bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Genesis 27
Genesis 27
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 26
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 28 →
1
Ikawa, Isaka alipokuwa mkongwe, macho yake yakatenda kiza, yasione; ndipo, alipomwita mwanawe mkubwa Esau, akamwambia: Mwanangu! Naye akamwitikia: Mimi hapa!
2
Akasema: Tazama, nimekuwa mkongwe, siijui siku ya kufa kwangu.
3
Sasa yachukue mata yako, ndio podo lako na upindi wako, uende porini kuniwindia nyama!
4
Kisha unitengenezee kilaji cha urembo, kama ninavyokipenda, uniletee, nile, roho yangu ipate kukubariki, nikingali bado sijafa.
5
Lakini Rebeka alikuwa ameyasikia, Isaka aliyomwambia mwanawe Esau. Esau alipokwisha kwenda porini kuwinda nyama ya kumpelekea baba,
6
Rebeka akamwambia mwanawe Yakobo kwamba: Tazama, nimesikia, baba yako akimwambia kaka yako Esau kwamba:
7
Niletee nyama ya porini, unitengenezee kilaji cha urembo, nile, nipate kukubariki usoni pa Bwana kabla ya kufa kwangu!
8
Sasa mwanangu, isikie sauti yangu, uyafanye nitakayokuagiza!
9
Nenda makundini kunichukulia huko wana wawili wa mbuzi walio wazuri, nimtengenezee baba yako nyama zao kuwa kilaji cha urembo, kama anavyokipenda.
10
Kisha utampelekea baba yako, ale, apate kukubariki kabla ya kufa kwake.
11
Lakini Yakobo akamwambia mama yake Rebeka: Tazama, kaka yangu Esau ni mwenye manyoya, lakini mimi sinayo.
12
Labda baba atanipapasa; ndipo, nitakapokuwa kama mdanganyifu machoni pake; hivyo nitajipatia maapizo, sio mbaraka.
13
Naye mama yake akamwambia: Maapizo yako na yanijie mimi, mwanangu! Isikie tu sauti yangu, uende kunichukulia wana wa mbuzi!
14
Ndipo, alipokwenda, akawachukua, akamplekea mama yake, naye mama yake akawatengeneza kuwa kilaji cha urembo, kama baba yake alivyokipenda.
15
Kisha Rebeka akazichukua nguo za mwanawe mkubwa Esau zilizo nzuri mno, alizokuwa nazo nyumbani mwake, akamvika mwanawe mdogo Yakobo.
16
Nazo ngozi za wale wana wa mbuzi akamvika mikononi namo shingoni mlimokuwa hamna manyoya.
17
Kisha akampa mwanawe Yakobo mkononi mwake hicho kilaji cha urembo pamoja na mkate, alioutengeneza nao.
18
Alipoingia mwa baba yake akasema: Baba! Naye akasema: Mimi hapa! Wewe ndiwe nani, mwanangu?
19
Yakobo akamwambia baba yake: Mimi ni Esau, mwanao wa kwanza; nimefanya, kama ulivyoniagiza. Inuka, ukae, ule nyama zangu, nilizokuwindia, roho yako ipate kunibariki!
20
Isaka akamwuliza mwanawe: Mwanangu, umepataje nyama upesi hivyo? Akasema: Bwana Mungu wako amemtuma, anijie njiani.
21
Kisha Isaka akamwambia Yakobo: Nikaribie, mwanangu, nikupapase, nione, kama wewe ndiwe mwanangu Esau, au kama siwe!
22
Yakobo akamkaribia baba yake Isaka, akampapasa, akasema: Sauti ni sauti yake Yakobo, lakini mikono ni mikono yake Esau.
23
Hakumtambua, kwa kuwa mikono yake ilikuwa kama mikono ya kaka yake Esau yenye manyoya; ndipo, alipombariki.
24
Alipomwuliza tena: Wewe ndie kweli mwanangu Esau? akasema: Ndio, ni mimi.
25
Ndipo, alipomwambia: Niletee karibu, nile nyama, ulizoniwindia, mwanangu, roho yangu ipate kukubariki! Akazileta karibu, naye akala; kisha akamletea mvinyo, akanywa.
26
Kisha baba yake Isaka akamwambia: Nikaribie, uninonee, mwanangu!
27
Alipomkaribia na kumnonea, akausikia mnuko wa mavazi yake, akambariki akisema: Tazama! Mnuko wa mwnangu ni kama mnuko wa shamba, Bwana alilolibariki.
28
Mungu akugawie umande wa mbinguni na manono ya nchi, ngano zako ziwe nyingi, hata mvinyo vilevile!
29
Makabila mazima na yakutumikie, koo za watu zikuangukie! Na uwe mkuu wa ndugu zako, wana wa mama yako wakuangukie! Atakayekuapiza na naapizwe! Atakayekubariki na abarikiwe naye!
30
Ikawa, Isaka alipokwisha kumbariki Yakobo, naye Yakobo alipokwisha kutoka usoni pa baba yake Isaka, ndipo, kaka yake Esau aliporudi kwa kuwinda.
31
Naye akatengeneza kilaji cha urembo, akampelekea baba yake, akamwambia baba yake: Baba, inuka, ule nyama, mwanao alizokuwinda, roho yako ipate kunibariki!
32
Ndipo, baba yake Isaka alipomwuliza: Wewe ndiwe nani? Akajibu: Mimi ni mwanao wa kwanza Esau.
33
Ndipo, Isaka aliposhangaa mshangao mkubwa mno, akasema: Sasa ni nani yule mwinda nyama aliyeniletea nyama, nikala, ulipokuwa hujaja bado, nikambariki? Naye atakuwa amebarikiwa.
34
Esau alipoyasikia haya maneno ya baba yake, akalia kilio kikubwa chenye uchungu mwingi sana, akamwambia baba yake: Baba, nibariki mimi nami!
35
Lakini akajibu: Ndugu yako mekuja kwa udanganyifu, akaipaat mbaraka yako.
36
Akasema: Kumbe haitwi jina lake Yakobo (Mdanganyi)? Naye amenidanganya sasa mara mbili: Kwanza ameuchukua ukubwa wangu, sasa ameichukua mbaraka yangu nayo. Kisha akauliza: Hukuniwekea mbaraka nami?
37
Isaka akajibu na kumwambia Esau: Tazama! Nimemweka kuwa mkubwa wako, nao ndugu zake wote nimempa, wamtumikie, hata ngano na mvinyo nimemfurikishia. Nawe wewe, mwanangu, nikufanyie nini?
38
Ndipo, Esau alipomwuliza baba yake: Baba, unayo mbaraka moja tu? Baba, nibariki mimi nami! Kisha Esau akaipaza sauti yake, akalia.
39
Ndipo, baba yake Isaka alipomwitikia na kumwambia: Tazama! Hapo, utakapokaa, manono ya nchi yatakuwa mbali, nao umande wa mbinguni juu.
40
Utajilisha mapato ya upanga wako, utamtumikia ndugu yako; lakini itakuwa, ukijikaza utalivunja kongwa, litoke shingoni pako!
41
Esau akamchukua Yakobo kwa ajili ya hiyo mbaraka, baba yake aliyombariki; kwa hiyo Esau akasema moyoni mwake: Siku za kumwombolezea baba ziko karibu; zitakapopita, nitamwua ndugu yangu Yakobo.
42
Rebeka alipopata habari ya lile shauri la mwananwe mkubwa Esau, akatuma kumwita mwanawe mdogo Yakobo, akamwambia: Tazama! Kaka yako Esau anajituliza moyo kwa kwamba, akuue.
43
Sasa mwnanangu, isikie sauti yangu! Inuka, ukimbilie Harani kwa kaka yangu Labani!
44
Na ukae kwake siku kidogo, mpaka machafuko ya kaka yako yatulie.
45
Hapo, haya makali ya kaka yako yatakapotulia, aache kukuwazia mabaya kwa kuyasahau uliyomfanyizia, ndipo, nitakapotuma kukuchukua huko. Kwa nini mwataka, nifiwe nanyi wawili siku moja?
46
Kisha Rebeka akamwambia Isaka: Ninachukizwa sana na kuwapo kwangu kwa ajili ya hao wanawake wa Kihiti. Kama Yakobo naye ataoa mwanamke miongoni mwao vijana wa kike wa Kihiti walio hivyo, kama hawa walivyo miongoni mwa vijana wa nchi hii, mimi nimeletewa nini huku?
← Chapter 26
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 28 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50