bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Genesis 12
Genesis 12
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 11
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 13 →
1
Bwana akamwambia Aburamu: Toka katika nchi yako kwenye ndugu zako namo nyumbani mwa baba yako, uende katika nchi, nitakayokuonyesha!
2
Nitakufanya kuwa taifa kubwa, nitakubariki na kulikuza jina lako, uwe mbaraka.
3
Nitawabariki watakaokubariki, naye atakayekuapiza nitamwapiza. Mwako ndimo, koo zote za nchini zitakamobarikiwa.
4
Ndipo, Aburamu alipoondoka, kama Bwana alivyomwambia, naye Loti akaenda naye. Naye Aburamu alikuwa mwenye miaka 75 alipotoka Harani.
5
Aburamu akamchukua mkewe Sarai na Loti, mwana wa nduguye, nayo mapato yao yote, waliyojipatia, nao watu wao wote, waliowapata huko Harani; ndivyo, walivyotoka kwenda katika nchi ya Kanaani.
6
Walipofoka katika nchi ya Kanaani, Aburamu akaikata hiyo nchi, mpaka akifika mahali pa Sikemu penye mvule wa More; siku zile Wakanaani walikaa katika nchi hiyo.
7
Huko Bwana akamtokea Aburamu, akamwambia: Nchi hii nitawapa wao wa uzao wako! Ndipo, alipomjengea Bwana pa kumtambikia, kwa kuwa alimtokea hapo.
8
Kisha akaondoka huko kwenda kwenye mlima ulioko upande wa maawioni kwa jua kwa Beteli, akalipiga hema lake mahali, Beteli ulipokuwa upande wa baharini nao Ai upande wa maawioni kwa jua; huko akajenga pa kumtambikia Bwana, akalitambikia Jina la Bwana.
9
Kisha Aburamu akaondoka huko, akaendelea kusafiri upande wa kusini.
10
Njaa ilipoingia katika nchi ile, Aburamu akashuka kwenda Misri kukaa ugenini huko, kwani njaa ilikuwa kubwa.
11
Walipofika karibu kuingia Misri akamwambia mkewe Sarai: Tazama, ninakujua kuwa mwanamke mwenye mwili mzuri.
12
Itakuwa, Wamisri watakapokuona watasema: Huyu ni mkewe. Basi, mimi wataniua, lakini wewe watakuacha, ukae.
13
Kwa hiyo sema, ya kuwa u dada yangu, nipate mema kwa ajili yako! Hivyo ndivyo, roho yangu nayo itakavyopona kwa ajili yako.
14
Ikawa, Aburamu alipoingia Misri, Wamisri wakamwona mke kuwa mzuri sana.
15
Nao wakuu wa Farao walipomwona, wakamsifia Farao; ndipo, huyo mwanamke alipochukuliwa kukaa nyumbani mwa Farao.
16
Naye akamfanyia Aburamu mema kwa ajili yake, akapata mbuzi na kondoo na ng'ombe na punda na watumwa wa kiume na wa kike na punda wa kike na ngamia.
17
Lakini Bwana akampiga Farao mapigo makuu, nao mlango wake, kwa ajili ya Sarai, mkewe Aburamu.
18
Ndipo, Farao alipomwita Aburamu, akamwambia: Kwa nini umenifanyizia hivyo usiponiambia, ya kuwa ni mkeo?
19
Kwa nini umesema: Ni dada yangu, mimi nikamchukua kuwa mke wangu? Sasa mchukue huyu mkeo, uende zako!
20
Kisha Farao akamwagizia watu, wampeleke yeye na mkewe na mali zake zote.
← Chapter 11
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 13 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50