bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Genesis 38
Genesis 38
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 37
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 39 →
1
Ikawa wakati huo, ndipo, Yuda alipoondoka kwa ndugu zake, akajiunga na mtu wa Adulamu, jina lake Hira.
2
Huko Yuda akaona binti Mkanaani, jina lake sua, akamchukua, akaingia kwake.
3
Naye akapata mimba, akazaa mtoto mume; jina lake yule akamwita Eri.
4
Alipopata mimba tena akazaa mtoto mume, akamwita jina lake Onani.
5
Akendelea, akazaa tena mtoto mume, akamwita jina lake Sela. Naye Yuda alikuwa huko Kizibu, alipomzaa.
6
Yuda akamwoza mwanawe wa kwanza Eri, jina lake mkewe ni Tamari.
7
Lakini Eri, mwana wa kwanza wa Yuda, akawa mbaya machoni pa Bwana, kwa hiyo Bwana akamwua.
8
Ndipo, Yuda alipomwambia Onani: Ingia kwa mkewe kaka yako, umsimikie unyumba naye na kumpatia kaka yako mzao kwake!
9
Kwa kuwa Onani alijua, ya kama huyo mzao hatakuwa wake yeye, basi, kila mara alipoingia kwa mkewe kaka yake kwanza akaziangusha mbegu zake chini, asimpatie kaka yake uzao.
10
Hayo, aliyoyafanya, yakawa mabaya machoni pa Bwana, kwa hiyo akamwua naye.
11
Ndipo, Yuda alipomwambia mkwewe Tamari: Kaa tu na ujane wako nyumbani mwa baba yako, hata mwanangu Sela akue! Kwani alisema moyoni, asife huyu naye kama kaka zake. Kwa hiyo Tamari akaenda, akakaa nyumbani mwa baba yake.
12
Siku zilipopita nyingi, binti Sua, mkewe Yuda, akafa. Yuda alipokwisha kujituliza moyo kwa ajili ya kufa kwake akapanda kwenda Timunati kwao waliowakata kondoo wake manyoya, yeye na rafiki yake Hira wa Adulamu.
13
Tamari alipopashwa habari kwamba: Tazama, mkweo anapanda kwenda Timunati kuwakata kondoo wake manyoya,
14
akayavua mavazi yake ya ujane, akajifunika kwa ukaya na kujitandia nguo, kisha akakaa hapo pa kuingilia Enaimu kwenye njia ya timunati, kwani aliona, ya kuwa Sela amekwisha kukua, lakini yeye hakuozwa naye, awe mkewe.
15
Yuda alipomwona akamwazia kuwa mwanamke mgoni, kwani alijifunika ushungi,
16
akamgeukia na kumwendea hapo njiani, alipokaa, akamwambia: Acha, niingie kwako! kwani hakumjua kuwa mkwewe. Akamwuliza: Utanipa nini ukiingia kwangu?
17
Akasema: Mimi nitakuletea dume la mbuzi, nitakayemtoa mle makundini; naye akamwambia: Nipe rehani, niishike, mpaka utakapomleta!
18
Akamwuliza: Nikupe rehani gani? Akamwambia: Pete yako yenye muhuri na mshipi wako na fimbo yako, unayoishika mkononi. Akampa, kisha akaingia kwake, naye akapata mimba.
19
Alipoinuka kwenda zake, akaondoa ukaya wake usoni pake, akayavaa mavazi yake ya ujane.
20
Yuda alipotuma dume la mbuzi mkononi mwa rafiki yake wa Adulamu, achukue nazo zile rehani mkononi mwa yule mwanamke, hakumwona.
21
Naye alipowauliza watu wa mahali hapo kwamba: Yuko wapi yule mwanamke mgoni wa patakatifu aliyekaa njiani hapo Enaimu? Wakamwambia: Huku hakuwako mwanamke mgoni wa patakatifu.
22
Akarudi kwake Yuda, akamwambia: sikumwona, nao watu wa mahali pale wanasema: Huku hakuwako mwanamke mgoni wa patakatifu.
23
Ndipo, Yuda aliposema: Na ajitwalie, tusije kutwezwa! Tazama, nimempeleka huyu dume la mbuzi, nawe hukumwona!
24
Miezi mitatu ilipopita, Yuda akapashwa habari kwamba: Mkweo Tamari amefanya ugoni, naye akapata mimba kwa huo ugoni. Ndipo, Yuda aliposema: Mtoeni, ateketezwe!
25
Alipotolewwa akatuma kwa mkwewe kwamba: Mimi nimepata mimba kwake yeye aliye mwenye vitu hivi; akaendelea kusema: Mtambue mwenye pete hii yenye muhuri na mwenye mshipi huu na mwenye fimbo hii!
26
Yuda alipovitambua vitu hivyo akasema: Yeye ni mwongofu kuliko mimi; ameyafanya, kwa kuwa sikumpa mwanangu Sela. Lakini hakumjua tena hata mara moja.
27
Siku zake za kuzaa zilipotimia, wakaona ya kuwa tumboni mwake wamo wana wa pacha.
28
Ikawa, alipozaa, mmoja akatoa mkono; ndipo mzalishaji alipomfunga mkononi pake uzi mwekundu kwamba: Huyu ametoka wa kwanza.
29
Lakini ikawa, alipourudisha mkono wake, mara ndugu yake akatoka; ndipo, aliposema: Kumbe umejipasulia ufa namna hii! Kwa hiyo wakamwita jina lake Peresi (Ufa).
30
Kisha ndugu yake akatoka naye mwenye uzi mwekundu mkononi pake, kwa hiyo wakamwita jina lake Zera (Mwekundu).
← Chapter 37
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 39 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50