bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Genesis 30
Genesis 30
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 29
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 31 →
1
Raheli alipoona, ya kuwa hamzalii Yakobo wana, ndipo, alipomwonea dada yake wivu, akamwambia Yakobo: Unipatie wana! Nisipowapata nitakufa.
2
Ndipo, makali ya Yakobo yalipomwakia Raheli, akamwambia: Je? Mimi ni kama Mungu aliyekunyima mazao ya tumbo?
3
Akajibu: Tazama! Yuko kijakazi wangu Biliha, ingia kwake, azae magotini pangu, mimi nami nipate mlango kwake yeye.
4
Akampa kijakazi wake Biliha kuwa mkewe, naye Yakobo akaingia kwake.
5
Hivyo Biliha akapata mimba, akamzalia Yakobo mtoto mume.
6
Ndipo, Raheli aliposema: Mungu amenihukumia, akaisikia nayo sauti yangu, akanipa mtoto mume, kwa sababu hii akamwita jina lake Dani (Mhukumu).
7
Kisha Biliha, kijakazi wake Raheli, akapata mimba tena, akamzalia Yakobo mtoto mume wa pili.
8
Raheli akasema: Nimepiga vita vya Mungu vya kupigana na dada yangu, nami nikashinda. Kwa hiyo akamwita jina lake Nafutali (Vita vyangu).
9
Lea alipoona, ya kuwa amekoma kuzaa, akamchukua kijakazi wake Zilpa, akampa Yakobo kuwa mkewe.
10
Huyu Zilpa, kijakazi wake Lea, akamzalia Yakobo mtoto mume;
11
ndipo, Lea aliposema: Nina bahati, akamwita jina lake Gadi (Bahati).
12
Zilpa, kijakazi wake Lea, akamzalia Yakobo mtoto mume wa pili;
13
ndipo, aliposema: Mimi ni mwenye shangwe, kwani wanawake watanishangilia. Kwa hiyo akamwita jina lake Aseri (Shangwe).
14
Rubeni alipotembea siku za mavuno ya ngano, akaona tunguja shambani akampelekea mama yake. Naye Raheli akamwambia Lea: Unigawie na mimi tunguja za mwanao!
15
Lakini huyu akajibu: Haitoshi, ukimchukua mume wangu? Unazitakia nini hizi tunguja za mwanangu? Raheli akajibu: Basi, na alale kwako usiku huu, nipate tu tunguja za mwanao!
16
Jioni Yakobo aliporudi toka shambani, Lea akamwendea njiani, akamwambia: Ingia kwangu! Kwani nimekununua leo kwa kutoa tunguja za mwanangu. Alipolala naye usiku huo,
17
Mungu akamsikia Lea, akapata mimba, akamzalia Yakobo mtoto mume wa tano.
18
Ndipo, Lea aliposema: Mungu amenipa mshahara wangu, kwa kuwa nimempa mume wangu kijakazi wangu, kwa hiyo akamwita jina lake Isakari (Mtu wa Mshahara).
19
Lea akapata mimba tena, akamzalia Yakobo mtoto mume wa sita;
20
ndipo, Lea aliposema: Mara hii Mungu amenipatia tunzo zuri. Sasa mume wangu atakaa kwangu, kwani nimemzalia watoto waume sita; kwa hiyo akamwita jina lake Zebuluni (Kao.)
21
Baadaye akazaa mtoto mke, akamwita jina lake Dina.
22
Ndipo, Mungu alipomkumbuka Raheli, Mungu akamsikia, akalifungua tumbo lake.
23
Kwa hiyo naye akapata mimba, akazaa mtoto mume, akasema: Mungu ameniondolea yaliyonitia soni,
24
akamwita jina lake Yosefu (Huongeza) akisema: Bwana aniongezee mwana mwingine!
25
Raheli alipokwisha kumzaa Yosefu, Yakobo akamwambia Labani: Nipe ruhusa, niende kwetu katika nchi yangu!
26
Nipe wake zangu na wanangu, ambao nilikutumikia, niwapate! Kisha niende zangu, kwani wewe unaujua utumishi wangu, niliokutumikia.
27
Naye Labani akamwambia: Ninataka kuona upendeleo machoni pako, kwa kuwa nimeona, ya kama Bwana amenibariki kwa ajili yako.
28
Akaendelea kusema: Ninakuomba, sema mshahara, unaotaka kwangu! Ndio, nitakaokupa.
29
Akamwambia: Wewe unajua mwenyewe, jinsi nilivyokutumikia, tena jinsi makundi yako yalivyokua kwangu.
30
Kwani kabla ya kuja kwangu yalikuwa madogo, lakini sasa yamesambaa kwa kuwa mengi, maana Bwana amekubariki pote, nilipokwenda. Sasa wao waliomo nyumbani mwangu niwafanyie kazi lini?
31
Naye akamwuliza: Nikupe nini? Yakobo akamwambia: Usinipe cho chote! Nifanyie hili tu: acha, niwachunge tene mbuzi na kondoo wako na kuwaangalia!
32
Tena nipite leo kwenye mbuzi na kondoo wako wote kuondoa kwao kondoo wote wenye mawaa na madoadoa nao wana weusi wote pia nao mbuzi wote wenye madoadoa na mawaa; basi, watakaozaliwa kuwa hivyo ndio mshahara wangu.
33
Navyo ndiyo, nitakavyojulikana katika siku zijazo kuwa mwenye kweli: utakapokuja kuwatazama walio mshahara wangu, kila mbuzi asiye mwenye madoadoa na mawaa naye kila kondoo asiye mweusi atakuwa amekwibwa na mimi.
34
Labani akamwitikia kwamba: Basi, na viwe hivyo, ulivyosema!
35
Kisha Labani akaondoa siku hiyohiyo madume ya mbuzi wote waliokuwa wenye madoadoa na mawaa nao majike ya mbuzi wote waliokuwa wenye madoadoa na mawaa, wote pia waliokuwa wenye peupe, nao kondoo weusi wote, akawatia mikononi mwa wanawe,
36
akawapeleka mwendo wa siku tatu, pawe hapo mahali pakubwa katikati yake yeye na Yakobo. Kisha Yakobo akapata kuwachunga mbuzi na kondoo wake Labani waliosalia.
37
Kisha Yakobo akajitwalia matawi mabichi ya mikumbi na ya milozi na ya migude, akayabanduabandua, yapate mabaka meupe ya kutokeza sana huo weupe penye hayo matawi.
38
Kisha akayasimika hayo matawi, aliyoyabandua hivyo, penye birika za kuwanyweshea maji mbuzi na kondoo kwamba: wao wakija kunywa maji, wayaone hayo, wanyegeshwe wakija kunywa.
39
Nao mbuzi na kondoo waliponyegeshwa mbele ya hao matawi, ndipo, hao mbuzi na kondoo walipozaa wenye madoadoa na vipakupaku na mawaa.
40
Hawa wana mbuzi Yakobo akawatenga, akawatanguliza mbele ya mbuzi na kondoo wengine, hao wote waliokuwa wake Labani wawatazame wale wenye madoadoa nao mbuzi na kondoo weusi; hivyo akajipatia makundi yake yeye, nayo haya hakuyachanganya nayo yake Labani.
41
Kila mara mbuzi na kondoo wenye nguvu waliponyegeshwa, Yakobo akayaweka yale matawi machoni pao mbuzi na kondoo penye birika, wazidi kunyegeshwa wakiyaona hayo matawi.
42
Lakini kwao wale mbuzi na kondoo waliokuwa wanyonge hakuyaweka; kwa sababu hii wale wanyonge wakawa wake Labani, lakini wale wenye nguvu wakawa wake Yakobo.
43
Hivyo ndiyo, huyu mtu alivyopata mali nyingi sanasana, mbuzi na kondoo wake wakawa wengi, nao watumwa wa kiume na wa kike na ngamia na punda alikuwa nao.
← Chapter 29
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 31 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50