bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Genesis 43
Genesis 43
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 42
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 44 →
1
Njaa ikawa nzito katika nchi.
2
Walipokwisha kuzila hizo ngano, walizozileta toka Misri, baba yao akawaambia: Rudini huko kutununulia vilaji vichache!
3
Ndipo, Yuda alipomwambia kwamba: Yule mtu alitushuhudia kwa ukali kwamba: Hamtauona uso wangu, ndugu yenu asipokuwa nanyi.
4
Ukitaka kumtuma huyu ndugu yetu kwenda pamoja na sisi, tutatelemka kukununulia vilaji;
5
lakini usipotaka kumtuma, hatuwezi kutelemka, kwani yule mtu alituambia: Hamtauona uso wangu, ndugu yenu asipokuwa nanyi.
6
Ndipo, Isiraeli aliposema: Kwa nini mmenifanyizia haya mabaya ya kumpasha yule mtu habari, ya kuwa yuko ndugu yenu mwingine?
7
Wakajibu: Yule mtu alituuliza mara kwa mara habari za kwetu na za udugu wetu kwamba: Baba yenu yuko mzima bado? Mna ndugu mwingine? Nasi hatukuwa na budi kumjibu hayo maulizo yake; tungalijuaje, ya kuwa anataka kutuambia: Sharti mmtelemshe ndugu yenu?
8
Naye Yuda akamwambia baba yake Isiraeli: Mtume huyu kijana kwenda na mimi, tupate kuondoka kwenda huko, tupone, tusife sisi na wewe na watoto wetu.
9
Mimi na niwe mdhamini wake, na umtafute mkononi mwangu! Nisipomrudisha na kumsimamisha mbele yako nitakuwa nimekukosea siku zote.
10
Kama hatungalikawilia, tungalikuwa tumekwisha kurudi hata mara mbili.
11
Basi, baba yao Isiraeli akawaitikia kwamba: Kama hayana budi kuwa hivyo, haya! Yafanyizeni! Chukueni vyomboni mwenu mazao ya nchi hii yanayosifiwa, tena mpelekeeni yule mtu kuwa matunzo yake: mafuta ya mkwaju machache na asali kidogo na manukato na uvumba na kungu na lozi!
12
Tena chukueni mikononi mwenu fedha za mara mbili, nazo fedha zile zilizorudishwa katika magunia yenu sharti mzirudishe mikononi mwenu, labda yuko aliyekosa kwa kupotelewa na amri.
13
Kisha mchukueni naye ndugu yenu, mwondoke kurudi kwake yule mtu!
14
Naye Mwenyezi Mungu na awapatie kuhurumiwa usoni pake yule mtu, awafungulie ndugu yenu mwingine, mje naye hata naye Benyamini! Lakini mimi, kama nilivyopotelewa na wana, kama inanipasa, na nipotelewe tena na wana.
15
Kisha hao watu wakayachukua hayo matunzo, nazo fedha za mara mbili wakazichukua mikononi mwao, naye Benyamini, wakaondoka kutelemka kwenda Misri. Walipomtokea Yosefu,
16
naye Yosefu alipomwona Benyamini kuwa nao, akamwambia mkuu wa nyumba yake: Waingize watu hawa humo nyumbani! Kisha chinja nyama, uiandalie vizuri, kwani watu hawa watakula kwangu saa sita.
17
Yule mtu akafanya, kama Yosefu alivyomwagiza, akawaingiza hao watu nyumbani mwa Yosefu.
18
Lakini watu hao wakashikwa na woga kwa kuingizwa nyumbani mwake Yosefu, wakasema: Tumeingizwa humu kwa ajili ya hizo fedha zilizorudishwa hapo kwanza katika magunia yetu, apate kutusingizia na kutulipisha yaliyotuangukia, atuchukue sisi pamoja na punda wetu, tuwe watumwa wake.
19
Kwa hiyo wakamkaribia yule mkuu wa nyumba ya Yosefu, wakasema naye hapo pa kuingia nyumbani,
20
wakamwambia: E bwana, tulipotelemka safari ya kwanza kununua ngano,
21
nasi tulipofika kambini, tukafungua magunia yetu, tukaona kila mtu fedha zake juu ndani ya gunia lake, nazo hizo fedha zetu zilikuwa zenye kipimo chao sawasawa, kwa hiyo tumezirudisha mikononi mwetu;
22
nazo fedha nyingine tumetelemka nazo mikononi mwetu za kununua vilaji; hatumjui aliyeziweka hizo fedha zetu katika magunia yetu.
23
Naye akasema: Tulieni tu, msiogope! Mungu wenu na Mungu wa baba yenu aliwapatia kilimbiko katika magunia yenu, fedha zenu zilifika kwangu. Kisha akamfungua Simeoni, akamleta kwao,
24
akawaingiza nyumbani mwake Yosefu, akawapa maji ya kuiosha miguu yao, nao punda wao akawapata chakula.
25
Nao wakayatengeneza matunzo yao, mpaka Yosefu akaja saa sita, kwani walisikia, ya kuwa watakula chakula huko.
26
Yosefu alipoingia humo nyumbani, wakampelekea hayo matunzo mikononi mwao nyumbani mwake na kumwangukia hapo chini.
27
Akawaamkia kwa upole, akawauliza: Baba yenu mzee, ambaye mliniambia, ya kuwa yuko mzima, na sasa hajambo?
28
Wakamwambia: Mtumwa wako baba yetu hajambo, yuko mzima bado; kisha wakamwinamia na kumwangukia.
29
Alipoyainua macho yake akamwona ndugu yake Benyamini aliyezaliwa na mama yake, akauliza: Kumbe huyu ni ndugu yenu mdogo, ambaye mliniambia habari zake? Akasema: Mungu na akugawie mema, mwanangu!
30
Kisha Yosefu akakimbilia chumba kingine, apate kulia machozi, kwani alichafukwa na moyo kwa kumfurahia nduguye, namo mle chumbani machozi yakamtoka kweli.
31
Alipokwisha kuunawa uso wake, akawatokea tena na kutulia kwa kujizuia, akaagiza: Leteni chakula!
32
Wakamwandalia yeye peke yake nao ndugu zake peke yao nao Wamisri waliokula naye peke yao, kwani ni mwiko wa Wamisri kula chakula pamoja na Waebureo, huwachukiza.
33
Wakawakalisha mbele yake, kama walivyofuatana: aliyezaliwa wa kwanza hapo palipoupasa ukubwa wake, naye mdogo hapo palipoupasa ujana wake; kwa hiyo hao watu wakastaajabu na kutazamana wao kwa wao.
34
Wakawapa vyakula vilivyotoka mezani pake Yosefu, lakini Benyamini akaandaliwa vyakula vilivyovipita vyao wote kwa wingi mara tano. Kisha wakanywa, hata wakachangamshwa pamoja naye.
← Chapter 42
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 44 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50