bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Genesis 35
Genesis 35
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 34
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 36 →
1
Mungu akamwambia Yakobo: Inuka, upande kwenda Beteli kukaa huko! Tena jenga huko pa kumtambikia Mungu aliyekutokea huko, ulipomkimbia kaka yako Esau!
2
Ndipo, Yakobo alipowaambia wao wa mlango wake nao wote, aliokuwa nao: Iondoeni miungu migeni iliyo kwenu bado! Kisha jieueni na kuvaa nazo nguo nyingine!
3
Kisha na tuondoke, tupande kwenda Beteli, nijenge huko pa kumtambikia Mungu aliyeniitikia siku ile, nilipokuwa nimesongeka, akawa pamoja na mimi katika safari hiyo, niliyokwenda.
4
Ndipo, walipompa Yakobo miungu migeni yote iliyokuwa mikononi mwao, nayo mapete ya masikioni mwao, naye Yakobo akayafukia chini ya mkwaju uliokuwa karibu ya Sikemu.
5
Walipoondoka, kitisho cha Mungu kikaiguia ile miji yote iliyowazunguka, wasiwakimbize wana wa Yakobo na kuwafuata.
6
Ndivyo, yakobo alivyofika Luzi katika nchi ya Kanaani, ndio Beteli, yeye pamoja na watu wote, aliokuwa nao.
7
Akajenga huko pa kutambikia, akapaita mahali pale Mungu wa Beteli, kwani ndiko, Mungu alikomtokea, alipomkimbia kaka yake.
8
Siku zile akafa Debora aliyekuwa yaya wake Rebeka, akazikwa upande wa chini hapo Beteli chini ya mvule, nao ukaitwa Mvule wa Maombolezo.
9
Mungu akamtokea Yakobo tena, aalipokwisha kurudi Mesopotamia, akambariki.
10
Hapo Mungu akamwambia: Jina lako ni Yakobo, lakini usiitwe tena jina lako Yakobo, ila jina lako liwe Isiraeli! Kwa hiyo wakamwita Isiraeli.
11
Kisha Mungu akamwambia: Mimi ni Mungu Mwenyezi; na uzae wana, upate kuwa wengi, taifa na kundi zima la mataifa litatoka kwako, nao wafalme watatoka kiunoni mwako.
12
Nayo nchi hii, niliyompa Aburahamu na Isaka, nakupa wewe nawe, nao wa uzao wako wajao nyuma yako nitawapa nchi hii.
13
Kisha Mungu akapaa juu na kutoka kwake mahali hapo, aliposema naye.
14
Mahali hapo, aliposema naye, Yakobo akapasimamisha nguzo, nayo nguzo hiyo ilikuwa ya mawe, akaimwagia kinywaji cha tambiko, kisha akaipaka mafuta juu yake.
15
Yakobo akapaita jina lake mahali hapo, Mungu aliposema naye, Beteli.
16
Kisha wakaondoka Beteli. Ikawa, uliposalia mwendo wa kipande kifupi tu kufika Efurata, Raheli akazaa, nako huko kuzaa kwake kukawa kugumu.
17
Hapo, machungu yake ya kuzaa yalipozidi, mzalishaji akamwambia: Usiogope! Kwani nayo mara hii utazaa mtoto mume.
18
Ikawa roho yake ilipomtoka kwa kupatwa na kufa, akamwita jina lake Benoni (Azimalizaye nguvu zangu), lakini baba yake akamwita Benyamini (Mbahati).
19
Ndivyo, Raheli alivyokufa, akazikwa hapohapo penye njia ya kwenda Efurata, ndio Beti-Lehemu.
20
Yakobo akasimamaisha juu ya kaburi lake nguzo ya mawe, nayo nguzo hiyo iko juu ya kaburi la Raheli hata siku ya leo.
21
Kisha Isiraeli akaondoka, akalipiga hema lake ng'ambo ya huko ya mnara wa Ederi.
22
Ikawa, Israeli alipokaa katika nchi ile, Rubeni akaenda, akalala na Biliha, suria ya baba yake; naye Isiraeli akavisikia.
23
Wana wa Yakobo walikuwa kumi na wawili. Wana wa Lea ni wanawe wa kwanza wa Yakobo: Rubeni, tena Simeoni na Lawi na Yuda na Isakari na Zebuluni.
24
Wana wa Raheli ni Yosefu na Benyamini.
25
Nao wana wa Biliha, kijakazi wake Raheli, ni Dani na Nafutali.
26
Nao wana wa Zilpa, kijakazi wake Lea, ni Gadi na Aseri. Hawa ndio wana wa Yakobo, aliozaliwa huko Mesopotamia.
27
Kisha Yakobo akafika kwa baba yake Isaka kule Mamure karibu ya Kiriati-Arba, ndio Heburoni, aburahamu na Isaka walikokaa ugenini.
28
Nazo siku zake Isaka zilikuwa miaka 180.
29
Ndipo, Isaka alipozimia, akafa, akachukuliwa kwenda kwao walio wa ukoo wake; naye alikuwa mkongwe mwenye siku za kushiba siku za kuwapo. Kisha wanawe Esau na Yakobo wakamzika.
← Chapter 34
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 36 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50