bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Genesis 48
Genesis 48
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 47
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 49 →
1
Ikawa, mambo hayo yalipokwisha, wakamwambia Yosefu: Tazama! Baba yako ni mgonjwa. Ndipo, alipowachukua wanawe wawili Manase na Efuraimu kwenda naye.
2
Walipompasha Yakobo habari kwamba: Tazama! Mwanao Yosefu anakuja kwako, Isiraeli akajitia nguvu, apate kukaa kitandani.
3
Yakobo akamwambia Yosefu: Mwenyezi Mungu alinitokea Luzi katika nchi ya Kanaani, akanibariki,
4
akaniambia: Utaniona, nikikupa kuzaa wana, nikupe kuwa wengi, uwe mkutano wa makabila ya watu; kisha nchi hii nitawapa wao wa uzao wako wajao nyuma yako, mwichukue kuwa yenu kale na kale.
5
Sasa wanao wawili uliowazaa katika nchi hii ya Misri, nilipokuwa sijafika huku Misri, ni wangu; Efuraimu na Manase watakuwa wangu, kama Rubeni na Simeoni walivyo wangu,
6
nao wanao wengine, utakaowazaa nyuma yao, watakuwa wako; lakini wale wataitwa pamoja na majina ya ndugu zao, wagawiwe nao mafungu yao ya nchi yatakayokuwa yao.
7
Nami nilipotoka Mesopotamia nilifiwa na Raheli njiani katika nchi ya Kanaani, uliposalia mwendo wa kipande kifupi tu kufika Efurata, nami nikamzika huko kwenye njia ya kwenda Efurata, ndio Beti-Lehemu.
8
Isiraeli alipowaona wana wa Yosefu akauliza: Hawa ni nani?
9
Yosefu akamwambia baba yake: Ndio wanangu, Mungu alionipa huku; ndipo, alipomwambia: Walete kwangu niwabariki!
10
Maana macho yake Isiraeli yalikuwa yameguiwa na kiza, hayakuweza kuona kwa ajili ya uzee. Yosefu alipowafikisha karibu yake, akawanonea na kuwakumbatia.
11
Kisha Isiraeli akamwambia Yosefu: Mimi sikuyawaza, ya kwamba nitauona uso wako, tena tazama! Mungu amenipa kuwaona nao wa uzao wako!
12
Ndipo, Yosefu alipowaondoa magotini pake, akamwinamia na kuufikisha uso wake chini.
13
Kisha Yosefu akawachukua wote wawili, Efuraimu kwa mkono wake wa kuume na kumweka kushotoni kwake Isiraeli, naye Manase kwa mkono wake wa kushoto na kumweka kuumeni kwake Isiraeli; ndivyo, alivyowapeleka kwake.
14
Lakini Isiraeli akaupeleka mkono wake wa kuuume, akaubandika kichwani pake Efuraimu aliyekuwa mdogo, nao mkono wake wa kushoto akaubandika kichwani pake Manase, naye akavifanya kusudi akiwabandikia mikono hivyo, kwani Manase ndiye aliyezaliwa wa kwanza.
15
Kisha akambariki Yosefu na kusema: Mungu, ambaye baba yangu Aburahamu na Isaka walifanya mwenendo machoni pake, yeye Mungu alikuwa mchungaji wangu tangu hapo, nilipozaliwa, mpaka siku hii ya leo;
16
naye malaika aliyenikomboa katika mabaya yote na awabariki hawa vijana, jina langu nayo majina ya baba zangu Aburahamu na Isaka yatajwe kwao, wawe wengi sana katika nchi hii!
17
Yosefu alipoona, ya kuwa baba yake ameubandika mkono wake wa kuume kichwani pake Efuraimu hakupendezwa; kwa hiyo akaushika huo mkono wa baba yake, auondoe kichwani pake Efuraimu, apate kuubandika kichwani pake Manase.
18
Naye Yosefu akamwambia baba yake: Hivi sivyo, baba, kwani huyu ni wa kwanza; ubandike mkono wako wa kuume kichwani pake!
19
Lakini baba yake akakataa akisema: Navijua, mwanangu, navijua kweli; huyu naye atakuwa kabila la watu, huyu naye atakuwa mkubwa, lakini ndugu yake mdogo atakuwa mkubwa kuliko yeye, nao wa uzao wake watakuwa mataifa mengi.
20
Kisha akawabariki siku hiyo kwamba: Mwisiraeli atakapobariki atalitaja jina lako kwamba: Mungu na akupe kuwa kama Efuraimu na kama Manase! Hapa napo akamtaja Efuraimu mbele ya Manase.
21
Kisha Isiraeli akamwambia Yosefu: Tazama! Mimi ninakufa, lakini Mungu atakuwa pamoja nanyi, awarudishe katika nchi ya baba zenu.
22
Nami nimekupa fungu moja zaidi ya ndugu zako, nililolichukua kwao Waamori kwa upanga wangu na kwa upindi wangu.
← Chapter 47
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 49 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50