bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Genesis 22
Genesis 22
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 21
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 23 →
1
Ikawa, mambo hayo yalipomalizika, Mungu akamjaribu Aburahamu, akamwambia: Aburahamu! naye akajibu: Mimi hapa!
2
Akamwambia: Mchukue mwana wako wa pekee, umpendaye, huyo Isaka, uende naye katika nchi ya Moria, umtoe huko kuwa ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima juu ya mlima mmoja, nitakaokuonyesha!
3
Basi, kesho yake Aburahamu akaamka na mapema, akamtandika punda wake, akachukua na vijana wawili kwenda naye, tena mwanawe Isaka; alipokwisha kuchanja nazo kuni za kuchomea ng'ombe ya tambiko, akaondoka kwenda mahali pale, Mungu alipomwambia.
4
Aburahamu alipoyainua macho yake siku ya tatu akapaona mahali pale, pangaliko mbali.
5
Ndipo, Aburahamu alipowaambia wale vijana wake: Kaeni hapa pamoja na punda! Mimi na huyu kijana tutakwenda huko kutambika, kisha tutarudi kwenu.
6
Aburahamu akazichukua zile kuni za kuchomea ng'ombe ya tambiko, akamtwika mwanawe Isaka, naye mwenyewe akashika moto na kisu mkononi mwake, wakaenda hivyo wao wawili pamoja.
7
Isaka akamwmbia baba yake Aburahamu: Baba! Akajibu: Mimi hapa, mwanangu! Akasema: Tazama! Moto na kuni tunazo, lakini mwana kondoo wa kuwa ng'ombe ya tambiko yuko wapi?
8
Aburahamu akasema: Mwanangu, Mungu atajipatia mwana kondoo wa kuwa ng'ombe ya tambiko. Kisha wakaenda hivyo wao wawili pamoja.
9
Walipofika mahali pale, Mungu alipomwambia, Aburahamu akajenga hapo pa kutambikia, akazitandika kuni juu yake; kisha akamfunga mwanawe Isaka, akamweka hapo pa kutambikia juu ya hizo kuni;
10
kisha Aburahamu akaukunjua mkono wake, akakishika kisu cha kumchinjia mwanawe.
11
Ndipo, malaika wa Bwana alipomwita toka mbinguni kwamba: Aburahamu! Aburahamu! Akaitikia: Mimi hapa!
12
Akamwambia: Usimkunjulie mtoto mkono wako! Usimfanyizie cho chote! Kwani sasa nimejua, ya kuwa unamwogopa Mungu, maana hukumnyima hata mwanao wa pekee.
13
Aburahamu alipoyainua macho yake akaona kulungu nyuma yake aliyekamatwa pembe zake na kichaka; huyo kulungu akamtumia kuwa ng'ombe ya tambiko mahali pake mwanawe.
14
Aburahamu akapaita mahali hapo: Bwana aona; kwa hiyo watu husema hata leo: Mlimani, Bwana anakoonwa.
15
Malaika wa Bwana akamwita Aburahamu toka mbinguni mara ya pili,
16
akasema: Ndivyo, asemavyo Bwana: Nimejiapia kwamba: Kwa kuwa umelifanya jambo hili, usininyime mwanao wa pekee,
17
nitakubariki kweli, nikupe, uzao wako uwe watu wengi sana kama nyota za mbinguni au kama mchanga ulioko ufukoni kwenye bahari, hao wa uzao wako wayatwae malango ya adui zao kuwa yao.
18
Katika uzao wako ndimo, mataifa yote ya nchini yatakamobarikiwa, kwa kuwa umeisikia sauti yangu.
19
Kisha Aburahamu akarudi kwa wale vijana wake, wakaondoka, wakaenda zao pamoja kwenda Beri-Seba; kule Beri-Seba ndiko, Aburahamu alikokaa.
20
Mambo hayo yalipomalizika, Aburahamu akapashwa habari kwamba: Tazama, naye Milka amemzalia ndugu yako Nahori wana.
21
Mwanawe wa kwanza ni Usi, ndugu yake ni Buzi, tena Kemueli, baba yao Washami,
22
na Kesedi na Hazo na Pildasi na Idilafu na Betueli.
23
Naye Betueli akamzaa Rebeka. Milka alimzalia ndugu yake Aburahamu hao wanane,
24
naye suria yake aliyeitwa Ruma akamzaa Teba, tena Gahamu na Tahasi na Maka.
← Chapter 21
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 23 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50