mama yako.
3
Naye Mwenyezi Mungu akubariki, akupe kuzaa wana wengi sana, upate kuwa mkutano wa makabila ya watu!
4
Akupe nayo mbaraka ya Aburahamu, wewe nao wa uzao wako wajao, upate kuichukua nchi hii ya ugeni wako, Mungu aliyompa Aburahamu.
5
Ndivyo, Isaka alivyomtuma Yakobo kwenda Mesopotamia kwa Mshami Labani, mwana wa Betueli, kaka yake Rebeka aliyekuwa mama yao Yakobo na Esau.
6
Esau akaona, ya kuwa Isaka amembariki Yakobo na kumtuma kwenda Mesopotamia, achukue mke huko, tena ya kuwa hapo alipombariki amemwagiza kwamba: Usijichukulie mke katika vijana wa kike wa Kanaani!
7
Tena akaona, ya kuwa Yakobo amemsikia baba yake na mama yake alipokwenda Mesopotamia.
8
Tena Esau akaona, ya kama vijana wa kike wa Kanaani walikuwa wabaya machoni pa baba yake, Isaka.
9
Ndipo, Esau alipokwenda kwa Isimaeli, akamchukua Mahalati, binti Isimaeli, mwana wa Aburahamu, umbu lake Nebayoti, kuwa mkewe pamoja na wakeze, aliokuwa nao.
10
Yakobo akaondoka Beri-Seba, akaenda Harani.
11
Njiani alipofika mahali palipomfaa akalala hapo usiku, kwani jua lilikuwa limekuchwa. Akachukua jiwe la hapo, akaliweka chini ya kichwa chake, akalala mahali pale.
12
Akaota, akaona ngazi, ilikuwa imesimikwa nchini, lakini ncha yake iligusa mbinguni; alipotazama akona, malaika wa Mungu wakipanda, tena wakishuka hapo.
13
Naye Bwana akamwona, akisimama juu, akasema: Mimi ni Bwana, Mungu wa baba yako Aburahamu na Mungu wa Isaka. Nchi hii, unayoilalia, nitakupa wewe nao wa uzao wako.
14
Nao wa uzao wako watakuwa wengi kama mavumbi ya nchi hii, nawe utaenea upande wa baharini na upande wa maawioni kwa jua na upande wa kaskazini na upande wa kusini; namo mwako na katika uzao wako ndimo, koo zote za nchini zitakamobarikiwa.
15
Tazama! Niko pamoja na wewe, nikulinde po pote, utakapokwenda; nitakurudisha katika nchi hii, kwani sitakuacha, mpaka niyafanyize, niliyokuambia wewe.
16
Yakobo alipoamka katika usingizi akasema: Kweli Bwana yuko mahali hapa, nami nilikuwa sikuyajua.
17
Kwa hiyo akaogopa, akasema: Kumbe mahali hapa panaogopesha, hapa sipo pengine, ndipo Nyumba ya Mungu ilipo, ndipo lango la mbingu lilipo.
18
Asubuhi na mapema Yakobo akaamka, akalichukua lile jiwe, aliloliweka chini ya kichwa chake, akalisimika kuwa kielekezo, akalimiminia mafuta juu yake,
19
akapaita mahali pale jina lake Beteli (Nyumba ya Mungu), lakini kwanza ule mji uliitwa Luzi.
20
Kisha Yakobo akaapa kiapo kwamba: Mungu akiwa pamoja na mimi na kunilinda katika safari hii, ninayokwenda, akinipa vilaji vya kula na nguo za kuvaa,
21
nipate kurudi na kutengemana nyumbani mwa baba yangu, Bwana atakuwa Mungu wangu,
22
hata jiwe hili, nililolisimika kuwa kielekezo, litakuwa Nyumba ya Mungu, nayo yote, utakayonipa, nitakutolea fungu la kumi.
← Chapter 27
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 29 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50