bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Genesis 2
Genesis 2
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 3 →
1
Ndivyo, zilivyomalizika kuumbwa mbingu na nchi na vikosi vyao vyote.
2
Siku ya saba Mungu alipozimaliza kazi zake zote, alizozifanya, akazipumzikia siku ya saba hizo kazi zake zote, alizozifanya;
3
kwa hiyo Mungu akaibariki siku ya saba na kuitakasa, kwa kuwa siku hiyo Mungu alizipumzikia kazi zake zote, alizozifanya za kuumba.
4
Hivyo ndivyo, mbingu na nchi zilivyopata kuwapo hapo, zilipoumbwa. Siku hizo, Bwana Mungu alipozifanya nchi na mbingu,
5
miti yote ya mashambani ilikuwa haijawa bado, nazo mboga zote za mashambani zilikuwa hazijaota bado, kwa kuwa Bwana Mungu alikuwa hajanyesha bado mvua katika nchi, tena hakuwako mtu wa kulima shamba.
6
Lakini kungugu lilipopanda toka nchini likanywesha upande wa nje wa nchi yote.
7
Naye Bwana Mungu alipomwumba mtu alimtengeneza na kutumia mavumbi ya nchi, kisha akampulizia puani mwake pumzi ya uzima; ndipo, mtu alipopata kuwa mwenye roho ya uzima.
8
Kisha Bwana Mungu akapanda shamba huko Edeni upande wa maawioni kwa jua; ndiko, alikomweka huyo mtu, aliyemwumba.
9
Bwana Mungu akaichipuza nchi miti yote ipendezayo kwa kutazamwa nayo ifaayo kwa kuliwa, napo hapo katikati ya shamba mti wa uzima na mti wa kujulia mema na mabaya.
10
Tena kule Edeni kulitoka jito la kulinywesha hilo shamba, likajigawanya papo hapo shambani kuwa makono manne.
11
Jina lake mto wa kwanza ni Pisoni, uliizunguka nchi yote ya Hawila iliyokuwa na dhahabu.
12
Nayo dhahabu ya nchi hii ilikuwa nzuri; tena kulikuwako magwede na vito vya oniki.
13
Jina lake mto wa pili ni Gihoni, nao ndio ulioizunguka nchi yote ya Kusi.
14
Jina lake mto wa tatu ni Hidekeli, nao ndio unaopita upande wa maawioni kwa jua wa nchi ya Asuri. Nao mto wa nne ndio Furati.
15
Bwana Mungu akamchukua Adamu, akamkalisha katika shamba la Edeni, alilime na kuliangalia.
16
Kisha Bwana Mungu akamwagiza Adamu kwamba: Miti yote iliyomo humu shambani utaila,
17
lakini mti wa kujulia mema na mabaya usiule! Kwani siku, utakapoula, huna budi kufa.
18
Bwana Mungu akasema: Hiafai, mtu akiwa peke yake, nitamfanyizia mwenziwe wa kusaidiana naye.
19
Bwana Mungu alipokwisha kuwatokeza katika nchi nyama wote wa porini na ndege wote wa angani akawapeleka kwa Adamu, aone, atakavyowaita; jina lake kila nyama mwenye uzima liwe lilo hilo, Adamu atakalomwita.
20
Adamu akampa kila nyama wa nyumbani na kila ndege wa angani na kila nyama wa porini jila lake, lakini yeye Adamu hakuona mtu mwenziwe wa kusaidiana naye.
21
Ndipo, Bwana Mungu alipomtia Adamu usingizi mzito, akalala usingizi kabisa. Kisha akamtoa ubavu wake mmoja, napo mahali pake akapaziba na nyama.
22
Huo ubavu, aliomtoa Adamu, Bwana Mungu akauumba kuwa mke, akampeleka kwake Adamu.
23
Adamu akasema: Kweli huyu ni mfupa utokao katika mifupa yangu, ni mwenye mwili utokao mwilini mwangu; kwa hiyo ataitwa mwanamke, kwa kuwa ametolewa katika mwanamume.
24
Kwa sababu hii mtu atamwacha baba yake na mama yake, agandamiane na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.
25
Nao wote wawili, Adamu na mkewe, walikuwa wenye uchi, lakini hawakuona soni.
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 3 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50