bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Genesis 17
Genesis 17
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 16
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 18 →
1
Aburamu alipokuwa mwenye miaka 99, Bwana akamtokea Aburamu, akamwambia: Mimi ni Mungu Mwenyezi, uendelee machoni pangu na kunicha!
2
Hivyo tutaagana sote wawili, mimi na wewe, nami nitakufanya kuwa watu wengi sanasana.
3
Ndipo, Aburamu alipomwangukia usoni pake, naye Mungu akaendelea kusema naye kwamba:
4
Tazama! Nina agano na wewe, uwe baba yao mataifa mazima ya watu.
5
Kwa hiyo usiitwe tena jina lako Aburamu (Baba mtukufu), ila jina lako liwe Aburahamu (Baba yao wengi)! Kwani nimekuweka kuwa baba yao mataifa mengi ya watu.
6
Nitakupa wazao wengi sanasana, nikufanye kuwa mataifa, nao wafalme watatoka kwako.
7
Nitalisimamisha agano langu, tuliloliagana mimi na wewe nao wa uzao wako wajao nyuma yako, liwe agano la vizazi vya kale na kale, niwe Mungu wako na Mungu wao wa uzao wako wajao nyuma yako.
8
Nitakupa wewe nao wa uzao wako wajao nyuma yako nchi hii, unayoikaa ugeni, ndiyo nchi yote ya Kanaani, mwichukue, iwe yenu kale na kale, nami nitakuwa Mungu wao.
9
Kisha Mungu akamwambia Aburahamu: Liangalieni Agano langu, wewe nao wa uzao wako wajao nyuma yako, vizazi kwa vizazi!
10
Nalo hili ndilo Agano langu la kuliangalia, tunaloliagana mimi na wewe nao wa uzao wako wajao nyuma yako: Kwenu sharti atahiriwe kila aliye wa kiume.
11
Mkizikata nyama za magovi yenu, hii itakuwa kielekezo cha Agano, tuliloliagana mimi nanyi.
12
Kwenu kila mtoto wa kiume aliye wa vizazi vyenu akimaliza siku nane sharti atahiriwe. Vivyo hivyo nao wazalia wa nyumbani nao wasio wa uzao wako walionunuliwa kwa fedha kwa wageni wo wote.
13
Hao wazaliwa nyumbani mwako nao walionunuliwa kwa fedha zako sharti nao watahiriwe. Hili Agano langu la kuzikata hizo nyama za miili yenu sharti liwe la kale na kale.
14
Kwa hiyo mtu mume mwenye govi asiyekatwa nyama ya govi lake sharti roho yake yeye ing'olewe, atoweke kwao walio wa ukoo wake, maana ni mwenye kulivunja Agano langu.
15
Kisha Mungu akamwambia Aburahamu: Mkeo Sarai asiitwe tena jina lake Sarai, ila jina lake liwe Sara (Mama mkuu)!
16
Kwani nitambariki, nikupatie kwake mtoto mume; nitakapombariki, atakuwa mama wa mataifa mazima, nao wafalme wa makabila ya watu watatoka kwake.
17
Ndipo, Aburahamu alipomwangukia usoni pake, akacheka na kusema moyoni mwake: Itawezekanaje, mwenye miaka mia azaliwe mtoto? Huyu Sara aliye mwenye miaka 90 atazaaje?
18
Kwa hiyo Aburahamu akamwambia Mungu: Afadhali Isimaeli angepata kuwapo machoni pako!
19
Ndipo, Mungu aliposema: Ni kweli, mkeo Sara atakuzalia mtoto mume, nalo jina lake uliite Isaka (Acheka); naye ndiye, nitakayemsimamishia Agano langu kuwa la kale na kale kwao wa uzao wake wajao nyuma yake.
20
Hata kwa ajili ya Isimaeli nimekusikia: Tazama, nitambariki naye na kumpa wazao wengi na kumfanya kuwa wengi sanasana, atazaa wakuu 12, nami nitamfanya kuwa taifa kubwa.
21
Lakini lile Agano langu nitamsimamishia Isaka, Sara atakayekuzalia siku zizi hizi za mwaka ujao.
22
Mungu alipokwisha kusema naye, akapaa juu na kutoka kwake Aburahamu.
23
Kisha Aburahamu akamchukua mwanawe Isimaeli nao wazaliwa wote wa nyumbani mwake nao wote, aliowanunua kwa fedha zake, watu waume wote pia waliokuwamo nyumbani mwake Aburahamu, akawakata nyama za magovi yao siku iyo hiyo, kama Mungu alivyomwambia.
24
Aburahamu alikuwa mwenye miaka 99 alipokatwa nyama ya govi lake.
25
Naye mwanawe Isimaeli alikuwa mwenye miaka 13 alipokatwa nyama ya govi lake.
26
Siku iyo hiyo moja Aburahamu na mwanawe isimaeli walitahiriwa.
27
Nao waume wote wa nyumbani mwake, wazalia wa nyumbani nao, aliowanunua kwa fedha kwa watu wasio wa kabila lake, wote walitahiriwa pamoja naye.
← Chapter 16
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 18 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50