bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Genesis 25
Genesis 25
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 24
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 26 →
1
Aburahamu akaoa tena, jina lake mkewe ni Ketura.
2
Huyu akamzalia Zimurani na Yokisani na Medani na Midiani na Isibaki na Sua.
3
Naye Yokisani akamzaa Saba na Dedani; nao wana wa Dedani walikuwa Waasuri na Waletusi na Walumu.
4
Nao wana wa Midiani walikuwa Efa na Eferi na Henoki na Abida na Eldaa; hawa wote walikuwa wana wa Ketura.
5
Kisha Aburahamu akampa Isaka yote pia, aliyokuwa aliyo.
6
Lakini wana wa masuria, Aburhamu aliokuwa nao, Aburahamu akawapa matunzo, kisha akawatuma angaliko mzima kuondoka kwa mwanawe Isaka, waende upande wa maawioni kwa jua kukaa katika nchi ya huko maawioni kwa jua.
7
Siku zote za miaka ya kuwapo kwake Aburahamu, aliyokuwapo, ni miaka 175.
8
Kisha Aburahamu akazimia, akafa kwa kuwa mkongwe sana, naye alikuwa mzee aliyeshiba siku zake; ndipo, alipochukuliwa kwenda kwao walio wa ukoo wake.
9
Wanawe Isaka na Isimaeli wakamzika mle pangoni mwa Makipela katika shamba la Yule Mhiti Efuroni, mwana wa Sohari, linaloelekea Mamure.
10
Ndilo lile shamba, Aburahamu alilolinunua kwa wana wa Hiti; ndiko, Aburahamu alikozikwa na mkewe Sara.
11
Aburahamu alipokwisha kufa, Mungu akambariki mwanawe Isaka. Naye Isaka akakaa kwenye kisima cha Mwenye Uzima Anionaye.
12
Hivi ndiyo vizazi vya Isimaeli, mwana wa Aburahamu, ambaye Hagari wa Misri aliyekuwa kijakazi wake Sara alimzalia Aburahamu.
13
Nayo haya ndiyo majina ya wana wa Isimaeli waliyoitwa hivyo, walivyofuatana kuzaliwa: Mwana wa kwanza wa Isimaeli ni Nebayoti, tena Kedari na Adibeli na Mibusamu,
14
na Misima na Duma na Masa;
15
Hadadi na Tema, Yeturi, Nafisi na Kedima.
16
Hawa ndio wana wa Isimaeli, nayo haya ndiyo majina yao, waliyoitwa katika vijiji vyao na katika makambi ya mahema yao; nao walikuwa wakuu 12 wa makabila yao.
17
Nayo hii ndiyo miaka ya kuwapo kwake Isimaeli, miaka 137; kisha akazimia, akafa, akachukuliwa kwenda kwao walio wa ukoo wake.
18
Nao wale walikaa toka Hawila mpaka Suri unaoelekea Misri hata kufika Asuri; hivyo alikuwa ametua mbele yao ndugu zake wote.
19
Hivi ndivyo vizazi vya Isaka, mwana wa Aburahamu: Aburahamu alimzaa Isaka.
20
Isaka alikuwa mwenye miaka 40 alipomchukua Rebeka kuwa mkewe, naye alikuwa binti Betueli, Mshami na Mesopotamia, dada yake Mshami Labani.
21
Isaka akamwombea mkewe kwake Bwana, kwani alikuwa mgumba; naye Bwana akayaitikia maombo yake, ndipo, mkewe Rebeka alipopata mimba,
22
Watoto walipogongana tumboni mwake, akasema: Kama ndivyo, nimevipatia nini? Akaenda kumwuliza Bwana.
23
Bwana akamwambia: Mataifa mawili yamo tumboni mwako, kabila mbili za watu zinatengana tumboni mwako zikitaka kutoka, kabila moja itatenda nguvu kuishinda ile nyingine, naye mkubwa atamtumikia nduguye.
24
Siku zake za kuzaa zilipotimia, ikaonekana, ya kuwa wana wa pacha wamo tumboni mwake.
25
Wa kwanza alipotoka alikuwa mwekundu, mwenye manyoya mwilini mote kama vazi la ngozi, wakamwita jina lake Esau.
26
Ndugu yake alipotoka baadaye, mkono wake ulikuwa unakishika kisigino cha Esau, wakamwita jina lake Yakobo. Naye Isaka alikuwa mwenye miaka 60, mkewe alipowazaa.
27
Hawa watoto walipokua, Esau akawa wa porini na fundi wa kuwinda, lakini Yakobo akawa mtulivu, akapenda kukaa hemani.
28
Kwa hiyo Isaka akampenda Esau, kwa kuwa alimpatia nyama za kula za porini, lakini Rebeka alikuwa anampenda Yakobo.
29
Siku moja Yakobo alipopika kunde, Esau akarudi toka porini, naye alikuwa amechoka sana.
30
Ndipo, Esau alipomwambia Yakobo: Nipe, nile upesi hicho chekunduchekundu! Kwani nimechoka sana. Kwa sababu hii wakaliita jina lake Edomu (Mwekundu).
31
Lakini Yakobo akasema: Niuzie leo hivi ukubwa wako!
32
Naye Esau akasema: Tazama, mimi ninakwenda kufa! Hapo ukubwa utanifaa nini?
33
Yakobo akasema: Uniapie leo hivi! Basi, akamwapia; hivyo ndivyo, alivyomwuzia Yakobo ukubwa wake.
34
Kisha Yakobo akampa mkate na hizo kunde, alizozipika; naye akala, akanywa, kisha akainuka, akaenda zake. Hivyo ndivyo, Esau alivyoubeza ukubwa.
← Chapter 24
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 26 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50