bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Genesis 21
Genesis 21
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 20
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 22 →
1
Bwana akamkagua Sara, kama alivyosema; naye Bwana akamfanyizia Sara, kama alivyomwagia.
2
Kwa hiyo Sara akapata mimba, akamzalia Aburahamu mtoto mume katika uzee wake siku zizo hizo, Mungu alizomwagia.
3
Mwanawe aliyezaliwa, Sara aliyemzaa, Aburahamu akamwita jina lake Isaka (Acheka).
4
Huyu mwanawe aburahamu akamtahiri, alipokuwa mwenye siku nane, kama Mungu alivyomwagiza.
5
Naye Aburahamu alikuwa mwenye miaka 100, mwanawe Isaka alipozaliwa.
6
Naye Sara akasema: Mungu amenipatia kuchekwa, kwani kila atakayevisikia atanicheka.
7
Akasema tena: Yuko nani aliyemwambia Aburahamu: Sara atanyonyesha wana? Kwani nimezaa mwana katika uzee wake.
8
Mtoto alipokua akakomeshwa kunyonya; siku hiyo, Isaka alipoacha kunyonya, Aburahamu akafanya karamu kubwa.
9
Sara alipomwona yule mwana wa Mmisri Hagari, aliyemzalia Aburahamu kuwa mfyozaji,
10
Akamwambia Aburahamu: Mfukuze huyu kijakazi pamoja na mwanawe! Kwani mwana wa huyu kijakazi hatapata urithi pamoja na mwanangu Isaka.
11
Neno hili likawa baya sana machoni pake Aburahamu kwa ajili ya mwanawe,
12
lakini Mungu akamwambia Aburahamu: Neno hilo lisiwe baya machoni pako kwa ajili ya huyo kijana na huyo kijakazi wako! Yote, Sara atakayokuambia, mwitikie sauti yake! Kwani watakaoitwa uzao wako ni wa Isaka tu.
13
Lakini mwana wa kijakazi naye nitamweka kuwa taifa zima, kwani naye ni uzao wako.
14
Kesho yake Aburahamu akaamka na mapema, akachukua mkate na kibuyu cha maji, akampagaza Hagari begani, kisha akampa na mwanawe; ndivyo, alivyompa ruhusa kwenda zake. Lakini alipokwenda akapotea katika nyika ya Beri-Seba.
15
Maji yalipokwisha kibuyuni, akamwacha mwanawe chini ya kijiti,
16
akaenda kukaa peke yake na kumwelekea mbali kidogo kama hapo, mtu anapotupa mshale kwa upindi, kwani alisema: Nisione, mwana anavyokufa! Alipokaa hivyo na kumwelekea akapaza sauti yake, akalia.
17
Mungu alipokisikia kilio cha mtoto, malaika wa Mungu akamwita Hagari toka mbinguni, akamwambia: Una nini, Hagari? Usiogope! Kwani Mungu amekisikia kilio cha mtoto hapo, anapolala.
18
Inuka, umwinue mtoto na kumshika kwa mkono wako! Kwani nitamfanya kuwa taifa kubwa.
19
Kisha Mungu akamfumbua macho; ndipo, alipoona kisima cha maji, akaenda kukijaza kile kibuyu, akampa mtoto, anywe.
20
Mungu akawa na huyu mtoto, akakua, akakaa nyikani, akawa mpiga upindi.
21
Akakaa katika nyika ya Parani; naye mama yake akamwoza mwanamke wa nchi ya Misri.
22
Ikawa wakati huo, ndipo, Abimeleki na Pikoli, mkuu wa vikosi vyake, walipomwambia Aburahamu kwamba: Mungu yuko pamoja na wewe katika mambo yote, unayoyafanya.
23
Sasa niapie na kumtaja Mungu kwamba: Hutanidanganya mimi wala wao wa uzao wangu wajao nyuma yangu, ila huo wema, niliokufanyia wewe, unifanyie mimi nayo nchi hii, unayoikaa ugeni!
24
Aburahamu akasema: Basi, mimi nitaapa.
25
Kisha Aburahamu akamwonya Abimeleki kwa ajili ya kisima cha maji, watumishi wake Abimeleki walichokinyang'anya.
26
Naye Abimeleki akasema: Simjui aliyelifanya jambo hilo, wewe nawe hujanipasha habari, mimi nami sijavisikia, ni leo hivi tu.
27
Kisha Aburahamu akachukua mbuzi na kondoo na ng'ombe, akampa Abimeleki; hivyo ndivyo, wao wawili walivyofanya agano.
28
Aburahamu akaweka wana kondoo saba peke yao,
29
naye Abimeleki akamwuliza Aburahamu: Hawa wana kondoo saba ukiwaweka peke yao, ni wa nini?
30
Akajibu: Hawa wana kondoo saba wa kike wachukue mkononi mwangu, upate kunishuhudia, ya kuwa nilikichimbua kisima hiki.
31
Kwa sababu hii wakapaita mahali pale Beri-Seba (Kisima cha Kiapo), kwa kuwa waliapiana hapo wote wawili.
32
Walipokwisha kulifanya agano hilo hapo Beri-Seba, Abimeleki na Pikoli, mkuu wa vikosi vyake, wakaondoka, wakarudi katika nchi ya Wafilisti.
33
Aburahamu akapanda mvinje hapo Beri-Seba, akalitambikia hapo Jina la Bwana aliye Mungu wa kale na kale.
34
Aburahamu akakaa ugenini katika nchi ya Wafilisti siku nyingi.
← Chapter 20
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 22 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50