bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Genesis 49
Genesis 49
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 48
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 50 →
1
Kisha Yakobo akawaita wanawe, akawaambia: Kusanyikeni, niwaeleze, yatakayowapata siku za sasa zitakapokwisha!
2
Kusanyikeni, wana wa Yakobo, msikilize! Msikilizeni baba yenu Isiraeli!
3
Wewe Rubeni, u mwana wa kwanza, u nguvu yangu na uwezo wangu wa kwanza, ukuu wako hutukuzwa, ukuu wako ni wa nguvu.
4
Lakini kwa kububujika kama maji hutapata ukuu wa kweli, kwani ulipokipanda kitanda cha baba yako, ndipo, ulipoyachafua malalo yangu kwa kuyapandia.
5
Simeoni na Lawi ni ndugu kweli, panga zao ni vyombo vya ukorofi.
6
Roho yangu isiingie penye njama yao, wala moyo wangu usifanye bia na mikutano yao! Kwani kwa makali yao waliua watu, kwa majivuno yao wakakata madume ya ng'ombe mishipa.
7
Na yaapizwe makali yao kwa kuwa yenye nguvu! Na yaapizwe machafuko yao kwa kuwa yenye upingani! Na niwagawanye kwao Wayakobo, na niwatawanye kwao Waisiraeli!
8
Wewe Yuda, ndugu zako watakusifu; mkono wako utawakamata wachukivu wako penye kosi, nao wana wa baba yako watakuangukia.
9
Yuda ni mwana simba. Mwanangu, ulipokwisha kukamata, hupanda kupumzika na kulala kama simba au kama mamake simba; yuko nani atakayekuamsha?
10
Bakora ya kifalme haitaondoka kwake Yuda, wala fimbo la mwenye amri halitaondoka miguuni pake, mpaka atakapokuja mwenye kutuliza, ambaye makabila ya watu watamtii.
11
Kipunda chake hukifunga mizabibuni, naye mwana punda humlisha miche ya mizabibu mizuri, huyafua mavazi yake katika mvinyo, nazo nguo zake katika damu za zabibu.
12
Macho yake huwa mekundu kwa kunywa mvinyo, nayo meno yake huwa meupe kwa kunywa maziwa.
13
Zebuluni atakaa pwani, Bahari Kubwa iliko, huko pwani, merikebu zinakofikia, apakane nao Wasidoni.
14
Isakari ni punda mwenye mifupa migumu, hupenda kulala, katikati ya mazizi ya kondoo.
15
Atakapoona matuo kuwa mema, atakapoiona nayo nchi hii kuwa ya kumpendeza, ndipo, atakapouinamisha mgongo wake kuchukua mizigo, awe mtumishi wa kufanya kazi za nguvu.
16
Dani atawaamua walio watu wake akiwa kama wenzake walio mashina ya Isiraeli.
17
Dani atakuwa nyoka njiani, atakuwa piri penye mikondo, awaume farasi visigino, waliowapanda waanguke nyuma.
18
Ninaungojea wokovu wako, Bwana!
19
Gadi atashambuliwa na vikosi vya vita, lakini naye atawashambulia na kuwanyatia.
20
Kwake Aseri ndiko, vyakula vya manono vitakakotoka, naye ndiye atakayewapatia wafalme vyakula vya urembo.
21
Nafutali ni kulungu aliyefunguliwa kukimbia, huimba nyimbo zilizo nzuri zaidi.
22
Yosefu ni tawi la mti wa matunda, tawi la mti wa matunda ulioko kwenye mboji, kwa hiyo matawi yake hutambaa na kuufunika ukuta.
23
Ijapo wapiga mishale wamchokoze kwa kumgombeza
24
na kumchukia, upindi wake hushupaa vivyo hivyo, nazo nguvu za mikono yake ziko tayari vivyo hivyo, yumo mikoni mwake amtawalaye Yakobo, hushikwa na mchungaji aliye mwamba wa Isiraeli.
25
Mungu wa baba yako ndiye atakayekusaidia Mwenyezi Mungu ndiye atakayekubariki kwa mbaraka zitokazo mbinguni juu na kwa mbaraka zitokazo vilindini ndani ya nchi na kwa mbaraka zitokazo maziwani na tumboni.
26
Mbaraka za baba yako zina nguvu kuzishinda mbaraka zao walionizaa, zitakupendeza kuliko matunu ya vilima vya kale na kale. Hizo ndizo zitakazokijia kichwa chake Yosefu, nao utosi wake yeye aliyewekwa kwa kutengwa na ndugu zake.
27
Benyamini ni mbwa wa mwitu mwenye uchu wa damu, asubuhi hula mawindo, jioni hugawanya mateka.
28
Haya ndiyo mashina yote kumi na mawili ya Isiraeli, nayo haya ndiyo yote, baba yao aliyowaambia alipowabariki, naye aliwabariki na kumpa kila mmoja mbaraka yake yeye.
29
Kisha akawaagiza na kuwaambia: Mimi sasa nitakapochukuliwa kwenda kwao walio ukoo wangu, sharti mnizike kwa baba zangu katika lile pango, lililoko shambani kwake Mhiti Efuroni!
30
Ndilo pango lile lililoko shambani kwa Makipela kuelekea Mamure; shamba hilo Aburahamu alilinunua kwa Mhiti Efuroni kuwa mahali pake yeye pa kuzikia.
31
Mle pangoni ndimo, walimomzika Aburahamu na mkewe Sara, naye Isaka na mkewe Rebeka waliwazika humo, naye Lea nilimzika humo.
32
Ndilo lile shamba lililonunuliwa kwa wana wa Hiti pamoja na lile pango lililoko.
33
Yakobo alipokwisha kuwaagiza wanawe maneno haya akaikunja miguu yake kitandani, akazimia, akachukuliwa kwenda kwao walio wa ukoo wake.
← Chapter 48
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 50 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50