bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Genesis 34
Genesis 34
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 33
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 35 →
1
Dina, binti Lea, ambaye alimzalia Yakobo, akatoka kuwatazama wanawake wa nchi hiyo.
2
Sikemu, mwana wa Mhiwi Hamori aliyekuwa mkuu wa nchi hiyo, alipomwona akamchukua, akalala naye kwa kumtolea nguvu.
3
Nayo roho yake ikagandamana naye Dina, binti Yakobo, akampenda huyu kijana, akasema naye maneno mazuri ya kuingia moyoni mwake huyu kijana.
4
Kwa hiyo akamwambia baba yake Hamori kwamba: Niposee huyu mtoto, awe mke wangu.
5
Yakobo aliposikia, ya kuwa yule amemchafua mwanawe Dina, wanawe waume walikuwa porini pamoja na makundi yake, kwa hiyo Yakobo akanyamaza kimya, mpaka wakirudi.
6
Hamori, babake Sikemu, alipomtokea Yakobo kusema naye,
7
wana wa Yakobo wakaja kutoka porini. Walipoyasikia hao waume wakaona uchungu na kukasirika sana, kwani aliwafanyia wao Waisiraeli upumbavu mbaya wa kulala na binti Yakobo; hilo ni jambo lisilofanywa.
8
Hamori akasema nao kwamba: Roho yake mwanangu Sikemu inamtamani mtoto wenu, sasa mpeni, awe mkewe!
9
Na mwoane na sisi mkitupa wana wenu wa kike, nao wana wetu wa kike mjichukulie!
10
Na mkae nasi, nyo nchi hii na iwe wazi mbele yenu; kaeni tu na kuchuuzia huku, mjipatie huku mahali patakapokuwa penu.
11
Naye Sikemu akamwambia babake Dina na ndugu zake: Afadhali nipate upendeleo machoni penu! Nayo mtakayoniambia nitawapa.
12
Ijapo mtake mali nyingi sana za ukwe na matunzo mengi, nitawapa, kama mtakavyosema; nipeni tu kijana huyu kuwa mke wangu!
13
Ndipo, wana wa Yakobo walipomjibu Sikemu na baba yake Hamori kwa udanganyifu, kwa kuwa alimchafua umbu lao Dina;
14
kwa hiyo wakasema na kuwaambia: Hatuwezi kulifanya jambo hili, tumpe mtu mwenye govi umbu letu, kwani hivi vitatutia soni.
15
Tutaweza kuwaitikia neno hilo hapo tu, mtakapokuwa kama sisi, kwenu wa kiume wote wakitahiriwa.
16
Ndipo, tutakapowapa wana wetu wa kike, tujichukulie nao wana wenu wa kike, tukae pamoja nanyi kuwa kabila moja.
17
Lakini msipotusikia na kutahiriwa, tutamchukua mtoto wetu, twende zetu.
18
Haya maneno yao yakawa mema machoni pake Hamori napo machoni pake Sikemu, mwana wa hamori.
19
Huyu kijana hakukawa kulifanya neno hilo, kwani alipendezwa naye binti Yakobo; naye alikuwa mwenye macheo kuliko wote a mlango wa baba yake.
20
Hamori na mwanawe Sikemu walipofika langoni pa mji wao wakasema na watu wa mji wao kwamba:
21
Watu hawa wanataka kukaa kwetu katika nchi yetu na kutengemana, wachuuzie huku; nanyi mnaiona nchi hii kuwa pana huku na huko, waenee nao; wana wao wa kike tutajichukulia kuwa wake zetu, nao wana wetu wa kike tutawapa wao.
22
Lakini liko neno moja, watu hawa wanalolitaka, wapate kutuitikia na kukaa kwetu, tuwe kabila moja, ni hili: Kwetu wa kiume wote watahiriwe, kama wenyewe walivyotahiriwa.
23
Je? Hivyo makundi yao na mapato yao na nyama wote, wanaowafuga, hawatakuwa mali zetu sisi? Kwa hiyo na tuwaitikie, wakae kwetu!
24
Wote waliotoka langoni pa mji wakamsikia Hamori na mwanawe Sikemu, wakatahiriwa wa kiume wote pia, ndio wao wote waliotoka langoni pa mji wake.
25
Ikawa siku ya tatu, walipokuwa wanaumwa sana, wana wawili wa Yakobo, Simeoni na Lawi, ndugu zake Dina, wakachukua kila mtu upanga wake, wakaingia mle mjini, watu walimokaa na kutulia, wakawaua wa kiume wote.
26
Naye Hamori na mwanawe Sikemu wakawaua kwa ukali wa panga, kisha wakamchukua Dina nyumbani mwa Sikemu, wakatoka kwenda zao.
27
Ndipo, wana wengine wa Yakobo walipowajia wale waliouawa, wakaziteka mali za humo mjini, kwa kuwa walimchafua umbu lao.
28
Wakawachukua mbuzi na kondoo wao na ng'ombe wao na punda wao nayo yaliyokuwamo mjini nayo yaliyokuwako mashambani.
29
Wakateka mali zao zote na wana wao wote na wake zao, nayo yote yaliyokuwamo nyumbani wakayanyang'anya.
30
Naye Yakobo akamwambia Simeoni na Lawi: Mmenipatia mabaya, mmefanya mnuko wangu kuwa mbaya kwao wanaokaa katika nchi hii, kwa Wakanaani na Waperizi, nami watu wangu wanahesabika upesi. Watakaponikusanyikia, watanipiga; ndivyo, nitakavyotoweka mimi na mlango wangu.
31
Lakini wakasema: Je? Tungeacha tu, amtumie umbu letu kama mwanamke mgoni?
← Chapter 33
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 35 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50