bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Genesis 44
Genesis 44
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 43
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 45 →
1
Yosefu akamwagiza mkuu wa nyumba yake kwamba: Magunia ya watu hawa yajaze vilaji, kama wanavyoweza kuchukua, nazo fedha za kila mtu ziweke juu ndani ya gunia lake!
2
Namo juu ndani ya gunia lake mdogo tia pamoja na fedha zake za ngano kikombe changu, hicho kikombe cha fedha. Akafanya hivyo, kama Yosefu alivyomwagiza.
3
Asubuhi kulipopambazuka, wakapewa ruhusa kwenda zao, wao na punda wao.
4
Walipokwisha kutoka mjini na kwenda mbali kidogo, ndipo, Yosefu alipomwambia mkuu wa nyumba yake: Ondoka, uwafuate hao watu na kupiga mbio! Utakapowapata waambie: Mbona hayo mema mliyofanyiziwa mnayalipa na kufanya mabaya?
5
Kumbe hicho kikombe sicho, bwana wangu alichokinywea? Tena hukitumia cha kuagulia. Haya mliyoyafanya ni mabaya.
6
Alipowapata akawaambia maneno yayo hayo.
7
Wakamwambia: Kwa nini bwana wetu anasema maneno kama hayo? Yasiwajie watuma wako maneno kama hayo, wayafanye!
8
Tazama! Hizo fedha, tulizoziona juu ndani ya magunia, tumezirudisha kwako toka nchi ya Kanaani. Tutawezaje kuiba fedha au dhahabu nyumbani mwa bwana wako?
9
Atakayeonekana kuwa nacho miongoni mwao watumwa wako na afe! Nasi tutakaopona tutakuwa watumwa wake bwana wetu.
10
Akaitikia kwamba: Basi, na viwe hivyo, kama mlivyosema! Atakayeonekana kuwa nacho, atakuwa mtumwa wangu, nanyi wengine mtakuwa hamna kosa.
11
Wakashusha upesi chini kila mtu gunia lake, wakafungua kila mtu gunia lake.
12
Naye yule mtu alipotafuta akaanza kwake mkubwa, akamaliza kwake mdogo; ndipo, kikombe kilipooneka katika gunia la Benyamini.
13
Ndipo, wote walipozirarua nguo zao, wakawachukuza tena kila mtu punda wake mzigo ake, wakarudi mjini.
14
Yuda na ndugu zake walipoingia nyumbani mwa Yosefu, naye alikuwa angalimo bado, nao wakamwangukia chini.
15
Yosefu akawaambia: Ni tendo gani hilo, mlilolitenda? Hamjui, ya kuwa mtu kama mimi huangua?
16
Yuda akajibu: Tumwambie nini bwana wetu? Tusemeje? Tutawezaje kujikania? Mngu anayaumbua maovu, watumwa wako waliyoyafanya; tazama, sisi pamoja naye aliyeonekana kuwa nacho hicho kikombe mkononi mwake tu watumwa wako.
17
Naye akasema: Hili lisinijie, nifanye tendo kama hilo! Yule mtu aliyeoneka kuwa nacho hicho kikombe mkononi mwake yeye tu atakuwa mtumwa wangu, nanyi wengine nendeni na kutengemana kwa baba yenu!
18
Ndipo, Yuda alipomkaribia na kumwambia: Tafadhali, bwana wangu, mtumwa wako na aseme neno masikioni pake bwana wangu! Makali yako yasimwakie mtumwa wako! Kwani wewe unalingana na Farao.
19
Bwana wangu alipowauliza watumwa wake kwamba: Mna baba au ndugu?
20
tukamwambia bwana wangu: Tuna baba, naye ni mzee, naye mtoto wa uzee wake yuko, lakini ndugu yake amekufa, akaachwa yeye peke yake wa mama yake, kwa hiyo baba yake anampenda.
21
Ukawaambia watumwa wako: Sharti mmtelemshe, afike kwangu, nipate kumwona kwa macho yangu.
22
Nasi tukamwambia bwana wangu: Huyu kijana hataweza kumwacha baba yake; akimwacha baba yake, huyo atakufa.
23
Ukawaambia watumwa wako: Ndugu yenu mdogo asipotelemka pamoja nanyi, hamtauona uso wangu tena.
24
Tulipopanda kwenda kwa mtumwa wako, baba yangu, tukamsimulia hayo maneno ya bwana kidogo!
25
Kisha baba yetu alipotuambia: Rudini kutununulia vilaji wangu!
26
Tukasema: Hatuwezi kutelemka; lakini ndugu yetu mdogo akienda pamoja nasi, tutatelemka; kwani hatuwezi kuuona uso wake yule mtu, ndugu yetu mdogo asipokuwa nasi.
27
Ndipo, mtumwa wako baba yangu alipotuambia: Ninyi mnajua, ya kuwa mke wangu alinizalia wana wawili;
28
mmoja alipoondoka kwangu, nikasema: Ameraruliwa na nyama, maana sikumwona tena mpaka sasa.
29
Sasa mkimchukua huyu naye na kumtoa kwangu, akipatwwa na kibaya njiani, mtanisukuma mimi mwenye mvi kushuka kuzimuni kwa kuyaona hayo mabaya.
30
Kama ningefika kwa mtumwa wako, baba yangu, tusipokuwa naye huyu kijana, ambaye roho ya baba ilifungamana nayo roho yake,
31
baba akaona, ya kuwa hayuko, angekufa papo hapo, nasi watumwa wako tungekuwa tunamsukuma mtumwa wako, baba yetu, mwenye mvi kushuka kuzimuni na kusikitika.
32
Kwani mimi, mtumwa wako, nimejitoa kwa baba kuwa mdhamini wake huyu kijana, nikamwambia: Nisipomrudisha kwako, nitakuwa nimemkosea baba yangu siku zote.
33
Sasa mtumwa wako na akae mahali pake huyu kijana kuwa mtumwa wa bwana wangu, naye huyu kijana na apande na kaka zake kwenda kwao!
34
Kwani nitawezaje kupanda kwenda kwa baba yangu, huyu kijana asipokuwa pamoja na mimi? Sitaweza kuyaona hayo mabaya yatakayompata baba yangu.
← Chapter 43
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 45 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50